Natafuta mtaalam wa kunisaidia kupata ajira na kuniondolea gundu

Pole Sana kijana mwenzangu unayopitia wewe Ndio mimi pia nayapitia
 
Mkuu,ushawahi kupatwa na gundu wewe????Ukiwa na gundu ndio hiyo kauli ya inakuwaje,inakuwaje inakuwaje nyingiiiii.Mana mtu qualifications unazi lakini hupati kitu,na hata ukipata hudumu nacho.Hakika nakwambia ukiwa na gundu hata printer kuprint jina lako inaweka kukataa Dunia Ina maajabu sana hii Jamaa namuelewa zaidi ya kumuelewa.
 
Sijui wewe ni dini gani,lakini kama ni Muislam,amka usiku wa manane...swali SUNNAT HAAJA.Fanya hivi.....Ukiamka usiku kwanzia saa nane kamili ....umechelewa sana iwe saa tisa na dakika 45,Kisha chukua udhu alaf swali SUNNAT tahajud rakaa nane baada ya hapo swali SALAT HAAJA.Hii ni swala maalum kwaajili ya haha zako.Ule mda uko sidja ya mwisho omba mahitaji Yako yoteeee.Fululiza hizi ibada Kila siku ya Mungu mpaka ufanikiwe(nani sure must UTAFANIKIWA).Kipi kitatokea......Everything will be aligned in a miraculous way,hakika nakwambia.Gundu litatolewa na mtu mwenye uwezo huo tena bila hata kumtafuta.Atakuja tu from nowhere.Yani haya mambo nasema mana nimesha pitia mengi ila Mungu alitaka kunionesha ukuu wake.Sisi katika dini yetu tumeambiwa na Mtume Muhammad(s.a.w)Kuna usiku mwingi Mungu anashuka mbingu ya chini na kunadi(Nani mwenye shida nimtatulie,Nani mwenye madhambi nimsamehe?nko)Hili jambo Si la uongo mana nmefanikiwa yote kupitia Qiyam Layl.Kazi Kwako.
 
