freshbaraka
Member
- Mar 4, 2017
- 13
- 50
- Thread starter
- #41
The best option ambalo litakulindia heshima yako ni Wewe kuruhusu either Mzazi wako wa kiume au ndugu yako kulala na mke utakae muoa, Ni gumu sana hili ila litakueka Huru na maneno maneno, Wazungu ku adopt mtoto kwao ni possible kwa vile family zao nyingi Nuclear baba mama na watoto sasa sie Africans ni extended tuna mlolongo wa ndugu watakunyima tu raha mkuu, Wachana na Mambo ya pepo au sijui Mungu, Kama kweli anakupenda Mungu Kwanini asikujalie capability ya kubebesha Mimba, BTW mkuu luse ameeleza professional kuwa tatizo lako linatibika i mean liko ndani ya uwezo don't give to early mkuu hakuna msaada wowote kutokea mawinguni huko utakaokuja kukunasua ni Wewe mwenyewe Kuamka na kuamua kutatua changamoto inayokusibu, Uniwie radhi kama ntakuwa nimeongea baadhi ya kukukera
Ni mawazo yako mkuu. Nayaheshimu. Sijakata tamaa na nina amini Mungu atanipa watoto wangu mwenyewe kwa wakati tu. Ila in the mean time nataka ni-adopt. Wale wa kwangu wakija hata baada ya miaka 15 sawa tu.
Kuhusu kuachana na pepo na Mungu, nashindwa hata niseme nini? Lakini hapo ndipo tofauti yetu wanadamu ilipo. Naona hapo unamkufuru Mungu mkuu unaposema eti kama ananipenda kwa nini asingenipa mtoto. Ni sawa na kusema nimkimbilie shetani kwa sababu Mungu hajanitendea ninachotaka. Sitaki hata kusema zaidi.
Lakini wenye ushauri wa aina hii tafadhalini msinipe hata kidogo. Bakini nao. Mimi kwangu Mungu atabaki kuwa Mungu hata kama ataninyima vyote. Soma kitabu cha Ayubu na jinsi alivyoteseka. Mke wake alifika mahali akaongea maneno kama hayo hapo juu. Matokeo yake alikufa na Ayubu alibaki Mungu akamjali mara dufu ya kila alichopoteza.
Mimi ni mwafrika halisi lakini Mungu na ufalme wake anakuja kwanza kabla ya jambo lolote lile. Fahari zangu mwenyewe, familia na ukoo vyote vinafuata. Ni tofauti zetu kiimani na kiroho.
Naheshimu mawazo ya kila mmoja. Na ninayafanyia kazi. Nimejifunza mambo mengi mazuri kutoka ushauri wa wadau hapa lakini "as a general rule..." kama una mawazo yoyote ya aina hii...."keep them to yourself.."
MUNGU KWANZA... Mimi kitu gani? Mimi ni mavumbi tu... na siku moja nitarejea mavumbini....UKOO??? Ukoo kitu gani? Zilikuwako koo maarufu duniani kama ile ya Kaizari....au.. Faraoh....leo ni historia.....
Kama Mungu aishivyo....sitamwasi kamwe...Ije mvua...lije jua.......