Poleni na majukumu ya kila siku
Nimekuja na ID yangu hii sina haja ya kujificha
Moja kwa moja kwenye mada,nahitaji msaada kama kuna mtu anamjua mganga wa uhakika anifanyie kazi yangu, kuna waganga huwa nasikia wanatoa watu mabusha, wanatuma majini au kumpa mtu ugonjwa nahitaji mganga wa hivyo
Hii dunia ina mengi,na ikifika kipindi cha vita unaambiwa usichague silaha,nahitaji jambo langu likamilike kwasababu kuna watu wanaweza kukukosea heshima mpaka wakapitiliza, ukimya na subira ni muhimu lakini kuna watu huwa wanaona kama umezubaa
Nikifanikiwa kazi yangu nitakupa ya shukrani sina hiyana
Watu wa mahubiri hapa sio sehemu yake.
Nawashukuruni naamini nitapata msaada wenu