Hizi player zamani vijijini zilikuwa zinaendeshwa na daina moo ya baiskeli soo unanyonga baiskeli ndo betri then rekodi player inaplay sauti ni speaker za Ahuja zile kubwa za msikitini inafungwa juu ya mti, usiku vijana mbalimbali toka vijiji mbalimbali ndio disco watu pori kwa pori wanakatiza maporini usiku Wana mapanga na marungu wanakutana na wanyama mfano fisi, chui, simba wanafata mziki kilometa 10 usiku sauti ufika mbali sana. Wanakula mziki usiku kucha alfajiri wanawahi kurudi majumbani kuwahi namba shuleni viboko vinakusubiria saa moja kamili viboko vinakuhusu. Mingi ilikuwa ni miziki ya misibani.