Elungata
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 40,205
- 33,287
Mmenishawishi kuhusu Tandam fuso,,sasa swali zinauzwa bei gani na pia Tandam fuso ndo inakuaje?.
Najua kipisi,pulling,semi,boxboard,,ila kwenye Tandam fuso niko gizani
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mmenishawishi kuhusu Tandam fuso,,sasa swali zinauzwa bei gani na pia Tandam fuso ndo inakuaje?.
Mkuu, ushauri nimeuvhukua na ufanyia kazi
Mmenishawishi kuhusu Tandam fuso,,sasa swali zinauzwa bei gani na pia Tandam fuso ndo inakuaje?.
Najua kipisi,pulling,semi,boxboard,,ila kwenye Tandam fuso niko gizani
Ok,,bei sasaView attachment 1484713
Hio juu ni Fuso Tandam
View attachment 1484714
Hio juu ndio Scania kipisi ya mizigo.
Muhimu ni kukata bima kubwa.Tanzania yapo magari mangapi?? yote yametumbukia ? biashara zote zina risk mkuu, na zote zina risk za kuhatarisha na kuua mtaji wote , ndio maisha yalivyo, tuna options mbili tu either tufanye au tusifanye
Ok ,sawa,niko page ya tatu ndo maana,,ila huu uzi wauweke stick,,naona kama una manufaa sanaKuna mdau kaeleza kwenye huu uzi jinsi wanavyo nunua na kuzibadilisha.
Vichwa vinazidi kuja sasa.Kumiliki sania ni issue ndogo. Kazi ni kupata dereva mtulivu na anaeielewa gari. Pili ni nani na wapi pa kutengeneza gani lako na tatu unaifanyaje hiyo biashara. Ziko aina 4 za mfumo wa biashara ya malori hapa Tz.
1. Unaoperate kama kampuni, yaani unatafuta mzigo wewe, unantuma tu dereva na unampa mileji yake. Pesa zote unalipwa wewe tajiri.
2. Unasafirisha mizigo yako ya biashara zako. Hii ni kama una hardware etc.
3. Unakaa kushoto...unatembea na gari. Unapatana kila kitu wewe na kszi ya dereva ni kuendesha tu.
4. Hesabu. Unamkabidhi gari dereva, mnakubaliana route na unampa mtaji wa mafuta. Dereva anakuletea hesabu kwa mzunguko wa kwenda na kurudi. Wewe unabaki na matengenezo makubwa, service na tairi. Humlipi posho.
Kila moja ina faida na hadara zake.
Nimeifanya hiyo kwa miaka zaidi ya 30 sasa.
Ushauri.
Unapotaka kununua gari la biashara angalia bei za vipuri na upatikanaji wa mafundi wazuri eneo lako. Usikimbilie magari ya kisasa au ya nyuma sana au lenye milleage nyingi sana.
Scania ni chaguo zuri. Ushauri baki kwenye 124
Uzi umeanza kama utani utaniVichwa vinazidi kuja sasa.
Ushauri makini sana huu.
Mkuu
Fuso ni biashara ya dereva na sio mwenye gari. Uliza maswali ya msingi kwenye biashara.
Mfano.
1. Wewe unalenga kupata faida kiasi gani kwa mwezi?
2.Hiyo milioni 100 ni pikipiki ngapi na hesabu yake ni kiasi gani kwa mwezi1?
3. Je ni bajaji ngapi? Hesabu kwa mwzi je?
4. Taxi. Ngapi ? Mapato kwa mwezi?
5. Fuso za mchanga je.
6. Fuso za mizigo?
7. Trucks za tani 10? Mfano scania 94? 93 etc
8. Scania za tani 30 ? Nk
Utaona bei za Fuso tandam inafikia .ilioni 80 wakati hiyo ni 124. Hesabu zao kwako tajiri ni mbingu na nchi, pia matengenezo ya fuso ni makubwa.
Hata bima kubwa ya fuso iko juu sababu ya risk ya fuso.
Vinginevyo jenga nyumba pangisha ila kipato cha nyumba ya 100m kwa mwaka ni kipato cha 124 cha mwezi !
SHINDANISHA HUO MTAJI USIUTUPE TUU KWA MASIFA.
Chif vp kuhusu kuongeza chassis (yani kupanadanisha chasis ili isipinde)kwenye fuso,unauelewa wowote kwenye hii modification?Uzi umeanza kama utani utani
yuko mwamba mmoja bado sijamuona hapa, atakuja tu..ni anauelewa wa hv vyombo balaa , uelewa mkubwa mno
Huu mm naufanya kuanzia kwa fuso adi scaniaChif vp kuhusu kuongeza chassis (yani kupanadanisha chasis ili isipinde)kwenye fuso,unauelewa wowote kwenye hii modification?
