Natafuta mji mtulivu wa kwenda kupumzika kwa mwezi mmoja

Nenda Bukoba utafurahi maisha kuna beach nzuri sana zenye mvuto was kipekee, kuna Bunena Beach, beach ya asili yenye mawe mazuri sana, unakaa juu ya maweza unausikilizia upepo mwanana kutoka ziwa Victoria hakuna kelele wala nini, vilevile kuna beach ya Kiloyera in nzuri hakuna mfano, kuna beach ya Bukoba Club hakika huu mji unapendeza sana. Halafu mjini katikati hamna cha foleni wala nini vyakula vya asili vipo vya kutosha na gharama ni za kawaida sana.

Binafsi hayo mazingira niliyapenda sana zaidi ule mji una amani na usalama kuliko miji yote niliyowahi kutembelea hapa Tanzania. Bukoba na viunga vyake hata usiku wa manane unatembea bila shida yoyote ile. Tatizo wanapenda sana kuongea kihaya kuliko lugha yoyote ile.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja ule mji hauna heka heka plus kuna sehemu kibao za evening walk.
Huwa napenda pia kwenda kuna beach hotel mbili napenda kushinda hapo.
Wish nitume picha nikiwa hapo [emoji12]
Hakika.
Bukoba ni mji ambao una mandhari nzuri sana, kijani karibu muda wote wa mwaka, hali ya hewa ni safi, Watu wa bukoba ni waungwana sana(japo wanapendana zaidi wao kwa wao..ukitaka wakuelewe ujue lugha yao😜)
Pia huo mji hauna watu wengi (msongamano). Bei ya vyakula ni ya chini..ila hawajui kupika lol.

Kwa ujumla Bukoba ni sehemu nzuri ya ku-refresh mind.
 
Wishes zimekuwa nyingi sasa. Emu tuma tuone labda na sisi tutakuwa inspired
 
Nenda Bagamoyo ukishidwa kwenda huko basi nenda Bukoba.
 
jaribu kwenda Pemba mkuu
 

Em mtendee haki Depal kwa kutuma picha 😊😊
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…