Natafuta mchumba wa kiume, awe anaishi London

Natafuta mchumba wa kiume, awe anaishi London

Shida ya wanawake wa sasa wanatafuta mfanyakazi au mfanyabiashara kwenye ndoa. Badala ya kutafuta mume ndiyo maana hamuolewi.
Hata akikuoa siku akifukuzwa kazi au biashara zikiyumba utamkimbia. Mnatanguliza masilahi mbele kuliko utu.
Kumbuka ndoa ni maisha halisi. Kuna kufukuzwa kazi, biashara kuyumba au kuugua. Utaweza kuvumilia hayo ikiwa uliingia kwenye ndoa kwasababu mumeo ni muajiriwa, amejiajiri au mfanyabiashara? Maneno ya busara yamenukuliwa kutoka Kwa Wong Fei
Well said ,[emoji108][emoji108]
 
Lakini atapata na ataolewa Mkuu....Mamdogo wangu kafunga harusi mwaka Jana akiwa na 43 .palipo na mwanamke aliyechelewa kuolewa,pana mwanaume pia aliyechelewa kuoa
Issue ni vigezo na masharti. Wanaoolewa ni Wale wanaotarajiwa kumpata mwenzi yeyote ili Mradi anapumua[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
HUko uliko hamna wanaume? Kama huko ulaya kote na unapofanyia kazi umeshindwa kupata basi wewe utakua una makandokando mengi KWAIO umeshindikana, mana miaka 40+ lazima una shida
Umeiacha london unakuja kwenye mitandao ya kijamii [emoji3]
 
Mimi nakuheshimu na wewe jiheshimu, hunijuu sikujui. Nisema wako watanzania wezangu lakini ni miji mbali mbali na pia mimi sio mtokaji saana kwa hiyo sijaona shida kutumia jukwaa hili.
Na kabla ya hapo nimeshawahi kuolewa na kabila tofauti kwa hiyo wacha kujaji watu.
Na kazini hata njiani pia wako makabila mengine mimi sitaki hao. Ahsante saaana
Hapa umejidhihirisha una shida kubwa sana. Hio miji haifikiki? Wewe unajifungia ndani 24/7? Huko unakofanya kazi hamna wanaume? Hadi miaka 40 ulikua unafanya nini kama si una shida? Kwanini uwakatae wa huko uliko, udhanie kwenye mitandao ya kijamii ndio uwapate, Au nyie ndio wanawake wa beijing?
 
Nahisi hutaki kunifahamu nishajibu tayari yote.
Na juwa kuheshimu WATU ndio ungwana.
Ukiambiwa ukweli unakimbilia heshima uheshimiwe..Ushauri wa bure, badilika na badilisha mindset yako na tabia yako, la sivyo miaka 50 utajikuta bado unachagua chagua
 
Sasa mimi wa Tandahimba huku nitaoa kweli kwa hali hii?
 
Mimi ni wanamke ninae penda kuwa na amani na furaha wakati wote. Natafuta mchumba atakaekuwa
pia anataka kuwa kwenye ndoa.

Mimi sina watoto ambae pia hana watoto. Najitahidi kuwa kwenye misingi ya dini na ambae pia yuko kwenye misingi ya dini.

Naipenda kazi yangu na nahitaji mume wangu mtarajiwa pia awe anafanya kazi. Naishi London, natoka Zanzibar, nafanya kazi ya ofsini mimi ni meneja wa ofisi, tunahusika na uhasibu.

Nina miaka 41, nahitaji mume wangu mtarajiwa awe na miaka kuanzi 41, muislamu na awe anaishi London pia,
rangi sio tatizo lakini awe kanizidi urefu, mimi ni 5'2".

Ahsanteni sana.
Unataka aliyeko London, kutoka kwenu Zenji humtaki?

Mtu una miaka 41, bado unaweka masharti kibao!? Utaehani wewe ndiye mfungua mlango wa mbinguni? Hadi kuja humu maana yake umesubiri weee, ukaona umri unakimbia.

Omba Mungu akujaalie mume mwema.
 
Unataka aliyeko London, kutoka kwenu Zenji humtaki?

Mtu una miaka 41, bado unaweka masharti kibao!? Utaehani wewe ndiye mfungua mlango wa mbinguni? Hadi kuja humu maana yake umesubiri weee, ukaona umri unakimbia.

Omba Mungu akujaalie mume mwema.
Kuna tatizo gani kutaka kutoka London lakini awe mtazania mwezangu.
 
Unataka aliyeko London, kutoka kwenu Zenji humtaki?

Mtu una miaka 41, bado unaweka masharti kibao!? Utaehani wewe ndiye mfungua mlango wa mbinguni? Hadi kuja humu maana yake umesubiri weee, ukaona umri unakimbia.

Omba Mungu akujaalie mume mwema.
Nani aliyokwambia nimesubiri tu miaka yote.
 
Back
Top Bottom