Nasumbuka sana wakuu mwenye kujua Tiba ya vidonda vya tumbo anijuze

Nasumbuka sana wakuu mwenye kujua Tiba ya vidonda vya tumbo anijuze

Nitangulize salam kwanza kwa ndugu wote wana jamii forum, kama kichwa cha Habari hapo juu kinavoeleza, ninasumbuliwa na vidonda vya tumbo huu mwaka wa 6 naomba kwa yoyote anayefaham dawa au ameshatumia dawa amepona anifahamishe na mimi niondokane na hiii karaha, , nipo mwanza, natanguliza shukran kwa yeyote atakayenijuza
Wala usihangaike, nakuanzisha tiba sasa hivi. Chukulia umeshapona. Be happy.

Anza kula mizizi ya mgomba mibichi, na yake magamba ya toto la mgomba (yale ) laini yanayolika> Osha vizuri mizizi kula kutwa mara tatu. Na yale magamba kula mara kwa mara.

Nipe majibu ndani siku tano, kama bado tumbo linakusumubuwa, ntakuongezea na mzizi mwengine wa kuchanganya, ulete mrejesho hapahapa JF, hiyo haijawahi kushindwa vidonda vya tumbo, hata vile sugu.

Wacha kula maharage mpaka utakapopona kabisa.
 
Epuka kukaa na njaa muda mrefu
Epuka soda na alcohol
Acha chakula jamii ya maharage, ndizi za kuiva, vyakula vya kukaanga na kurosti, maziwa fresh.
Hapo kwenye soda tu ndio sipo, ila Hivi ndio vyakula tajwa navyokula sana sana, na cha kustaajabisha sina nidhamu ya kula kabisa yaani hata nikipitisha siku bila kunywa chai na kuchelewa kula chakula cha mchana bado nadunda na vidonda vya tumbo ni historia. Na miaka ni Robo Karne + hivyo imepiga hatua.

Hapo sijaongelea mfungo wa majuma kadhaa ,kutimiza dini na maombi ya kawaida.

Nafikiri kuna vitu vya ziada vinavyosababisha vidonda vya tumbo ambavyo vinasababishwa na mwili wa mtu husika kureact na baadhi ya misosi
 
Mkuu dawa kuondoa gesi ni kutumia juisi ya viazi mbatata au ulaya changanya na bicarbonate ( chapa maandazi) kijiko kidogo cha chai kwenye juisi, chukua kiazi kimoja kisage kwa Brenda au grater saga chote tia maji vijiko vitatu ili juisi owe nzito meza na makapi yake ni vizuri zaidi hasa tumbo likiwa wazi, yaani hujala chochote, hasa asubuhi na JIONI UTAKUJA KUNISHUKURU siku Moja.
Maana halisi ya kuwa jamii forum, ubarikiwe sana mkuu
 
Wala usihangaike, nakuanzisha tiba sasa hivi. Chukulia umeshapona. Be happy.

Anza kula mizizi ya mgomba mibichi, na yake magamba ya toto la mgomba (yale ) laini yanayolika> Osha vizuri mizizi kula kutwa mara tatu. Na yale magamba kula mara kwa mara.

Nipe majibu ndani siku tano, kama bado tumbo linakusumubuwa, ntakuongezea na mzizi mwengine wa kuchanganya, ulete mrejesho hapahapa JF, hiyo haijawahi kushindwa vidonda vya tumbo, hata vile sugu.

Wacha kula maharage mpaka utakapopona kabisa.
shukrani Sana, Nina swali Tafadhali,mizizi ya mgomba pamoja na magamba ya mgomba mchanga yote natumia ndani ya siku Tano?
 
Samahani nauliza kufaham, Je, Mizizi pamoja na magamba ya mgomba nikitafuta naimeza ? Au nameza tu maji maji yake FaizaFoxy
 
Mtoa mada utapoteza pesa zako bureee kwanza kapime wingi wa gesi lakini anza na dozi ya bamia nakuhakikishia ndani ya miezi 6 utakua umepona kabisa fungu la bamia ni sh 500 tu
Hizi bamia unachemsha na kula au unazipika kawaida tu?
 
