Nataka kughairi kufunga ndoa, zimebaki week 3. Nifanye nini kutimiza azma yangu?

Hii hali huwa inatokea ,ila ukioa utashangaa jinsi utakavyo jisikia amani ! Kwa hiyo piga maombi endelea na mchakato
 

Kama ameshalipa mahari na anaogopa mkataba wa ndoa. Namshauri afunge ndoa ya kimila kwa utaratibu wa kabila lake ama mila zao. Ndoa za kimila zimembana sana mwanamke kuliko za kanisani ama kiserikali
 
Kiimani hilo ni pepo, kemea!
Kisaikolojia hiyo itakuwa aina fulani hivi ya disoder au gamophobia (fear of marriage)
Kijamii itakuwa kuna stage uliivuka katika makuzi!
So, pambana tu. Mambo yatakuwa sawa.

Na huo ni mwanzo tu. Bado kuna phobia nyingine ya kuongeza familia. Usianze kumwambia mtoto wa watu atoe mimba, mara hauko tayari kuwa baba.
Ndoa ni committment, tafuta wanasaikolojia wakusaidie
 
Asante, ndoa imetangazwa tayar, bado kama safari moja tu ya mwisho mkuu, then send off kwa bi mdada, then marriage

Watakubali kweli?
Kama baba yako yupo hai, wahi fasta kamweleze, ukifuata huu ushauri wangu utakuja kunishukuru.
Vinginevyo utapata matatizo makubwa ya kimahusiano na jamii kama utaingia mitini.
Futa wazo la kurogwa.
 
Mkuu, naamini umepita shule. Katika kipindi cha mtihani watu wengi hupata heavyness (uzito) pindi anapo elekea exam room lakini huwez ahirisha mtihani sababu ya huo uzito. Tena unajipa courage kuwa 'utapasua' na unaenda na kufaulu.

Naamini u-mkristo;
Si kila jambo linalokufanya usiwe confortable ni baya, hata katika biblia Jeremiah alifika sehem aligoma kulitamka jina la Mungu kutokana na majanga yaliyokuwa yakitokea pindi atamkapo lkn je, ni jambo baya kutamka jina la Mungu? Jeremia 20: 7-9

Nabii Yona aliagizwa na Mungu aende Ninawi lkn hakuwa comfortable kwenda na akakimbilia sehem nyingine (Tashishi) japo yalikuwa ni maagizo ya Mungu. (Yona 1:1-3)

Kitu kingine kinawagharimu sn vijana ni ile katika ujana wao kutamka kuwa hawataoa au ndoa ni mzigo ama kwa sabab yoyote au mihemko ya company na age.

Maneno ni spirits, by the time unataka kuoa zile spitits (maneno) zinaanza kukuzonga ukitulia peke yako na kukushuhudia kuwa unaenda against na confession yako hvo kukupa uzito sn, ukichanganya na maneno ya washkaji mliyokuwa mnajazana ujinga unaona km unaenda kufanya usaliti juu ya 'wana'.
Shirikisha viongozi wako wa kiroho kwa msaada zaidi.

Kwa kuwa unakiri kuwa binti hana changamoto yoyote so far, Ushauri wangu ni kuwa:

Songa mbele, ndoa ni jambo jema mbele za Mungu. Mpango wa Mungu kuitawala dunia ulianza na ndoa pale bustanini Eden.

Katika vitu shetani anashambulia sn ni pamoja na ndoa kwa kuwa ndoa ni nuclear point ya kanisa, na usisikilize wale wanaokushauri kutokuoa, hayo ni mafundisho ya kishetani (1Timotheo 4:1-3)

Shetani anajua unapokaa bila ndoa maana yake unajiweka katika hatari ya uzinzi lakini pia utapishana na baraka za ndoa ambazo huwezi kuzipata ukiwa peke yako bali pale unapooa (Mwanzo 1:26-28).
 
Hiyo ni dalili mbaya kwa ndoa yako ikiwa utalazimisha kufunga ndoa sasa. Kifupi hiyo hali unayosikia ni ujumbe tosha kuwa ndoa kwako bado kwa sasa. Tumia hatua hizi kulimaliza hilo jambo.

1. Haraka sana Shirikisha ndugu zako wa karibu na viongozi wako wa kidini kwa kuwaambia wazi kuwa huwezi tena kufunga ndoa kwa sasa kwa sababu zako binafsi (watahamaki na watakulaumu sana lakini mwisho wa siku watalikubali na kulibeba kama jambo lao)

2. Tafuta namna ya kumueleza binti kuwa huwezi kufunga ndoa kwa sasa. (Ataumia na kusikitika sana, lakini atatulia tu).

3. Waombe msamaha na waambie watu wako wa karibu kuwa mpango wa kufunga ndoa umehairishwa kwa muda kidogo! Tarehe za ndoa zikivuka tu, anza kuwarudishia michango yao.

4. Kaa kimya. Nasema kaa kimya.
 
Umepigiwa bi harusi mtarajiwa?
 
Piga chini, uchumba unavunjwa bali ndoa haivunjwi. Muhimu, usioe.
 
Hiki kipindi ndo shetani anakuwaga anapambana sana na wahusika, ahirisha uone kama utapata huo wepesi unaoutafta, yaan utashangaa ilikuwaje ukaamua kuhairisha unless kama kuna kingine labda mtarajiwa umegundua hafai n.k lakin kama syo hvyo shetan anataka kukurudisha nyuma, hata sisi yalitupata hayo tukasali sana na sasa tunafurahia ndoa
 

Fungua funga
 
Asante Sana mkuu kwa ushaur wako, nimeupokea
 
Asante Sana mkuu kwa kunipa nguvu na moyo mkuu, Asante Sana
 
Kama baba yako yupo hai, wahi fasta kamweleze, ukifuata huu ushauri wangu utakuja kunishukuru.
Vinginevyo utapata matatizo makubwa ya kimahusiano na jamii kama utaingia mitini.
Futa wazo la kurogwa.
Mzee hayupo mkuu!
 
Asante mkuu, ila stage gani nlivuka katika makuzi, sijaelewa ndg
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…