Nataka kuuza nyumba, viwanja, gari na vitu vyote vya ndani nirudi bara kuanza upya kutoka Zanzibar

Wazo langu ni kuuza hv vyote walau nipate 150M to 140M
Ushauri: Tuliza kichwa kwanza! acha papara, mhemko, hisia, uharaka na msukumo! Kumbuka: Akili na maarifa ndiyo huleta hela mpaka utajiri!

1000 ni ndogo ila pia ni nyingi! Bilioni moja ni nyingi lakini pia ni ndogo! Unatakiwa ufahamu si kila anaweza kuzalisha hela hasa kwa makuzi na malezi ya watoto wa Kitanzania!

Watanzania tumekuzwa hivi:

Kuzaliwa-nenda shule -ukasome kisha ufaulu -halafu uajiriwe serikalini-Halafu ufe!
 
Tuliza akili tajiri, kibinda unacho idea unazo ila acha pupa.

Yaani unataka kufanya biashara zaidi ya 4 kwa mkupuo kwa hela hiyo hiyo.

Anza na hiyo utakayoisimamia wewe, hizo frem nyingine kama utajenga, pangisha kwa watu wenginr ili wakuletee wateja kwenye hiyo biashara yako ya duka.
 
Kiukweli jamaa wa unguja hawapendi kabisaaa kuona mtu anayetoka bara anafanikiwa, sijui ni kwanini..??

Watakupa chakula ila sio mafanikio, ili ufanikiwe lazima uwe mjanja

Kingine, wanakemea sana watoto wa wenzao kuingiza wanawake/wanaume kwenye nyumba za kupanga... Lakini watoto zao hasa wa kike hawashindi nyumbani mwao, kutwa kushikana viuno beach, watoto wao wa kiume wanavuta sana bangi na sigara
 
konakona nyingi sana ndio unapata ardhi...
 
Ila ku supply nako changamoto saivi.....suppliers washakuwa wengi
 
Asante kwa ushauri 🙏
 
Uza viwanja ila nyumba usiuze nitafute inbox nikushauri unaweza kufanya nini?
 
Asante sana kwa ushauri 🙏
 
Zanzibar bado fursa ni nyingi, hiyo nyumba uliyonayo inakupa pesa... Pangisha vyumba ama viwili, tumia kimoja.... Alphard ichukue mwenyewe piga kazi... Japo kwasasa ni low season... Tumia network uliyokuwa nayo wakati upo kazini... Huwezi kosa ya mafuta kwa siku
 
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…