Nataka kuuza nyumba, viwanja, gari na vitu vyote vya ndani nirudi bara kuanza upya kutoka Zanzibar

Nataka kuuza nyumba, viwanja, gari na vitu vyote vya ndani nirudi bara kuanza upya kutoka Zanzibar

Wewe ni :

mjinga


1.mtu asiyejua kitu au jambo fulani


2.tamko la dharau au tusi kwa anayechukuliwa kutojua kitu


Nb: Njia za kumiliki ardhi zimerahisishwa sana!
Unaweza kuonyesha Ujinga wangu uko wapi?

Kwa sheria ya Sheria ya Kamisheni ya Ardhi namba 6 ya mwaka 2015,
na Sera ya Taifa Ya Ardhi Zanzibar ya mwaka 2008 na marekebisho yake mwaka 2018,

Sheria ya Umiliki wa Ardhi Nam. 12 ya 1992;

Sheria ya Baraza la Ardhi Nam. 7 ya mwaka 1994,

umezisoma?
MTanganyika (Tanzania Bara) Haruhusiwi kumiliki Ardhi Zanzibar na atamiliki kwa kufata Taratibu kama Mwekezaji anavyofanya yaani kama Mzungu au mtu mwingine
 
Nimepita Zanzibar itoshe kusema tu huko mahotelini Kuna pesa sana, Kuna jamaa mmoja muhindi allifungua clinic ndani ya hotel flani anawalipisha Wazungu Dollar 100 kama consultation fee hata kama mzungu ana mafua hapo bado dawa kiufupi yule kabachori alikuwa anavuna sana pesa.
 
Nimepita Zanzibar itoshe kusema tu huku mahotelini Kuna pesa sana, Kuna jamaa mmoja muhindi allifungua clinic ndani ya hotel flani anawalipisha Wazungu Dollar 100 kama consultation fee hata kama mzungu ana mafua hapo bado dawa kiufupi yule kabachori alikuwa anavuna sana pesa.
Itabidi nirudi nikapige mishe huko
 
Wewe ni :

chizi

1.mtu afanyaye mambo ya kihunihuni


2.mtu mwenye wazimu au mwenye akili kidogo
mm ni chizi ila ww ni punguani yan mnajifanya wajuaj sana ktk maisha ya watu jitathmin,yan ulicoment km mchawi alietoka kuwanga inaonyesha ni jins gn unaroho ya makasiriko kwa mamb yasiyo na ulazima,

Mchiz kaomba ushaur kitu ipo wazi ww unaanza kumuuliza maswal ya kimandazi
 
Uza kiwanja nunua bajaji 3 huku Dar. Wape vijana kwa Siku elfu 20 bajaji moja. Utaishi vizuri tu
 
MTanganyika (Tanzania Bara) Haruhusiwi kumiliki Ardhi Zanzibar na atamiliki kwa kufata Taratibu kama Mwekezaji anavyofanya yaani kama Mzungu au mtu mwingine
Katika kitu ambacho kimefichwa kwa ajili ya kuboresha muungano wetu ni hiki:

unwritten law : law based chiefly on custom rather than legislative enactments​


wewe njoo na NIDA kama hupati ardhi hapa Zanzibar!
 
Ndugu wana JF poleni na kazi na mihangaiko ya maisha.

Mimi ni kijana wa miaka 29 mzaliwa wa Morogoro na kukulia DSM hasa maeneo ya Tandika! Nilipohitimu masomo yangu pale UDSM 2017 nilikuja Unguja mwezi wa 7 mwaka huo huo kujaribu bahati yangu, kilichonileta ni soka na alieniunganisha na hio timu ni rafiki yangu. Lkn ligi ya Unguja hailipi kwa mwaka huo ilikuwa ni kujitolea tu.

Mwishowe nikaongea na mwenye timu kuwa maisha ya soka yamenishinda narudi nyumbani, yule tajiri aliuliza kinachonisibu na mimi nikamueleza, Lkn alishangaa sana kusikia mimi ni muhitimu wa chuo kikuu na nimekosa kazi mpaka nimeamua kuja kucheza mpira ili nipate kula.

Yule tajiri alitokea kunielewa sana, akanambia nisiondoke na pale kwenye nyumba ya timu mtaani atanihamisha nitakaa peke yangu na atanitafutia kazi na kweli alitimiza, Mwaka uliofata yaani 2018 mwezi wa 8 niliajiriwa kwenye taasisi moja inayojishughulisha na masuala hapa Unguja.

Ile taasisi ilinibadilishia maisha yangu sana kwani ndani ya muda mchache nilikuwa miongoni mwa wafanyakazi tegemezi pale kwenye taasisi, elimu yangu ikanisaidia kupata nafasi nzuri na mshahara mzuri zaidi kwani wengi wa waajiriwa walikuwa hawana elimu kubwa na wengi ni mabeach boy tu wa mtaani.

