Nataka kuanzisha umissionari wa kupeleka Ukristo kutoka Afrika kwenda Ulaya na Marekani, naombeni mawazo

Unafungu lolote Yesu hakuja kuleta dini.
Dini ni nini?
Biblia inaelezea dini ya Kweli, kama kuna dini ya kweli basi ya uongo ipo. Na dini ipo.

Shida ninayoiona hapa watu wanatafsiri dini kimagharibi hawahwa wenye tabu. Tutafsiri kiebrania
 
Asante sana mtumishi ngoja niombe connection na Mungu niende huko nipeleke wamishonari wangu wakitanzania.

Pia mkuu waafrika masikini ni waafrika wasio na Yesu. Ukiwa na Yesu wewe ni mrithi pamoja na Yesu. Vitu vyote alivyonavyo Yesu ni vyako. Ndio maana Paulo anasema. Vitu vyote ni vyetu.

Mkristo kujiona maskini ni matokeo ya wazungu waliokuja kuleta injili ya kuwaandalia mazingira wakoloni watupige mali.
 
We jamaa unachekesha sana. Unachukua soda kutoka Mlandizi unapeleka kuziuza Dar. Unachukua Ndizi kutoka mahakama ya Ndizi unapeleka Kagera. Unachukua Sangara kutoka Dar unapeleka kuuza Mwanza. Nakutakia Kila la kheri mkuu
Wazungu wengi hawana mambo ya dini na hawajielewi mkuu. Ni kama asilimia moja tu.
Ndio maana UK walikuwa wanaomba waletewe mapadri kutoka Afrika maana huko wanaisha tu kilasiku.
 
Dini ilicho wafanyia wazungu miaka ya kale hawana hamu nayo tena.

Ukristo umekwisha poteza nguvu ulaya na wao wazungu wana sababu zao za kupuuza dini sioni kitu kipya ukiwa pelekea ambacho hawafahamu kuhusu dini.

Wazungu wapo mbali kimawazo na kifikra kuhusu dini kuliko wewe wao ndio walikuwa wa mwanzo kuiexperience hiyo dini waliyo kuletea wanaijua ndani na nje.
 
Wale waliielewa dini vizuri ilipokuja kama free choice enzi za wakina paulo.
Tatizo lilianza baada ya karne ya kwanza baada ya dini kuporwa na wanasiasa na kuitumia kama kifaa cha kushurutishia utii hasa kwa wazungu wa magharibi.

Wengi hawamuoni Mungu wanamuona kasisi, wanaona dola. Hili zoezi limefanyika kwa miaka zaidi ya 1000. Ili kujikomboa kwenye huu ufashisti waliingia vita vya zaidi ya miaka 30. Hii imepelekea wengi waishie kuwa matheists na siku hizi ni mashoga.

Sasa mimi nataka kuwafariji, kuna namna nitaongea nao, watanielewa mtu.
Ni watu wema sana.
 
Hakuna kitu kipya utaenda kuwafundisha wazungu kuhusu dini yao wasicho fahamu labda wewe ndio wakufundishe mengi kuhusu dini yao usiyo yafahamu.
 
Zungumza na Mungu sio wanadamu.woto wa popote ni Mungu huhusika
 
Nisawa kabisa kwa maana saivi wao ndio hawamjui Mungu kabisa ilikuwa ni babu zao
 
Unafungu lolote Yesu hakuja kuleta dini.
Dini ni nini?
Biblia inaelezea dini ya Kweli, kama kuna dini ya kweli basi ya uongo ipo. Na dini ipo.

Shida ninayoiona hapa watu wanatafsiri dini kimagharibi hawahwa wenye tabu. Tutafsiri kiebrania
"Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii kwenda kuwatazama, yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa"

YAKOBO 1:27


Sasa hapo umeona wapi pamesemwa uKristo ni dini.
 
uKristo sio dini. keep it in your mind and in your heart!
 
Hakuna kitu kipya utaenda kuwafundisha wazungu kuhusu dini yao wasicho fahamu labda wewe ndio wakufundishe mengi kuhusu dini yao usiyo yafahamu.
Ukristo ni dini kutoka palestina. Hao walioelekewa kama wewe tu. Shida walipotuletea waliileta kwa hila za kiutawala na kibiashara. Ila wachache tunajua utamu wa Ukristo tumeanza kuwaonea huruma.

Asilimia zaidi ya 90 hawajui kabisa ukristo mkuu. Maana kwa miaka mingi walitawaliwa na ukristo kama dini ya serikali za watu sio kqma ufalme wa serikali ya Mungu.
 
Zungumza na Mungu sio wanadamu.woto wa popote ni Mungu huhusika
Naona kama sauti ya Mungu inanielekeza sana kwa hawa jamaa aisee.
Labda kwa sababu wanaushawishi mkubwa, wakimuelewa Kristo na ufalme wake ulivyomtamu basi dunia nzima itaokolewa kwa upesi, chachu ikitokea Afrika.

Ndio maana huwa nikiwaona huku mtaani siwaachi
 
"Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii kwenda kuwatazama, yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa"

YAKOBO 1:27


Sasa hapo umeona wapi pamesemwa uKristo ni dini.
Dini ni nini?
Nakushukuru kwa mchango mzuri.
 
Mbona hapaa tz bado hawamjui Mungu vya kutosha?!wazo lako zur anza hapa kwanza ili wasije kengeushwa na hhao wazungu,Imani potofu nyingi mno
 
Unachanganya Ukristo na uyahudi. Ukristo umeanzishwa na watu nje ya middle east wakiwemo watu wa ulaya mfano wa early founders ni Roman Catholic
 
Unachanganya Ukristo na uyahudi. Ukristo umeanzishwa na watu nje ya middle east wakiwemo watu wa ulaya mfano wa early founders ni Roman Catholic
Unachanganya roman catholicism na ukristo. Drivers wa hawa jamaa hasa wale wa zamani ilikuwa ni greek mythology. Hizo ndio zilikuwa na ushawishi kuliko Kristo mwenyewe. Ndio maana sanamu nyingi unazoziona sio za Yesu wala Maria au mitume ni miungu ya kigiriki. Wakina Diana, Apollo etc.

Na hawa ndio walichangia kuwafanya wazungu wengi wawe kama sasa hawajui kitu. Waliwazuia kusoma maandiko, waliwalazimisha dini kwa chuma kupitia serikali. Walifanya nafasi yao kwa ufahamu wao inabidi twende waafrika tukawarudishie matumaini wazungu. Ukiwafuatilia kimsingi ni watu waliokata tamaa na maisha wanajiishia tu kama wanyama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…