Nataka kukaa mbali na mtoto

Nataka kukaa mbali na mtoto

Usimuache huyo mtoto ataumia mno maana naelewa maumivu ya kumpoteza na kukata mawasiliano ghafla na mtu unayempenda na uliyemzoea haijalishi ni nani kwako
 
Natumain wazima kama kichwa Cha habari kinavojieleza.

Nilikuwa kwenye mahusiano na mtu lakini nilikuta tayari anamtoto wa miaka 5 mwenzangu hakuwai Kuishi na mzazi mwenzio na mtoto analelewa Kwa bibi yake, baada ya kunitambulisha yule mtoto kiukweli nilikuwa nampenda sana na mtoto alikuwa Yuko karibu sana na Mimi ni mpole anaadabu sana.

Baada ya muda nikahama mkoa x ila mtoto Kila akiwa na babaake anasema msalimie mama na simu anaomba anipigie niongee nae now nimetengana na baba Kwa sabbu tulizoshindwa kuzitatua na mtoto sahiz anamiaka 8 lakini nikirudi haipiti siku lazima Aje kunisalimia na ananiita mama lakin sioni tatizo najua ni upendo tu.

Kubwa kuliko Wana mahafali madrasa akaja kunipa taarifa na kilasiku huwa anakuja kunikumbusha nisisahau kwenda kutokana na ubusy na kwakuwa ni mtoto Kuna details hakunipa yaani muda wa sherehe na mahitaji mengine nikaamua kumpigia simu babaake kumuuliza aniambie muda Cha ajabu baba Hana taarifa na hakupewa na mtoto na huwa wanaonana sana.

Nimejisikia vibaya nahisi huu ukaribu Sasa utaleta tafrani nataka nikae mbali na huyu mtoto bila kumuonyesha kuwa sipo kbisa na babaake
namnagan nimuweke mbali na isimuathiri huyu mtoto?

Na kma sio uamuz mzuri mnaweza kunisahihisha

Mnamtesa snaa Huyu mtoto. Najua kuna Baraka za kuchuma hapo
 
😂😂Wew umeona single tu hapo😂😂😂
sophy27 rafiki yangu kwanza pokea pongezi zangu.
Ni nadra sana wasichana wa kisasa kuwa na upendo wa aina hasa umetengana na babake.

Ushauri wangu;
Huna haja ya kumtenga mtoto na upendo wako jspo chanzo kilikuwa ni mahusiano yenu lakini wewe ni mkomavu kiakili kwani uliweza kutenganisha mapenzi na upendo kwa mtoto.

Epuka kumtenga huyo mtoto zaidi ni kuongeza umakini hasa unaposhirikishwa jambo umdadisi kama amemhusisha na baba yake.

Hongera sana
 
Single
Wee endelea tuu mie nilipigwa kibuti mapema tuu. Alafu imagine ananikataa mie kumbe alikuwa ana date na single father 🤣🤣🤣🤣

Hapa ndipo unapojua wanawake wanapenda kishare de libolo🤣🤣🤣🤣
Kwanin lkn🤣🤣🤣🤣
Subiri akipata pesa utamtafuta ukae karibu yake
Pesa Haina maana km ukiamua kumpenda mtu utu Ndo kitu Cha kwanza
 
Jitahidi uende kwenye hayo maafali, jitahidi pia kumpenda kama anvyokupenda wewe.

Nilitaka kuuliza vipi kuhusu mama yake?

Katika hizo sababu zilizoshindwa kutatulika ikitokea sababu ya kutatulika unaweza kurudiana na huyo mr?

Yote ya yote moyo au nafsi ya mwanadamu au pengine kiumbe chochote huwa kina hisia za upendo kwa mtu au kitu bila ya kua na sababu.

Mtu au chochote kinachoonyesha kuwa upendo nawe, jitahidi nawe kuonyesha upendo kuzidi yeye, itakusadi sana kama sio leo basi kesho au mtondogoo.
Mamaake kashaolewa somewhere mbali kidogo na alipo mtoto Asante nitazingatia ushauri
 
Back
Top Bottom