Natafuta mchumba wa kiume, awe anaishi London

Natafuta mchumba wa kiume, awe anaishi London

Mimi ni wanamke ninae penda kuwa
na amani na furaha wakati wote.

Natafuta mchumba atakaekuwa
pia anataka kuwa kwenye ndoa. Mimi sina watoto ambae pia hana watoto.

Najitahidi kuwa kwenye misingi ya dini na ambae pia yuko kwenye misingi ya dini. Naipenda kazi yangu na nahitaji mume wangu mtarajiwa pia awe anafanya kazi.

Naishi London, natoka Zanzibar, nafanya kazi ya ofsini mimi ni meneja wa ofisi, tunahusika na uhasibu.

Nina miaka 41, nahitaji mume wangu mtarajiwa awe na miaka kuanzi 41, muislamu na awe anaishi London pia,
rangi sio tatizo lakini awe kanizidi urefu, mimi ni 5'2". Vile vile awe Mswahili/mzanzibari/Mtanzania mwezangu.

Ahsanteni saaana
Zanzibar2014

Upendo hauna vigezo, punguza masharti
 
Lakini atapata na ataolewa Mkuu....Mamdogo wangu kafunga harusi mwaka Jana akiwa na 43 .palipo na mwanamke aliyechelewa kuolewa,pana mwanaume pia aliyechelewa kuoa
Asilimia ni ndogo sana kwa wanawake kuolewa katka umri mkubwa kuanzia 35+ na hasa kwa sisi Waafrika.

Huyo ndugu yako ilikuwa bahati yake tu. Katika wanawake 10 wa umri huo ni mmoja 5 tu ndio anaweza olewa ( 1:10). Tena awe na vizuri financially.
 
Dah sifa zote nnazo kasoro kuishi london...Je sisi wa Leeds huku unatufikiria?
 
Mm ni mstaafu lakini bado nina nguvu za kunyandua kwa kasi ya 5G.
Nina taaluma nyingi ikiwemo CPA(T)
Ikikupendeza njoo PM tuyajenge.
 
Nimesoma comment anazoreply mleta uzi daah, wazanzibar mnamajibu yasiyoumiza kwa maswali yanayochefua...Utapata mumee ila utafika umechoka mno, mm nimekosa vigezo vyotee ila nimepanda ustaarabu wako!
 
Ikawe kheri kwako.
Ukipata watatu nigaie mmoja ila awe wa huko London
 
Mimi ni wanamke ninae penda kuwa na amani na furaha wakati wote. Natafuta mchumba atakaekuwa
pia anataka kuwa kwenye ndoa.

Mimi sina watoto ambae pia hana watoto. Najitahidi kuwa kwenye misingi ya dini na ambae pia yuko kwenye misingi ya dini.

Naipenda kazi yangu na nahitaji mume wangu mtarajiwa pia awe anafanya kazi. Naishi London, natoka Zanzibar, nafanya kazi ya ofsini mimi ni meneja wa ofisi, tunahusika na uhasibu.

Nina miaka 41, nahitaji mume wangu mtarajiwa awe na miaka kuanzi 41, muislamu na awe anaishi London pia,
rangi sio tatizo lakini awe kanizidi urefu, mimi ni 5'2".

Ahsanteni saaana
Nakuombea upate hitaji la moyo wako.

Mungu ni mwema
 
Inaonyesha bibie kama kweli upo ng'ambo si mtu wa kujichanganya sana.

Hadi kubeba box hujui maana yake, kweli?
Samahani kwa kweli sikufahamu vizuri. Na Ni kweli muda mwingi niko kazini sio sana kuwa na watu, ahsante saana.
 
Back
Top Bottom