Natafuta mke tutakaye-adopt watoto pamoja naye


Ni mawazo yako mkuu. Nayaheshimu. Sijakata tamaa na nina amini Mungu atanipa watoto wangu mwenyewe kwa wakati tu. Ila in the mean time nataka ni-adopt. Wale wa kwangu wakija hata baada ya miaka 15 sawa tu.

Kuhusu kuachana na pepo na Mungu, nashindwa hata niseme nini? Lakini hapo ndipo tofauti yetu wanadamu ilipo. Naona hapo unamkufuru Mungu mkuu unaposema eti kama ananipenda kwa nini asingenipa mtoto. Ni sawa na kusema nimkimbilie shetani kwa sababu Mungu hajanitendea ninachotaka. Sitaki hata kusema zaidi.

Lakini wenye ushauri wa aina hii tafadhalini msinipe hata kidogo. Bakini nao. Mimi kwangu Mungu atabaki kuwa Mungu hata kama ataninyima vyote. Soma kitabu cha Ayubu na jinsi alivyoteseka. Mke wake alifika mahali akaongea maneno kama hayo hapo juu. Matokeo yake alikufa na Ayubu alibaki Mungu akamjali mara dufu ya kila alichopoteza.

Mimi ni mwafrika halisi lakini Mungu na ufalme wake anakuja kwanza kabla ya jambo lolote lile. Fahari zangu mwenyewe, familia na ukoo vyote vinafuata. Ni tofauti zetu kiimani na kiroho.

Naheshimu mawazo ya kila mmoja. Na ninayafanyia kazi. Nimejifunza mambo mengi mazuri kutoka ushauri wa wadau hapa lakini "as a general rule..." kama una mawazo yoyote ya aina hii...."keep them to yourself.."

MUNGU KWANZA... Mimi kitu gani? Mimi ni mavumbi tu... na siku moja nitarejea mavumbini....UKOO??? Ukoo kitu gani? Zilikuwako koo maarufu duniani kama ile ya Kaizari....au.. Faraoh....leo ni historia.....

Kama Mungu aishivyo....sitamwasi kamwe...Ije mvua...lije jua.......
 
POLE SANA,,,MUNGU AKUSAIDIE KAKA,,DUNIAN YOTE NI MAPITO,,HOPE KUNA SIKU HILI LITAPITA KWAKO...STAY STRONG BROTHER
 
Pole sana ndugu na hongera kwa ujasiri wako, Mungu anamalengo kwa kila limtokealo mwanadamu simamia maamuzi yako.
 


Safi sana!!! Endelea kumwinua Bwana Yesu katika maisha yako...maana aja upesi na ujira wako!!!
 
Hii ni ile mbinu BBC walisema ya kuyadanganya mayai ya mwanamke kisha mimba inatungwa pasipo mbegu za mwanaume just like kuku wa mayai wanaotaga bila jogoo.
 
Mungu akakubarikie muujiza wake. Lakini juu ya yote, ailinde amani na furaha ya moyo wako. Kila la kheri
 
Pole sana mkuu nimesoma ushauri wote na nimetambua misimamo yako.Mimi binafsi ningekushauri kama huyu mdau.Hapa kuna points nyingi sana embu rudia tena kusoma hapa kwa ajili yangu tafadhali.Mungu akuepushe na Yatima hewa maana kwenye vituo kuna watoto yatima wenye wazazi.Waliofanya kwenye hivi vituo nadhani mtakuwa mnaelewa ninachokisema hapa.
 


Asante sana mkuu. Ni kweli kuwa kuna ushauri mwingi sana umetolewa hapa. Na 98% ya ushauri huu ni mzuri. Mfano uliotoa hapo ni mojawapo. Jambo jema ni kuwa mimi ninasoma kila mchango wa mawazo unaotolewa. Ndiyo maana nimeshukuru hapo kabla na bado naendelea kushukuru kwa ushauri wenu. Na pia pale ninapohisi ushauri unaotolewa unamkufuru Mungu kwa kweli siwezi kukaa kimya. Ninajitokeza na kusema sitaki aina hiyo ya ushauri. Mungu atabaki kuwa Mungu...

Asanteni sana. Nimejifunza mambo mengi sana na mengi ni ya manufaa makubwa.
 


Asante sana mkuu. Ni kweli kuwa kuna ushauri mwingi sana umetolewa hapa. Na 98% ya ushauri huu ni mzuri. Mfano uliotoa hapo ni mojawapo. Jambo jema ni kuwa mimi ninasoma kila mchango wa mawazo unaotolewa. Ndiyo maana nimeshukuru hapo kabla na bado naendelea kushukuru kwa ushauri wenu. Na pia pale ninapohisi ushauri unaotolewa unamkufuru Mungu kwa kweli siwezi kukaa kimya. Ninajitokeza na kusema sitaki aina hiyo ya ushauri. Mungu atabaki kuwa Mungu...

Asanteni sana. Nimejifunza mambo mengi sana na mengi ni ya manufaa makubwa.
 


Hongera sana kaka!!! Aisee dunia hii inawahitaji sana watu kama wewe ambao wamenyooka kama chuma cha pua kwa habari ya Mungu na ufalme wake.
 

Very true indeed! You just spoke my mind.
 

πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…