Kaka mganga wa kwanza ni Mungu,Hakika nakwambia.Nlipitia hayo yote.Usi expect kupata feedback unayo itarajia.Ni kheri anae kupa ushauri juu ya uwezo wa Mungu na Si kukupelea kwa mganga(kumbuka sipingi wewe kwenda huko,ila je utapelekwa kwa anae kufaa?Wengi matapeli,au wengine wanaweza kumtibu huyu lakini mwengine hawawezi).Wenye Karama wanaweza kujitibu WENYEWE(spiritually)lakini sisi bado Darja zetu za ucha Mungu ni ndogo spiritual things huwa twatibiwa na watabibu wakidini au waganga,lakini mimi nnacho kwambia mwombe Mungu yeye mwenyewe akuletee mtabibu mzuri juu ya majanga yako(atamleta,tena atakutibu kirahisi kama kupuliza unyoya mwepesi kwa kuku,kikubwa muombe mumgu kwanza).Wajiona umekaa sana kitaa eee?Mimi nmemaliza University mwakwa 2010 nkapata ajira mwaka 2017 February,hapo vipi????Nlipitia dhoruba iliyo nifanya niwe humble kweli kweli nliyaona maisha katika Dimension tofauti na mwanzo.Simdharau tena Baa medi anae jiuza simjaji(nimekoma kujaji watu katika maisha),siku niliyo mpeleka mama yangu Muhimbili na kupanga mstari mbele pakiwa na watu zaidi ya hamsini kwenye foleni mama goti linamtafuna anaumwa mpaka analia machozi na huduma ya haraka( FAST TRUCK)ipo na Sina uwezo wa kulipa(NLILIA ILE SIKU SITA ISAHAU) ...ndo nlijua wanao chukua maamuzi ya kujiuza na kuwa ma baa medi au kazi nyingine tunazo ziona za hivyo tuwaache walivo.Nikwambie tu,ilifika mahali hata baadhi ya washkaji zangu walikuwa wanaiambia live kabisa...."We jamaa nenda kaongee na wazazi nyumbani,hii sio kawaida"mana Kila kitu kilikuwa kinagoma.Mambo nlokuwa na collabo na washakiji nayo yanaharibika,kwa ujumla nlikuwa nawaharibia mpaka wao,ikafika kipindi wakawa wananikwepa.Na kweli msipo kuwa nao wanafanikiwa.Siku moja nlikwenda Bodi ya mkopo hapa Dar kufatilia mkopo wangu majumuisho yake,hapo sasa ndo nlithibitisha...THIS ISSUE IS SERIOUS.Mana nlipanga mstari kama wenzangu wengine,tukaenda wee,nilifika zamu yangu mwenye computer akaitwa ofisi nyingine.Tukangojaaa,nkajichokea,kwenda nje kwa nyuma kule namkuta anakunywa supu wala hana habari,kumshtua akasema hivi bado kuna watu???Si nlimaliza??Nkamwambia noo mbona ulituacha???Akarudi ofisini,kuanza kazi taarifa zangu kaziona vizuri sasa atoe hardcopy ndio mtihani.Printer haifanyi kazi,jamaa kahangaika wee,akanambia kama hebu kaa pembeni aje mwingine,kuja mwingine faster katolewa hardcopy yake kasepa,jamaa akasema niende printer Iko poa,kujaribu tena kwangu ikagoma akacheka,akamuita wa nyuma yangu ikakubali akaondoka,akaniita tena ikagoma,jamaa akaniangaliaaa kisha akamuita mfanya kazi wa ofini ya jirani aje alone maajabu.Yule wa osifi ya jirani akakaa yeye sasa kwenye computer kujaribu jina langu ilikataa,kujaribu aliefata ikakubali,kwa ujumla watu wakawa wananishangaa Mwisho wa siku nlijiona kituko nkatoka zangu.Nlicho kifanya sasa,ni kufanya ibada za usiku,Wallah saa nane za usiku ilikuwa ni kharam kwangu kula.Naomba nalia mpaka kwikwi ndani ya swala.Naomba mpaka nahisi kabisa Mungu huyu hapa.Yani nahisi kabisaa,Mungu huyu hapa na anashauku ya kunisikiliza.Ukafika mwezi wa ramadhani,nkasema hapa sasando penyewe,nlifanya ibada sanaaa,kwenye kumi la mwisho nkiwa natafuta usiku wa cheo....Kuna mtu akanijia ndotoni akanambia njoo badae tuonane stendi ya Mbezi mwisho.Nlivoamka tu asubuhi nkaoga huyoooo,mpaka Mbezi mwisho stendi,nkawa na randa randa tu pale,baada swala ya dhuhri nkarudi Tena kiranda randa ikafika mahali nkawa kama nimejikatia tamàa hivi,mara naskia mtu anaita kakaa,kakaa jiran yangu akanigusa kunionesha waitwa kule...ni jamaa alikuwa kwenye gari na kataka kuondoka.Nkaenda huku natetemeka.Kiganja chake ni kikuwa zaidi ya changu,akanishika mkono Ile ya kusalimiana kumbe alikuwa kashika na kitu flani.Alinishika kama sekunde thelathini hivi.Naapa kwa Mungu jamaa alivoniangalia machoni...sikuweka kubandua macho yangu kutoka kwenye macho yake,aliniangaliaaa haongei kitu.Napata tabu nataka kujitoa siwezi,huo mda nimelowa iamcho mpaka kwenye boxer.Kisha akanambia (MAELEZO YOTE YA JINSI YA KUTUMIA YAKO KWA NDANI).Kisha akaniachia.Sikutaka kumwangalia Wala kugeuka.Nliondoka zangu nkaenda kukaa ng'ambo ya barabara Ili jasho likauke Ili nipande hiace niende nnapokaa.Siku Ile nlipo tumia hiyo dawa,nlilala usingizi ambao sikumbuki kwenye maisha yangu kama nshawahi kula usingizi mnono vile.Nkawa naihisi furaha(Joy)hata nkiwa natembea mpaka machozi yananitoka.Story tu iwe fupi,baada ya miezi mitatu,nliitwa interview katika sehem ambayo ni tata kweli kweli,Kila alofanyiwa interview alikuwa na mtu wake pale ofisini,wonder enough,kazi mkapata Mimi.Nlipata mafanikio ya haraka mabayo naamini yalifidia mda wooote nlochelewa kupata ajira.Mungu kwanza,Mungu atakuletea mtabibu wa kweli hata kupitia kwa marafiki zako tu utasikia hebu twende sehem flani,kumbe ndo Mungu kakupangia huko,lkn tanguliza maombi sana kwanza.
 
Njoo PM nikuangalie email nyota
 
Mimi ni mkiristo ndugu yangu. Hii njia ya sala za usiku nimeitumia kuanzia April to December 2022 lakini haijasaidia. Labda sikufanya kwa usahihi au unafuu wangu utapatikana kwa namna tofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…