Renegade
JF-Expert Member
- Mar 18, 2009
- 7,221
- 6,940
Kwa kweli Uchawi ni Imani ya Mtu, Lakini kWaamini MUNGU wana nguvu kuliko uchawi! Usiombe kukutana na watu wa namna hii, kuna watu wanapendwa na Mungu,wanalindwa na Mungu mwenyewe.Na huo ndio ubaya wa ushirikina mtarogana mpaka muwe masikini
Mtu ukiingia katika haya mambo inabidi mfukoni uwe na pesa ya kutosha
Kuna stori nilishawahi kuiandika hapa,
Wakati fulani nilikuwa naishi na kufanya kazi upande wa pili, nikiwa uko kuna watu walikorofisha nikawasimamisha kazi, Wakaunda jopo kuniendea kwa mganga, nikasikia nikafanya maombi nikamaliza, ikapita.
Nyingine, Kulikuwa na mkakati wa kuniondoa kwenye nafasi yangu, akaletwa na mtu kabisa, Kuna mshikaji alikuwa rafiki sana, akanifuata na kuniomba anipeleke kwa Babu yake eti amesikia taarifa mbaya,Nilimwambia MUNGU niliyenaye anatosha, Ikapita, Japo nilifanyiwa vitimbi sana lakini mpaka leo namshukuru MUNGU nimeshinda.