Maisha yalibadilika sana ndani ya muda mfupi safari za Dar, Arusha, Zenji kwa mwewe ilikuwa kawaida sana kwangu, nilipata pesa nyingi pia nje ya mshahara wangu, Nyingi zikiwa ni tips toka kwa wageni tukiwa safarini.

Mimi napenda sana watoto na wageni wengi wenye watoto walikuwa hawawezi kuniacha hivi hivi maana watoto wao walinipenda kwa muda mfupi na mara nilipojua hili shimo nililishikilia kweli kweli japo corona ilifanya taasisi ikayumba kidogo na baadhi ya wafanyakazi kupunguzwa lkn nashukuru sikuwa miongoni mwao.

Wakati wa corona mabosi walishindwana (Nasema mabosi kwa kuwa taasisi ni share older ya watu watano), Baadhi walitaka kampuni ifungwe kupisha janga la corona na wengine walisisitiza kazi ziendelee hata kama ni kwa hasara Ila jina la kampuni liwe midomoni mwa watu, Mvutano huu ulipelekea muanzilishi mmoja wa kampuni kujitoa na kudai share zake na akapatiwa na kuletwa share holder mwingine (Huyu aliyejitoa ndio aliyenipa kazi baada ya kuuganishwa na yule jamaa mwenye timu)

Kutokana na changamoto ya corona, mshahara ulipunguzwa sana na tukawa tunalipwa kama posho tu. Hali hii ilifanya niingie bank kucheki balance yangu na nikakuta nina namba nzuri tu kwenye account zote mbili (Ya Tsh na Dolar) nikaamua kununua viwanja vitatu hapa Unguja, nikanunua Alphard pia nikampa mtu aifanye private hire na nikawa nampa wageni wa pale kazini wanaotaka usafiri kwa siri kubwa maana hairuhusiwi taasisi ina magari yake pia inakodisha. Nilibakiwa na pesa kidogo sana kwenye acc kw ajili ya kula na matumizi madogo madogo maana ardhi ni ghali sana Unguja hasa maeneno jirani kama Kisauni, Mbweni, Kiembe Samaki, Chukwani, Fuoni, Kwerekwe nk!

Penye rizki hapakosi fitna wahenga walisema, kuondoka kwa yule bosi mmoja ikiwa kama kinga niliyokuwa nayo pale kwenye taasisi imeondoshwa na hapo nikaanza rasmi kuoneshwa mm sistahili kuwa pale, kwanza nikondolewa nafasi niliyopewa kwa kigezo kuwa mimi sijasomea masuala ya utalii japo hakuna yeyote aliyesomea wengi wamesomea lugha tu Kifaransa, Kipoland, Kirusi, Kitalina nk, kuondoshwa kwa hiki cheo kukafanya nibaki nategemea mshahara tu though haukuwa mdogo mana ni tarakimu 7 lkn nilipoteza pesa nyingi nilizokuwa napata kwenye kuandaa safari za ndege, hotel, chakula, sehemu wanazotembelea wageni nk

Wageni wengi walinizoea na walikuwa wanatoa recommendation nzuri dhidi yangu hiyo hata ofisini nikawa sikosi mia mia nje ya mshahara, lkn kadri muda ulivyokuwa unaenda nilianza kuona visa na mikasa, ubaguzi wa wazi wazi dhidi yangu! Mtu anakuchokoza kwa kukuita kafiri kisa tu muda wa kuswali umefika na wewe hujaenda kuswali ama hujasitisha huduma, wengine wanakuita ukawa timu pinzani, wengne wanasema aliyekuleta kaondoka wewe unafanya nini ilimradi tu ujibu ukatwe mshahara ama usimamishwe kazi nk

Haya tote yalianza kunikinaisha na ile kazi maana sasa nilikuwa simalizi miezi 6 bila adhabu kusimamishwa bila malipo ama kukatwa mahahara hata “Akijamba Mwantumu naambiwa nanuka mm” hii hali ilinikera sana. Lkn mtoto wa maskini hadeki niliendelea kuhustle kama kawaida nikijituma huku na kule na mwaka jana mwanzoni nilifanikiwa kujenga nyumba kwenye moja ya viwanja vyangu, Nyumba ya vyumba vinne viwili vikiwa ni master, jiko sebule na dining na stoo nikaipiga fence tamu sana nikaiacha ikiwa inahitaji finishing ndogo sana za ndani lkn rangi madirsha milango tiles mafeni gypsum tyr kifupi ni complete house

“Barabara hata iwe ndefu vipi haikosi kona kona, mwaka Jana mwez wa 6 yule dereva wangu nilimpa wageni 7 wanataka kuzunguka shamba (Shamba ni eneo nje ya mji hapa Unguja, Huko kuna mahotel na starehe nyingine nyingi) wale wageni wakaomba waongozane na mmoja wa mwenzetu pale ofisini, Hapo ndo kitumbua kiliingia mchanga kwani wakiwa njiani yule mwenzangu aliisifia gari kuwa inatunzwa vizuri iko fresh sana na yule dereva wangu ndipo akaropoka kuwa gari ya boss wako X hii.

