Kwanza hali zenu nyote na ni wazima pia,
najitahidi mnooo kuheshimu kila mtu lakini
huu mkasa ulionikuta siku chache tu baada ya kujiunga hapa nahisi bora
niulize kuwa siamini kabisa.
Naombeni mnijuze kama pia mna Wanaijiria humu, mbona naaza kuombwa pesa na mbaba mmoja.
Nauliza kama pia Mnawanaijiria humu kuwa bado siamni kabisa, au hii ni tabia
ya (baadhi) wa kina baba/kaka wa kitanzania, kuwaomba pesa kina mama/dada.
Labda kuwa maisha yamebadilika sasa saana huko nyumbani kwa hiyo (baadhi) ya kina baba/kaka sasa pia wanawaomba pesa kina mama/dada??
“Mimi nilisema nafanya kazi kwa hiyo nahitaji mume wangu mtarajiwa pia awe anafanya kazi” Hii namaanisha kuwa sitegemei pesa za mume wangu mtarajiwa kuwa nina zangu, kwa hiyo na yeye pia awe anafanya kazi/biashara ili tusaidiane maisha kwa pamoja ili pia asitegemee pesa zangu mimi tu!!
Lakini sasa nimeanza kuogopa mnooo kwa kuanza kuombwa pesa hapa mtandaoni ( kwa mtu ambae simjui kabisa mbali ya kuchat nae hapa jukwaani tu) baada ya matusi yote niliyotukanwa na kuhukumiwa mnoooo na ( baadhi ya) kina kaka/baba, hata bila ya kufahamu nini nimewakosea.
Vile vile nashindwa kuelewa sasa kuwa
( baadhi ) ya kina baba/kaka humu wanasema kuwa kina dada/mama wanawafanyeni nyinyi chuma ulete.
Kwa hiyo sasa (baadhi yenu) nyinyi humu mnataka kutufanya sisi sasa kina mama/dada chuma ulete!! Au tuseme bibi kizee mimi tu labda kwa sasa. 🤣😂
Naombeni mnijuze kama pia mna Wanajiria humu au hii ni tabia pia ya
(baadhi) wa kina kaka/baba wa kitanzania kuwachuna/kuwatapeli wanawake. 🙏🙏
Chengine jamani mimi siajiri watu kazi na wala sijui sheria za kazi huku niliko London. Mimi ninaukaazi wa huku na nafanya kazi zaidi ya hapo sijui sheria nyengine. Kama nilivyosema mimi nilikuja huku nikiwa mdogo kwa hiyo siwezi kumpa mtu yoyote ushauri kuhusu sheria za huku za kazi, vizuri mutizame nyinyi huko kwenye online au mmuajiri wakili akuelezeeni.
Nasema haya kuhusu sheria za kazi kuwa sitaki kusema kitu nisichokijua au kumpotosha mtu yoyote. 🤦🏽♀️🤦🏽♀️
Vile vile nimeona pia ( baadhi ) ya wa kina kaka/baba kutaka urafiki na mimi sasa, niwe muwazi na kusema la ukweli kabisa ili tusipotezeane muda hapa, hasa kuwa niko bizi mnooo na maisha yangu, mimi sio mtu wa marafiki na sina marafiki wa kiume.🙄😳
Mimi niko hapa kutafuta mume tu na mwenye vigezo vyote, na kama hamna ni sawa pia hama shida hata kidogo, bali nitabaki kwa kusoma threads za watu wengine nitakapo kuwa na muda
ili kujifuza na kufahamu hali ya huko nyumbani sasa.🙏🙏