Natafuta mchumba wa kiume, awe anaishi London

Natafuta mchumba wa kiume, awe anaishi London

Mimi ni wanamke ninae penda kuwa
na amani na furaha wakati wote. Natafuta mchumba atakaekuwa
pia anataka kuwa kwenye ndoa.

Mimi sina watoto ambae pia hana watoto. Najitahidi kuwa kwenye misingi ya dini na ambae pia yuko kwenye misingi ya dini.

Naipenda kazi yangu na nahitaji mume wangu mtarajiwa pia awe anafanya kazi. Naishi London, natoka Zanzibar, nafanya kazi ya ofsini mimi ni meneja wa ofisi, tunahusika na uhasibu.
Nina miaka 41, nahitaji mume wangu mtarajiwa awe na miaka kuanzi 41, muislamu na awe anaishi London pia,
rangi sio tatizo lakini awe kanizidi urefu, mimi ni 5'2".

Ahsanteni saaana
Kila laheri bibie. Mungu akujalie hitaji la moyo wako.
 
Du! Sasa Miaka 41yrs bado Unachagua? Nchi yenyewe England, Maisha yako bado ni magumu hauna unafuu wowote Angalia utazeeka na utamu wako
Wewe chukua chochote kinachokuja wacha kuchambua mdogo wangu
Sawa nimekusikia, ahsante saana.
 
Upo UK Sehemu gani Mimi. Namjua Mtu yupo Barmigam anafundisha university of bath

Pia kigezo Cha dini Hakina maana kitoe la sivyo utaangaika Sana na uo umri wako. Maana watz wengi hapo UK Ni ngumu amuache demu wa kizungu wa 40+ ili atafute Mbongo

Andika tangazo upya

Sema upo na 40+ yrs
Unataka Mwanaume anayeishi Jiji flani hapo UK
Ondoa kigezo Cha dini hapo
 
Samahani kama ushauri wangu utakuwaza, BT mume au mke hupatikani katika mazingira yanayo kuzunguka lakini humu watakudhihaki unless nawe unafurahisha jukwaa but mumeo anapatikana katika mazingira yako yanayo kuzunguka, either marafiki, majirani , business partners na n.k ,so usiwachukulie poa hangaika nao hao utanishukuru, coz wengi utapima vigezo vyako kiuhalisia BT sie huku tutakudangaja kwa sababu hatujuani kiundani. Mungu akutangulie katika safari yako inshallah!!,
Sawa ahsante sana
 
Mimi ni wanamke ninae penda kuwa na amani na furaha wakati wote. Natafuta mchumba atakaekuwa
pia anataka kuwa kwenye ndoa.

Mimi sina watoto ambae pia hana watoto. Najitahidi kuwa kwenye misingi ya dini na ambae pia yuko kwenye misingi ya dini.

Naipenda kazi yangu na nahitaji mume wangu mtarajiwa pia awe anafanya kazi. Naishi London, natoka Zanzibar, nafanya kazi ya ofsini mimi ni meneja wa ofisi, tunahusika na uhasibu.

Nina miaka 41, nahitaji mume wangu mtarajiwa awe na miaka kuanzi 41, muislamu na awe anaishi London pia,
rangi sio tatizo lakini awe kanizidi urefu, mimi ni 5'2".

Ahsanteni saaana
Mwenyezi Mungu atimize hitaji la moyo wako.
 
Upo UK Sehemu gani Mimi. Namjua Mtu yupo Barmigam anafundisha university of bath

Pia kigezo Cha dini Hakina maana kitoe la sivyo utaangaika Sana na uo umri wako. Maana watz wengi hapo UK Ni ngumu amuache demu wa kizungu wa 40+ ili atafute Mbongo

Andika tangazo upya

Sema upo na 40+ yrs
Unataka Mwanaume anayeishi Jiji flani hapo UK
Ondoa kigezo Cha dini hapo
Sawa nimekusikia, lakini niseme tu, kuwa na imani ni muhimu kwangu. Ahsante saana.
 
Back
Top Bottom