Nataka kuanza safari yangu ya kuwa Data analyst unanishauri nini katika safari yangu?


Kwn kusoma hii Data analyst inahitaji uwe na background ya kitu gan au hata computer application pekee unaweza?
 
Kwa kifupi, elewa kwa nini unataka kuwa mchambuzi wa taarifa (Data Analyst)

Ni muhimu kujua jinsi ya kutumia excel kuchakata taarifa. Hata hivyo, excel ina limitations kadhaa hasa unapokuwa na kiwango kikubwa cha dataset.

Kwa hiyo pamoja na kujifunza excel, jifunze pia program kama SQL itakusaidia kuchambua taarifa hata kama una dataset kubwa.

Pamoja na uchakataji, lazima ujifunze njia ya kuwakilisha (visualizations) taaarifa zako ulizopata kwa uchambuzi wako. Kuna mifumo mingi lakini baadhi ni Power BI au Tableau
 
Kwn kusoma hii Data analyst inahitaji uwe na background ya kitu gan au hata computer application pekee unaweza?
Kuna vitu vingi kama Power BI, SQL, Python na nyinginezo ila Excel ukiijua inasaidia kwenye hizo zingine, ni kama vile mtu anajifunza kusoma na kuandika lazima ajue irabu na silabi ili iwe rahisi kwake kuunda maneno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…