Hizi bamia unachemsha na kula au unazipika kawaida tu?
Unazikata kata vipande vidogo, unachemsha kwa dakika 3 tu zisikae sana jikoni, unakunywa hata mara 2 kwa siku, waeza kuweka na chumvi kiduuuuchu kupata ladha ukipenda
 
Hizi bamia unachemsha na kula au unazipika kawaida tu?
Kuna njia nyingine ya bamia mbichi unablend na maziwa fresh, nusu glass unakunywa asubuhi kabla hujala chochote na usiku nusu saa kabla hujala dinner..... inahitaji ujasiri sana ila wengi wamepona
 
Nitangulize salam kwanza kwa ndugu wote wana jamii forum, kama kichwa cha Habari hapo juu kinavoeleza, ninasumbuliwa na vidonda vya tumbo huu mwaka wa 6 naomba kwa yoyote anayefaham dawa au ameshatumia dawa amepona anifahamishe na mimi niondokane na hiii karaha, , nipo mwanza, natanguliza shukran kwa yeyote atakayenijuza
Njoo pm sichaji hata shilingi
 
Kama upo Dar, nitakuunganisha na kijana wangu, akupeleke kwa mzee ambae yupo kibamba.

Anai amewapeleka watu, wamepona sasa wanakula maharage na Dagaa kama zamani, garama za dawa ni 50,000.
Mkuu kuwa serious watu wengi tunasumbuliwa na vidonda tumetibiwa hospitali bila mafanikio. Ni kweli huyo mtu anatibu? Una ushahidi?

Nimeishatibiwa na wataalamu wengi wa tiba asili bila mafanikio
 
Kuna njia nyingine ya bamia mbichi unablend na maziwa fresh, nusu glass unakunywa asubuhi kabla hujala chochote na usiku nusu saa kabla hujala dinner..... inahitaji ujasiri sana ila wengi wamepona
Kwa muda gani mkuu?
 
Vidonda vya tumbo pambana sana na gesi tumboni kwa kuangalia aina ya chakula ambacho unakula. Usipende kutumia vyakula vyenye Acid tumia zaidi vyakula vya Base. Asali maziwa fresh, nyama nyekundu, utumiaji wa nyanya kwa wingi achana nao kabisa
Mkuu kwani gesi ndio chakula cha H. Pilori kwamba ukiondoa gesi watakufa?

Naona hapa tunachanganya mada ndugu zangu. Vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na H. Pilori tiba yake ni kuwaua hawa bacteria ama kwa dawa za hospitali au dawa za asili.

Tunapoongelea vidonda vya tumbo tujaribu kutofautisha hivi vitu viwili jamani.
 
Nitangulize salam kwanza kwa ndugu wote wana jamii forum, kama kichwa cha Habari hapo juu kinavoeleza, ninasumbuliwa na vidonda vya tumbo huu mwaka wa 6 naomba kwa yoyote anayefaham dawa au ameshatumia dawa amepona anifahamishe na mimi niondokane na hiii karaha, , nipo mwanza, natanguliza shukran kwa yeyote atakayenijuza
Habari yako mkuu pole sana kwa maradhi yako yanayo kusumbuwa nitafute kwa wakati wako ili niweze kukutibu maradhi yako upate kupona uguwa pole.
 
Mkuu kuwa serious watu wengi tunasumbuliwa na vidonda tumetibiwa hospitali bila mafanikio. Ni kweli huyo mtu anatibu? Una ushahidi?

Nimeishatibiwa na wataalamu wengi wa tiba asili bila mafanikio
Kuna mtu, alihitaji kuunganishwa na mtabibu, ila akawa na shaka 50,000 yake, shida hapa ni mtu kuhofia kupoteza pesa yake.
 
Kuna mtu, alihitaji kuunganishwa na mtabibu, ila akawa na shaka 50,000 yake, shida hapa ni mtu kuhofia kupoteza pesa yake.
Nani aliyewahi kushuhudia mgonjwa wa H. Pilori anaponeshwa na huyo mganga?
 
Tengeneza juice mixer ya bamia na tango kunywa mara 2 kwa siku jitahidi ule kwa wakati.
 
Back
Top Bottom