Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?

Nataka kumiliki Scania R450. Je, pesa itarudi baada ya muda gani?

Hii biashara asikuambie mtu ni nzuri ukianza na dereva awe mzuri. Dereva atakuwezesha kuwa kwenye reli ama lah. Hata gari iwe mpya kiasi gani kama deree ni pasua kichwa ni changamoto Sana...

Hapo komaa na 124 itakufaa sana Kwa unaeanza kama wewe..
Ukitaka ruti ambayo sio pasua kichwa nenda dar nyanda za juu kusini mbeya,Iringa ,njombe huko. Ule mfumo wa mdua kuwa unaenda na mzigo unarudi na mazao utakufaa Sana..
 
Wakuu,

Niseme machache.

Marehamu Rugemalila Mutahaba aliwai kusema maneno haya, naomba kumnukuu" Ukifanya biashara na haikupi changamoto basi hiyo biashara haina faida achana nayo"

Akaenda mbali tena, Mjasiriamali wa kweli ni yule anayebadilika badilika huwez kukomaa na biashara ya aina moja tu kwa wakati wote, Mwisho wa nukuu.

Hii biashara ina changamoto zake lakini ina pesa, sehemu yeyote yenye changamoto pesa inapatikana hapo.

Scania 113M ni horse nzuri lakini ina mapungufu yake, hii gari haitumii umeme mwingi na ulaji wake wa diseal ni mkubwa, lakini pia haina Kitanda.

Kwa mfano trip ya Dar -Lubumbashi, halafu Lubumbashi - Dar hiyo gari inatumia diseal lita 2400 na muda mwingine mpaka 2500 wakati scania 114L, 124L inakula lita 2200.

Kwa ushauri wangu, unaweza kuanza na scania 114L yenye horse power 380 cabin ndogo. Au ukishindwa sana basi chukua DAF XF 95 manual, (camis engine)

View attachment 1484869

View attachment 1484870

Kama nilivyosema awali, Dereva ndiye mtu muhimu sana atakaye kutoa hapo ulipo mpaka sehemu uliyopanga wewe kufika. Tatizo kubwa kwenye hii biashara wamiliki wengi wanamchukulia dereva kama barmaid.

Dereva mzuri unampataje? Madereva wazuri siku zote wanaibwa kutoka kwenye makampuni mengine.

Tengeneza mofolojia ya kazi yako vizuri, kwa mfano kuna kampuni X inamlipa dereva mileage ya kwenda Lubumbashi na kurudi dar TSHS 1milion

Kiaje? Dereva anapewa shs 500k kwenda Lubumbashi na anavyoingia Mgodini kupakia copper unampatia dola 100, akirudi dar unampa shs 300k kama return mileage. Sasa dereva kama huyo kwanini asiheshimu kazi na kutunza gari lako vizuri..!

Kwenye hii kazi reporting ni muhimu sana, mwenye mzigo wake anataka kujua gari iko wapi na imelala wapi? Sasa ili uweze kwendana na hii ari huna budi kutengeneza Kanuni ambayo itakuwa kama katiba ya kazi ofisini kwako.

Dereva aanze safari saa moja asubuhi na ikifika saa kumi na mbili jioni apaki gari atafute guest alale na atume ujumbe kwako kukupa report. ( Kuwa mkali sana kwa dereva anayepuuzia hili)

Madhara ya kutembeza gari usiku ni makubwa sana na yanaweza kukufilisi kabisa na ukajuta kwanini uliingia kwenye hii biashara ya magari kama wanavyoelezea wadau hapo juu.

Breakdown, jitahidi sana kuepuka hitilafu za njiani, funga spare za uhakika ambazo utaweza zipata sub-scania au kwenye maduka mengine ambayo yako vizuri.

Na unapopata breakdown najua kichwa kinawaka moto na pressure inakuwa juu, jitahidi sana kujicontrol, pokea simu ya agent aliyekupakilisha mzigo au mteja mwenyewe mwambie ukweli na umpe uhakika wa usalama wa mzigo wake na uhakika wa kutoka hapo ulipo nasa.

Kutokupokea simu za hao watu kutakuharibia sana na siku nyingine utashindwa aminiwa na ukizingatia ndiyo kwanza unaanza.

Kwenye hii biashara tuna utatu mtakatifu, ambao ni Dereva, Agent / Wakala wa mizigo na Fundi wako wa gari, Hawa watu ishi nao vizuri, kuwa nao karibu kushindwa mchepuko wako.

Chonde chonde usiruhusu lori lako kubeba mkaa, (kama ni kagunia kamoja basi akamwagie maji ndiyo akabebe)

Rate za mizigo sokoni huwa zinabadilika kutoka na ari ilivyo kwa wakati huo na kabla ya kumpatia agent nyaraka zako za gari basi jiridhishe kwa kufanya utafiti kidogo wa bei maana nao ni watafutaji kama wewe.

Shukrani sana!

Muwe na jumapili njema iliyobarikiwa
Kwanini kubeba mkaa? Nifumbue hapo
 
Back
Top Bottom