Nataka kufanya DNA test ya watoto wa kaka kupitia mimi je inawezekana?

Huu ndio ushauri sahihi.Ufuate.
 
Hakuna haja ya kuwachonganisha,
Sababu ni hizi hapa ukishajua hamna damu yenu kuna ambao utawatenga na kiuhalisia kama mama yao ni mmoja huwezi kuwatenga utawajengea ugomvi usio na mashiko, Hivyo kuliko kuwatelekeza kwa kuwajengea ugomvi na vidonda vya maisha
Fanya hivi:
Bora uwatenge sasa hivi bila kuwapima DNA,
AU
Kuwalea hivyo hivyo japo moyo wako tayari una kitu,
Chochote utakachofanya kitaongeza sonona moyoni mwako hapo baadae,

Hata kama huko nyuma ya pazia shemeji anagawa hovyo bila heshima mwache watoto wakikua timua baki na watoto.
 
Je,kama sio wenu utawatelekeza?

Iko hv kwetu sisi waislamu, mwenye watoto ni baba mwenye ndoa yake halali, hata kama ikidhibiti kisayansi kuwa sio damu yake lkn katika sheria ya mungu ni wake kwakuwa ndio mwenye shamba.

Point yangu ni hivi kuna haja gani ya kupima wkt mpaka Baba yao anafariki wanajua yule ni baba yao, unataka kuwatengenezea mazingira gani huko mbeleni?

Acha hiyo kitu chief
 
Kwan mkuu kuwalea watoto,narudia watoto,nasisitiza watoto hata Kama sio wako Kuna shida gani?mbona Kuna wengine wanachukua watoto sio wao na wanawalea ?wewe walee tu kwani huwez jua Nani atakuwa Nani na Nani atakusaidia wapi.wewe walee tu acha kuwawekea wasiwasi utaanza kuwachukia mdogomdogo.

Kama baba yao alifariki na hakuwahi kuleta Mambo hayo wewe unayaleta ya Nini ? Huoni Kama unakosea au unatafuta sababu ya kuwafukuza wakawe watoto wa mtaani.kama unashindwa kuwalea tafuta ndugu wengine wakusaidie ila Hilo unalolitafuta ni Kama unawatafutia sababu ya kuwafukuza na pia unamkosea marehemu.
 
Acha hizo hata wewe ukipimwa DNA utakuta sio wa ukoo wako
 
Mkuu uko sahihi ntakujia inbox
 
Je
Je Wewe ukiwa ndiye tatizo( mtoto wa nje)?
 
Kaka yako kaacha watoto wanne. Yaelekea wewe huamini kama ni watoto wa marehemu kaka yako, hivyo unataka vipimo vya DNA ili kujidhihirisha kwamba kweli ni watoto wa huyo kaka yako. Je utatumia sample kutokea kwako katika kupima hayo? Una uhakika gani kwamba wewe ni Mtoto wa baba yako? Utakuta huna vinasaba vya huyo unayemuita Baba au pengine hata marehemu kaka yako hana vinasaba hivyo. Itakuwa vigumu sana kuthibitisha wazazi wa watoto hao pasipo kuwa na vinasaba vya marehemu. Fanya mpango upate kibali cha kuufukua mwili wake na kuchukua sample zinazohitajika kwa zoezi hilo ndiposa uendelee na zoezi unalolihitaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…