Huu mm naufanya kuanzia kwa fuso adi scania
naona mdau hapa anajibuChif vp kuhusu kuongeza chassis (yani kupanadanisha chasis ili isipinde)kwenye fuso,unauelewa wowote kwenye hii modification?
Mkuu, ungeelezea gharama za huduma hiyo. Pia ungeelezea changamoto za magari hayo na gharama za kukarabati.Huu mm naufanya kuanzia kwa fuso adi scania
Hiyo 22 unanua used from Japan au hapa bongoMkuu sina uhakika na bei ila niongelee upande wangu huwa tunanunua Fuso ya kawaida yan single diff ambayo inakuwa bado nzma kabsa kuanzia milion 22 hadi 28, halafu tunaipeleka garage Moshi kwenda kuongeza chassis na kuwa Tandam.
Pia inarembwa na kufanyiwa kila kitu hadi ikitoka hapo inakuwa km mpya. Cost zote inaweza kusimamia milion 42 hadi 50 na gari inakuwa imesimama balaa
NB: hyo cost ya milion 42 had 50 ni kuanzia gharama ya kununua gari hadi kufanyia kila ktu.
Gharama za kazi hii hutofautiana kulingana na kazi itakayofanywa kwa gari hisika. Fuso zote za tani 3 huitajiwa kuwekewa double chasis ili ziweze kubeba tani 10 kwa single au 16 kwa tandamMkuu, ungeelezea gharama za huduma hiyo. Pia ungeelezea changamoto za magari hayo na gharama za kukarabati.
Mkuu hapo kwenye wanawake naomba urudie kwanza mana itanisaidia siku na mimi nikiwa na wazo kama la huyu bahariaMkuu,
Nikupongeze sana kwa uthubutu huu.
Hii biashara ni nzuri ila ina changamoto zake za hapa na pale ila ina pesa.
Ili uweze kutoboa kwenye hii biashara jitahidi kumudu jazba zako kwa dereva wako tena hasa akiwa porini , Dereva ndiye mtu anayeweza kukufanya ufanikiwe na kukufanya ufeli mazima.
Trailer zipo za aina mbili,
Flatbed na Skelton
Kwa vile wewe ndiyo unaanza basi nakushauri uchukue flatbed kwa sababu kazi zote utabeba. Vilevile uchukue Trailer yenye (axles za BPW).
Kampuni zinazozalisha hizo trailer zipo nyingi hapo mjini, Superdoll, Simba na wengineo, Nashauri ununue trailer za mtumba.
Kikazi,
Kuna trip za local( za ndani)
Kuna trip za transit ( Nje ya nchi)
Trip za ndani sikushauri uzifanye kwasababu zinachosha gari na magurudumu. Ni bora ufanye hizo za Transit tu, tena za Dar - Lubumbashi tu.
Trip za Dar - Lubumbashi hazichoshi gari ingawa gari inachukua mwezi mzima au zaidi lakini pesa yake unaiona, Gari inaenda na mzigo na inarudi na mzigo (Copper)
Sasa ili uweze kufanya hizo trip za transit kwa mtu wa gari moja, nakushauri ufanye joint venture na mtu mwingine ambaye ana gari nyingi ili uweze kupata c28 ya TRA na hii itakusaidia kujikusanya na kujifunza mchezo.
Kwanini nasema hivyo, sijajua mfuko wako ukoje ila kuna mlolongo wa makadirio ya kodi, kukata vibali vya Zambia na mambo mengine, kwa gari moja ni story tu.
Mkuu, Magurudumu ya gari yako hakikisha umenote zile serial number na uwe mfwatiliaji wa kuyakagua kila baada ya trip.
Dereva mtaji wake ni Diseal na Magurudumu, akiishiwa huko njiani anayanywa fasta na yanauzika sana hapo Tunduma au huko Mpika.
Punguza wanawake (Mademu) magari ni kama Majini hayapendi uchafu wa mwili, na pia dereva asikuzooee sana maana wanakuwaga na vinasaba vya kiswahili unaweza kujikuta yeye ndiye kawa boss na wewe ukawa mfanyakazi wake. Zingatia Services ya gari, usifuge magonjwa kwenye gari!
Naomba niishie hapa,
Cheza na dola mkuu.
Shukrani
Asante kwa taarifa mtaalam. Je bei ikoje kwa tani 10 na tani 16.Gharama za kazi hii hutofautiana kulingana na kazi itakayofanywa kwa gari hisika. Fuso zote za tani 3 huitajiwa kuwekewa double chasis ili ziweze kubeba tani 10 kwa single au 16 kwa tandam