Nataka kujiunga na Upadre ila kuna ufafanuzi ambao sijaupata

Jambo la kwanza u padri ni wito, mchakato wake una mambo mengi kuanzia ukuaji wako, uhusiano wako na kanisa nk.

Ushauri. Kila Jimbo lina mkurugenzi wa miito waweza kufika kwa paroko wako kwa hatua za awali kisha yeye atakupa mwongozo sahihi.

Tumsifu Yesu Kristo.
 
1. Hakuna umri wa mwisho kuwa padre, hata uzeeni unaweza pewa daraja takatifu
2. Unapata malezi ya kuendana na elimu uliyonayo. Malezi yataanzia pale ulipoishia wewe.
3. Ukishajiweka chini ya malezi salama majibu yote yatapatikana. Hii ni nia njema, unahitaji kuanza malezi mara moja
 
Usimvunje moyo mwenzako.
 
Jambo la kwanza u padri ni wito, mchakato wake una mambo mengi kuanzia ukuaji wako, uhusiano wako na kanisa nk.
Hiyo ndio inaitwa vetting kwa wale mliouliza vetting ni kitu gani kwenye kujiunga upadri

Vetting yake sio ya kitoto

Utachimbwa ndani nje
 
Kama unataka upadre wa jamii forum basi subiri majibu ya wadau ila kama una nia ya kweli ni vyema ukaenda kanisani na kukutania na padre wa miito ambaye atakujibu maswali yako yote bila wasiwasi.
Hapa hapa pia kuna majibu mazuri. Ni kuchambua tu jema na baya. Amefanya vizuri na atapata msaada anaouhitaji
 
Seminari kuu sio miaka 6,ni miaka 8 hadi 9, Miaka mitatu (3) Ni Falsafa, Miaka minne (4) ni Teolojia, Mwaka mmoja (1)wa Uchungaji.Sometimes km kuna shida Ktk ufaulu au nidhamu huweza kwenda miaka ,8 hadi 9 na sometimes 10.
 
Yesu alichukuwa watu hoe hae kina Mtume Petro na wakawa bonge ya mitume...
 
Seminari kuu sio miaka 6,ni miaka 8 hadi 9, Miaka mitatu (3) Ni Falsafa, Miaka minne (4) ni Teolojia, Mwaka mmoja (1)wa Uchungaji.Sometimes km kuna shida Ktk ufaulu au nidhamu huweza kwenda miaka ,8 hadi 9 na sometimes 10.
Mwaka mmoja wa malezi sijauona apoa,wazee wa kipalapala ntungamo,na segerea
 
Tafuta kuonana na mkurugenzi wa miito jimbo katoliki ulilopo
 
Number 3 imekuengua..... wewe ni mlei
 
Kwanza hakuna masomo yanaitwa masomo ya upadre. Upadre ni Sakramenti. Pili umeshafeli kabla hata hujaanza jitihada zako. Upadre sio wa kombania. Njia sahihi muhimu na ya kwanza ni kuonana na paroko wa mahali husika uliopo.
 
Swali la kwanza Hakuna mwisho wa umri kujiunga na upadri.

Kuhusu elimu ukitoa kidato cha sita,siyo chini ya miaka 10 ya kusoma vyuo vikuu ukisomea huo upadri.HAIPUNGUI MIAKA KUMI.

Swali la tatu,Kwa kuwa ulishakuwa na mtoto hili ni kikwazo kwako.Ila sina hakika na hili.

Hayo mengine ndivyo ilivyo.

ILA UPADRI NI WITO SIYO KAZI.HILO ULIJUE.

PIGIA MSTARI NENO WITO.WITO.

UKIWA HUNA. WITO UTAKWENDA KUTEMWA TU AU UTAJITEMQ MWENYEWE .
 
Kwanza hakuna masomo yanaitwa masomo ya upadre. Upadre ni Sakramenti. Pili umeshafeli kabla hata hujaanza jitihada zako. Upadre sio wa kombania. Njia sahihi muhimu na ya kwanza ni kuonana na paroko wa mahali husika uliopo.
Alichomaanisha masomo ya theolojia,malezi ñk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…