Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?

Biashara kichaa hiyo
 
Mkuu mie nakushauri anza na Fuso Tandam ndio utapiga pesa zaidi. Ninakushauri hivyo kwa kuwa hapa home tuna Scania tatu na Fuso mbili ila Fuso ndio zinapiga kazi kuliko Scania.

Na pia kama ni Scania kwa wewe unaeanza sikushauri kwa kuwa ni usumbufu sana hasa ikishaanza kuchoka. Scania za kukutoa umaskini ni zile model za kizamani.

Na pia wanaokushauri kuhusu magari ya abiria naomba usiwasikilize kabisaa, maana yana changamoto nyingi sana. Mie binafsi nina Nissan Caravan mbili ila ni kichefu chefu kitupu.

NB: Nimekushauri kutokana na uzoefu wangu wa kuishi na hayo magari kwa muda mrefu.
 
Dereva anapeleka mzigo mkoa wa rukwa ikifika wakati wa kurudi anakwambia hamna mzigo.kumbe kapakia tani saba za mahindi anapeleka manzese kushusha.
Si unaweza kufunga security camera ya kisiri ambayo ipo linked na simu unaona live kama gari ina mzigo au la? Ni wazo tu sijawahi kuona lakini naamini kuna technolojia hii.

Mfano: Amazon product ASIN B07CL3M4BY
 
So kama ni scania apite na 124L sio? tandamu... unanishawish mkuu.. mimi nilikuwa na target ya kuchukua kipisi 94 badala ya tandam
 
so kama ni scania apite na 124L sio ?? tandamu...unanishawish mkuu.. mm nilikua na target ya kuchukua kipis 94 badala ya tandam
113 au 124 mkuu, ila R420 ndio hovyo kabsa, sie moja ilikuwa ikitembea wakat mvua inanyesha inakuwa haifunguki zaid 60kph.

Pia kipisi hata 93 iko bomba saana, ila tu tandam ni bora kulikon kipisi kwa sababu ya masuala ya mizani
 
Gharama za uendeshaji je.. kipisi vs Tandam..mizan inalala wap?
Kama unavyojua kwny utumiaje wa mafuta Fuso inatumia kidogo zaid kulinganisha na kipisi, pia Fuso Tandam inapakia had tani 16 na ikipita mizan sio shida.

Ila kipisi ukipakia tani 16 lazima upigwe faini kwenye mizani, kuna kitu wanaita GVM kama sikosei yaani uzito wa gari ikiwa tupu kwa Kipisi inakuwa nzito zaidi. Ndio maana kwenye mizan inazidi.

Sie sana Tandam zinapiga kazi kwenda kupeleka mahindi huko kwa Usukumani. Gari inakodishwa hadi 1.6 milion kwa trip na ukitoa gharama ya kila ktu hadi kulipa vijana inabaki hadi 1.1 milion.
Na gari ndani ya siku mbili tu inakuwa imeshaenda na kugeuza.

Mkuu mie ni mvivu sana ku-type text ndefu ila nadhani nmejitahidi kadri ya uwezo wangu
 
Ingependeza ziaidi kama mngetuwekea na picha Tandem vs Kipisi
 
Upande wa service je?? Tandam vs kipis.. gharama ni sawa au kuna mwenye afadhal?
 
Yaani mimi kila nikimkumbuka yule mama ambaye lori lake lilitumbukia mto wami nakosa hamu kabisa ya magari
Tanzania yapo magari mangapi?? Yote yametumbukia? Biashara zote zina risk mkuu, na zote zina risk za kuhatarisha na kuua mtaji wote, ndio maisha yalivyo, tuna options mbili tu either tufanye au tusifanye.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…