Mjukuu wa Magika
JF-Expert Member
- Jul 5, 2019
- 550
- 1,071
Wana jamvi,
Kama bado hujawahi kukutana na changamoto ya familia unaweza kudhani watu humu wanaleta stori za kusadikika. Mimi na mke wangu tumeishi naye kwa miaka nane sasa na kwa kipindi hicho chote nimejitahidi kuwa mwaminifu na kuhudumia familia vizuri.
Sasa vituko vya huyu mwanamke anagawa vitu vya ndani kama mafuta, mchele, maharage na hata mkaa. Vitu vinaisha kabla ya muda hata sehemu ninapofanya manunuzi huwa wanashangaa, husema huenda nina nyumba ndogo ila mimi ni mwaminifu kwa huyu mwanamke.
Kituko kikubwa alichokifanya ni kutoroka nyumbani akiwaacha watoto hivi sasa kamaliza miezi yapata mitatu taratibu mawazo ya kuoa mwanamke mwingine yanakuja ili kusaidiana maisha. Isitoshe mwanamke huyo hana elimu kubwa na hana ajira japo mimi ni payee sijawahi kumdharau kwa hali yake zaidi ya kumrekebisha pale anapokesea.
Sasa nimeona hali imekuwa climax na ninataka kuachana nae na watoto nitalea mwenyewe. Ushauri wenu wakuu 🤔