Natafuta mji mtulivu wa kwenda kupumzika kwa mwezi mmoja

Bukoba pako poa sana mkuu chakula cha asili mpaka chips wanatengeneza kwa mayai ya kienyeji samaki fresh kabisa. Nyama choma kuku wa kienyeji na bei yake ni rafiki pia kuna hotel na lodge nzuri bei poa hari ya hewa na beach fresh, Pia ni wakarimu boda boda mpaka 500. Usalama unaweza kutembea kwa mguu mpaka asubuhi na usikutane kibaka wala jambazi kama alivosema mdau hapo juu. Nitarudi tena Bukoba
 
Mkuu nenda moshi eneo linaitwa HIMO. nikuzuri sana..nimeenda Mara nyingi..utafurahi..pia MARANGU kuzuri itafurahi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Himo pale jua kali Sana na joto la kutisha utafikiri uko kwenye Jangwa la Kalahari, pia kuna harufu chafu sana throughout the year inayotoka kwenye kiwanda cha ngozi cha Woisso. Himo hapafai hata kwa nukta moja bora Marangu...japo kwa mujibu wa mleta Uzi sehemu inayomfaa kwa mtazamo wangu ni Bukoba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimeeeecheeekaaaa eti boda boda jero

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata usicheke ndugu ule mjini ni mzuri mno japo watu wengi hawaufahamu, hata uteremke stend SAA saba usiku unaweza kushangazwa na bei za bodaboda, mfno sehemu ambapo ungepelekwa hata kwa elf tano au saba utashangaa unaambiwa book moja au mia tano na ukienda mbali sana utashangaa haizidi elf moja na mia tano. Bukoba niliipenda sana kuliko sehemu yoyote hapa Tanzania, changamoto ya mji wa Bukoba ni kwamba hadi mjini katikati lugha ya Kihaya inatumika sana, Wahaya wanapenda sana lugha yao na wala hawana tabia ya kuongeaongea kiswahili km sehemu nyingine. Nadhan wanaweza kuwa ndo kabila pekee hapa Tanzania linalo tumia kilugha kuliko kabila lolote hapa nchini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii Bukoba lazima ni nzuri,kila mtu anaizungumzia. Tatizo ni km 1000+ from Dar na utalii wa ndani unanoga kuendesha
 
Hii Bukoba lazima ni nzuri,kila mtu anaizungumzia. Tatizo ni km 1000+ from Dar na utalii wa ndani unanoga kuendesha
Sio mchezo utaenjoy sema kutoka dar ni safari kweli ila kama una private car utafanya utalii wa ndani mana unapita mikoa kama 6 Pwani,Morogoro,Dodoma,Singida,Tabora,Shinyanga,Geita then ndo Kagera yenyewe.
 
Ni kweli ilianzia bukoba wakiiga kutoka Uganda na safari mpaka ya karibu km 6 ni jero
 
Ni kweli wanapenda kuongea lugha yao.
 
Unatuzingua wewe...mwenda kupumnzika huqa amepanga na hana mbwembwe...nyie wenye vijihela vya nyanya kwa mbwembwe[emoji125]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unatuzingua wewe...mwenda kupumnzika huwa amepanga na hana mbwembwe...nyie wenye vijihela vya nyanya kwa mbwembwe[emoji125]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…