Jamaa akachimbwa na yule mwanamke akamfungukia kuhusu nyumba na mengne mengi anayoyajua kuhusu mimi. Kesho yake nikaitwa na boss kuulizwa kwanini wageni hawakodi magari ya ofisi na badala yake gari fulani linaonekana kubeba sana wageni wa kampuni hasa wale wanaopita kwenye mikono yangu!

Nilijitetea sana kwamba yule jamaa bei zake ni nusu ya zetu na wageni wengi ni vishuka (hawana pesa) ndo maana nampa yeye kuiepusha taasisi na hasara lkn maelezo yangu hayakufaa kitu! Boss alikuwa anajua kila kitu na mwsho akanipa barua ya kunisimaisha kunifukuza kazi. Nilimsihi sana anisamehe lkn haikufua dafu sana alisistiza nilipokula na kuihujumu taasisi pametosha.

Wakati huu sikuwa na akiba yoyote bank maana ndo nilitoka kumalizia ujenzi nikabaki nasubiri pesa za kwenye gari niwe nakula lkn jamaa nae akwa analalamika kukosa wageni hivyo pesa ikazidi kuwa ngumu na tayari nilikuwa nawasaidia ndugu zangu wengi hivyo nikaanza kuona pengo sasa.

Nikauza kiwanja kimoja mwak jana mwezi 10 ili nijitafute lkn imeshindikana ile pesa nimeishia kuila tu na kusaidia ndugu! Sasa nimebakiwa na kiwanja kimoja ambacho nilikinunua 18M thamani kwa sasa inaweza kufika 25M mpk 22M, 20M ikawa bei ya chap kwa haraka, nina Alphard japo biashara haiendi nimechoka kugombana na madereva, na nina nyumba ambayo thamani yake inaweza kufika 100M kwa hapa Unguja.

Wazo langu ni kuuza hv vyote walau nipate 150M to 140M Kisha nikanunue nyumba 3 Tandika za 15M each, 2 nizipangishe na moja niifanyie ukarabati niweke flem zangu Tatu nifungue duka la chakula na mahitaji yote ya nyumbani na nje niweke genge, flemu ya pili nifungue glosary ya kawaida ya mtaani na nje niweke chips na flem ya Tatu nifungue mama lishe!

Hili ni wazo langu naomba ushauri zaidi hata ulio nje ya huu wana JF.

NAWASILISHA.
Nawachukia mno wazanzibari.

Huu muungano wanaoung'ang'ania wana faida nao ila sisi wananchi wa kawaida hatuutaki hata kuusikia.
 
Kwa nini usendeshe gari yako mwenyewe,deal za kuchukua wagen toka airport to any hotel ziko wazi na nying znz,pili kwa nini usipangishe nyumba yako.watu wengi wanaofanya kazi za ma hotl znz hupanga chumba kimoja kimoja. Shamba anza ukulima kuliko kuuza.hivyo vitu ulivyonavyo ni asset nzuri maishan acha uoga.pambana jiajiri.hao ndugu wafike mahali waeleww unaanza upya.ww ni tajir tayar kuna watu hawana hata pa kulala,
Wazo zuri
 
Mkuu bajaji ni bei gani kwa Dar mpya?
Mkuu naona kama homesick inakusumbua umepakumbuka sana nyumbani si ndiyo?

Ushauri wangu fanya yote ila usije kuthubutu kuuza hio nyumba coz nyumba zanzibar zina thamani sana kutokana na ufinyu wa ardhi

Ni bora ukakomaa na hyo gari huku unaangalia upepo unavuma vipi! Kurudi huku bara halafu mambo yakuharibikie hata hao ndugu zako unaowasaidia watakukimbia
 
Hio sheria ni kweli ipo.ila haipo.enforced ndio maana wapo wabongo wengi wanamiliki Ardhi Zanzibar , nina wadau wangu Tanga nimekuwa nao wanaishi Zanzibar na wamejenga kabisa.
Tanga na Zanzibar Ni kama Kitu kimoja..
Mimi Mzaliwa wa Zanzibar na Nimekulia Tanga..
Nilihamia Tanga mwaka 1987..

Wengi wa Tanga Sana sana Pangani wanajiita wazanzibar..
Na zanzibar Mara Nyingi wanadai Tanga iko.kwao na Bagamoyo...

Watu wa Tanga Wengi Nikiwemo Mimi Tuna familia Huko zenji na ndugu pia..
 
Back
Top Bottom