Natafuta mji mtulivu wa kwenda kupumzika kwa mwezi mmoja

Natafuta mji mtulivu wa kwenda kupumzika kwa mwezi mmoja

Nenda Bukoba utafurahi maisha kuna beach nzuri sana zenye mvuto was kipekee, kuna Bunena Beach, beach ya asili yenye mawe mazuri sana, unakaa juu ya maweza unausikilizia upepo mwanana kutoka ziwa Victoria hakuna kelele wala nini, vilevile kuna beach ya Kiloyera in nzuri hakuna mfano, kuna beach ya Bukoba Club hakika huu mji unapendeza sana. Alafu mjini katikati hamna cha foleni wala nini vyakula vya asili vipo vya kutosha na gharama ni za kawaida sana. Binafsi hayo mazingira niliyapenda sana zaidi ule mji una amani na usalama kuliko miji yote niliyowahi kutembelea hapa Tanzania. Bukoba na viunga vyake hata usiku wa manane unatembea bila shida yoyote ile. Tatizo wanapenda sana kuongea kihaya kuliko lugha yoyote ile.

Sent using Jamii Forums mobile app

😂😂😂😂 na kweli bukoba hadi mjini pale ni kihaya tu ila uzuri huwa wanakirimu sana wageni especially ukionesha hali ya kutaka kujifunza lugha tu au kukubali lifestyle yao.

Kwetu Kagera ila bukoba huwa naenda kwa nadra
 
Umofia kwenu wakuu!

Ambao mna uzoefu mkubwa na maeneo (miji midogo) ya nchi hii. Naomba ushauri au mapendekezo, ni mji gani mdogo naweza kwenda kukaa kwa muda wa mwezi mmoja (brain recharging)

Uwe ni mji mdogo, uliotulia kwa mandhari na hali ya hewa, ambao jioni naweza enjoy evening walk, uwe ni mji salama, na wenye vyakula vizuri vya asili, kwa mfanano mzuri think of somewhere like Lushoto (Lushoto ndio kwetu so don't mention)

Binafsi nimewaza kwenda Tarakea Rombo, lakini naona ni vyema nipate mawazo kwa wadau. N.B, iwe ni sehemu yenye nyumba za wageni ambazo ni classic.
Asanteni.
View attachment 1412207
Jaribu Kyela sehemu ipo ziwa nyasa inaitwa Matema beach,alafu unaibukia tukuyu mara moja moja.You won't regreat.
 
Chakechake panakufaa sana Mkuu. Ni mji mzuri. Utakunywa supu za aina zote, kuanzia samaki, mbuzi, ng'ombe na hata pweza ndo kwao.
 
Nenda Pangani ukatulie maeneo karibu na bahari ya Hindi maeneo ya Ushongo kule ukatulie Beach za Emayani, Mike hotel na Ushongo Beach Club.
 
Musoma, Tanga, kwa kutulia, chakula, usafi na usalama 100% jion unatembea hadi usk saa 6 bila mashaka then Bukoba, Iringa, Moshi hii ni kwa uzoefu wangu
 
Mkuu Bukoba it is!. Una beach, samaki, chakula cheap, mandhari, usafiri to and fro, usalama, totoz....
 
Uje na Chato mkuu hutajuta! Nitakupeleka mbuga ya kutengenezwa ya Burigi, Airport ya kisasa, mataaa ya barabarani pasipo magari mengi..... Vijiwe vya kahawa vya kisasa, utakula na kulala kwa gharama nafuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nenda bukoba kama walivosema walionitangulia ni sehem mzuri mwenyew nilipapenda sana.Sema wanaongea ki lugha balaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom