Nataka kuachana na ualimu haraka. Nikimbilie wapi?

Nataka kuachana na ualimu haraka. Nikimbilie wapi?

Late 2009 kuna Mwl mmoja alifanya uamuzi kama huu unaoutaka wewe, yeye alisoma kozi fupi ya Ualimu wa Sekondari mwaka 2006 kipindi Shule za kata zimeanzishwa. Sasa alimua kwenda kusoma Degree ila aliamua kubadili kozi ya kwenda kusoma chuo, alichagua Accountancy na alifanikiwa kudahiliwa UDOM.

Wakati anaomba ruhusa kwa mwajiri wake(DED) alidanganya kuwa anaenda kusoma Ualimu akapewa ruhusa.

Baada ya kumaliza Chuo akiwa na Degree ya Accountancy akashindwa kurejea kwa mwajiri ili aendelee na kazi maana alidanganya tangu mwanzo. Akaamua kuingia mtaani ili atafute kazi. Aisee mambo yakawa magumu sana akafanya Application nyingi za kazi bila kuitwa hata Interview moja, stress si ikapiga hodi akakondeana hatari maana mwanzoni alikuwa bonge. Wenzio ambao hawakudanganya wakarejea kazini(Ualimu) bila usumbufu wowote tena wengine waliopata GPA kubwa walipangiwa Vyuo vya Ualimu kwenda kufundisha, yeye akaanza kujutia uamuzi wake.

Sasa hivi sijui yuko wapi maana mara ya mwisho nilikutana naye mwaka 2015.

Kwa hiyo binafsi nashauri kama hauna chanzo kingine cha ugali, usiache ualimu ukakimbilia kusoma kozi nyingine tofauti na hiyo Ualimu, imagine walimu wamejaa mtaani wenye degree na wanatamani wakafundishe hata Primary angalau wapate hela ya kusogeza siku
Ualimu ni kama kitanzi fulani hivi.
Kujinasua inabidi utumie timing vinginevyo kinakifyatukia.
Huko halmashauri unyama sana
 
Kama una chanzo cha mapato kingine unaweza acha, lkn nakushauri Usiache kaz km huna direction, kutoka no rahis Ila kuingia ni shughuli pevu lkn bora hata ungekuwa na BA, ya education lkn kwa dip utaona hela haitosh pia wapo wengi mtaan wanatamn nafasi ulonayo
Kweli kaka maisha magumu hku mixer ndugu Atari tupu
 
Ualimu ni kama kitanzi fulani hivi.
Kujinasua inabidi utumie timing vinginevyo kinakifyatukia.
Huko halmashauri unyama sana
Upo sahihi .... mshahara umetoka jana lakin leo sina kitu na gas inaelekea ukingoni , na ndugu na wadogo zangu wanaomba chochote, wanaamini nnakaz nna pesa kumbe taabu tupu
 
Ahsante ndugu lkn vp nikienda kuchukua bacherol ya physics ama biology pasipo ualimu?
still unapoteza muda mkuu kwanza muajiri wako haitambui hiyo course, ingekua enzi za Kikwete ungeweza enda kusoma hata Mass Communication ukae chuo hata miaka 10 hakuna wakuzuia mshahara au kukuuliza mbon hurudi kazin...
Kwasasa nenda kasome Bachelor ya ualimu bahat nzuri una masomo ya sayansi, ukitoka chuo rudi kazini fight kutoka ktk ualimu uhamie taasisi nyingine za serikali NECTA TET UKAGUZI TMDA TBS ukihangaika nao hawa ndani ya 2yrs wanakuhamishia kwao unalamba pesa nzuri, shida yenu walimu hamhangaiki kuuliza taasisi au wizara ambazo unaweza kuhamia... Asikudanganye mtu sasa hivi ajira hazipo otherwise kama una undugu na kiongoz mkubwa sana ambaye akikohoa tu unapewa kazi... Zamani wabunge wakurugenz DC Rc walikua wanaweza kumtafutia kazi mtu na akapata, ila sikuhiz hata wao wenyewe watoto wao wapo nyumban hawana kazi...
 
Ngoja nifate ushauri ndugu
 
Kinacho kufanya upigike siyo ualimu, ila ni uvivu wako na kutokufikiria nje ya box. Kama usipobadilika hata uwe na masters maisha yako yatakawa hivyo hivyo tu.

Usione watu wanaendesha vimagari vyao na wamejenga nyumba zao ukadhani ni vyeti vyao au kazi zao ndo zinawalipa. Siyo hivyo....ni uchakarikaji.

Popote ulipo pana fursa, ni wewe tu kuwa na jicho la tatu..na kuondoa uvivu.
 
Upo sahihi .... mshahara umetoka jana lakin leo sina kitu na gas inaelekea ukingoni , na ndugu na wadogo zangu wanaomba chochote, wanaamini nnakaz nna pesa kumbe taabu tupu
Yaani una Mshahara kila mwezi, una muda then mpaka sasa unategemeabkuja pesa za mshahara tu huo mshahara ukijunuisha muda unaopata kutokana na kazi ya uwalimu ungetumia Kama mtaji kutengeneza pesa ya pili.
 
Mkuu usipende kua negative, utanisamehe kama ntakukera..ila yuko sahihi eneo lolote mjini mfano posta,mnazi,livingstone,mwenge (mlimani kwa madalali), na kwingine kwenye parking hukosi waosha magari..nna miez sijaosha gari town bei ilikua 3000 labda itakua imepanda, kulifuta tu vumbi gari 1500 mpaka 2000.

Gari ni nyingi sana mjin mkuu na nyingi zinapark na kutoka so hii ni fursa japo inaweza isifike 1M kama alivosema mana kuna gharama ya sabuni ya unga na maji..ila jiulize mtu kaingia town saa 2 asubuhi mpaka saa 12 jion. Mbona gar 10 easy tu tuseme kila saa ana gari 1... hata akipata magari 6 kwa siku bado si haba kuliko mzunguka na mavyeti moka imepaukaaa kutwa kuomba nauli!
Kwamba hapo mjini utakua uko mwenyewe tu mpaka kila siku uwe na bahati ya kupata magari 10 ya kuosha?ingekua ni rahisi hivyo mbona kila mtu angetaka kuifanya hiyo kazi.
 
Uamuzi wa kuacha kazi ni sawa na uwamuzi wa mtu kutaka jinyonga hashirikishwi mtu so jilipue mwanangu acha kazi uwalimu kitu gani bwana ila mwalimu mbona tunaoma walimu wanamiliki nyumba za kisasa, magari mazuri ,.watoto zao wanasoma shule nzuri hawa walimu wa serikali gani au Wana majini ndani
 
Upo sahihi .... mshahara umetoka jana lakin leo sina kitu na gas inaelekea ukingoni , na ndugu na wadogo zangu wanaomba chochote, wanaamini nnakaz nna pesa kumbe taabu t

Mungu akubariki sana ndugu, maana ungemkopesha mungesha vunja udugu / ujamaa wenu .maana hana kwa kutoa hyo pesa .
Acha kujidhalilisha mwalimu acha dhalilisha walimu kama shida zako ni wewe usiwapake matokeo walimu nyie ndio mnatakiwa kufukuzwa kazi maanq hamjitambui
 
Back
Top Bottom