Natafuta mji mtulivu wa kwenda kupumzika kwa mwezi mmoja


πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ na kweli bukoba hadi mjini pale ni kihaya tu ila uzuri huwa wanakirimu sana wageni especially ukionesha hali ya kutaka kujifunza lugha tu au kukubali lifestyle yao.

Kwetu Kagera ila bukoba huwa naenda kwa nadra
 
Jaribu Kyela sehemu ipo ziwa nyasa inaitwa Matema beach,alafu unaibukia tukuyu mara moja moja.You won't regreat.
 
Chakechake panakufaa sana Mkuu. Ni mji mzuri. Utakunywa supu za aina zote, kuanzia samaki, mbuzi, ng'ombe na hata pweza ndo kwao.
 
Nenda Pangani ukatulie maeneo karibu na bahari ya Hindi maeneo ya Ushongo kule ukatulie Beach za Emayani, Mike hotel na Ushongo Beach Club.
 
Musoma, Tanga, kwa kutulia, chakula, usafi na usalama 100% jion unatembea hadi usk saa 6 bila mashaka then Bukoba, Iringa, Moshi hii ni kwa uzoefu wangu
 
Mkuu Bukoba it is!. Una beach, samaki, chakula cheap, mandhari, usafiri to and fro, usalama, totoz....
 
Uje na Chato mkuu hutajuta! Nitakupeleka mbuga ya kutengenezwa ya Burigi, Airport ya kisasa, mataaa ya barabarani pasipo magari mengi..... Vijiwe vya kahawa vya kisasa, utakula na kulala kwa gharama nafuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu nenda bukoba kama walivosema walionitangulia ni sehem mzuri mwenyew nilipapenda sana.Sema wanaongea ki lugha balaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…