Nataka kuanzisha umissionari wa kupeleka Ukristo kutoka Afrika kwenda Ulaya na Marekani, naombeni mawazo

Nataka kuanzisha umissionari wa kupeleka Ukristo kutoka Afrika kwenda Ulaya na Marekani, naombeni mawazo

Inaonekana ililetwa na kikundi cha jamaa wachache tu. Waliwaacha wenzao karibu asilimia 90 bila kujua kitu.

Pia wengi waliokuja walikuwa ni mamafia wa kidini, kulainisha njia kwa mabeberu wachache wakina Carl Peters waje wapige madili huku.

Afrika mkuu ni sehemu bora kabisa mwanadamu anapaswa kuishi. Siwezi kupakimbia. Huko kama sio kuwapelekea Injili basi kwenda kutalii tu.
Achana na story za mapanafricanist, missionary walikuja kama wao
 
Wakuu nimegundua Ulaya na Marekani kuna upagani mwingi sana.
Wala hakuna ukristo kule ni zuga tu.

Sina wasiwasi na uarabuni na china, Maana huko kwa utafiti wangu kuna wakristo kificho wengi sana ila wanaingia misikitini na kuswali kwa ajili tu ya usalama wao.

Nimefikilia hawa wazungu kabla hawajapotea niwapelekee umishonari, niwe na kikosi kazi cha waafrika wachapakazi, Masponsor ni sadaka za waafrika Matajiri na masikini.

Naombeni mawazo jinsi ya kuwapata hawa jamaa kirahisi huko makwao na kwenye mitandao. Kwa sasa ninayo app inayoweza kutengeneza autosubtitles kwa karibu lugha za wazungu wote.
Wapo wamisionari wengi sana vijana wa kikatoliki na hata madhehebu mengine nchi za Ulaya, America, Asia nk. Jiunge nao uende kuhubiri Enjili duniani kote!
 
Wapo wamisionari wengi sana vijana wa kikatoliki na hata madhehebu mengine nchi za Ulaya, America, Asia nk. Jiunge nao uende kuhubiri Enjili duniani kote!
Asante sana, connection zao. Hata link
 
Una umri upi na elimu umefika level gani? Je wewe ni mkatoliki aliyebatizwa?
Kama hadi niwe mkatoliki, basi ntatafuta mfumo tofauti wa kwenda na vijana wangu tuwasaidie hawa jamaa.
 
haya ni mafunuo, hadi ufunuliwe. ni kazi ya Roho Mtakatifu baada ya mtu kuokolewa. njoo kwa Yesu upate wokovu, uyajue haya na mengine mengi.
Acha kuandika ujinga mafunuo , mafunuo taka taka tupu nyie watu wa namna hii ni wapumbavu sana mkishindwa swali mnakimbilia mafunuo.

Kwamba wewe peke yako dunia nzima ndio una hayo mafunuo ya ukristo sio dini huu ni upumbavu acha mara moja
 
Kama hadi niwe mkatoliki, basi ntatafuta mfumo tofauti wa kwenda na vijana wangu tuwasaidie hawa jamaa.
Sawa pia ila ujue kwamba ule ni mtindo wa maisha wa watu na hawaoni kama kuna shida na wanalindwa na sheria pia. Ukiingilia mfano mambo ya ushoga katika nchi inayohalalisha mambo hayo waweza kujikuta wewe unashtakiwa kwa uhalifu!
 
Back
Top Bottom