Nataka kuuza nyumba, viwanja, gari na vitu vyote vya ndani nirudi bara kuanza upya kutoka Zanzibar

Ni kweli kabisa na baadhi ya maeneo ya Bagamoyo
 
Usiuze ulichonacho, endelea kupambana upate kingine.

Chukua arphard yako endesha mwenyewe uku ukisikilizia mchongo.

Hiyo 150m itaungua na uwe chizi.
 
Kijana usiuze nyumba wala gari.Nyumba yako ifanye kuwa bnb au itangaze huku bara am sure watu wengi tu wanakuja huko weekend unawakodishia gari chukua wageni wakifika unawachaji kuwapeleka kwako na nyumba unawachaji kwa siku watakazo kaa huwezi kulala njaa hapo hizo nyumba unazotaka kununua tandika hela yake utaipata kupitia hio nyumba ya zbar na gari .
 
Mkuu Asante sana. Nakupm unipange zaidi
 
Ushauri mzuri ila asipoufata ipo siku ataukumbuka...
 
Mkuu pole kwa maswahibu, nina rafiki wakike mtu wa bara, ambaye ana gari ya kawaida tu, amepanga mbweni na ana kikampuni cha mfukoni tu japo ana vibali vyote hence analipa kodi, kazi yake anapokea watalii na kuwapangia safari, na hii kazi amejifunza mwenyewe bila msaada wa yeyote, mwaka wa 4 huu yuko kwenye game. Changamoto gari yake ni ya kawaida/ haiko licensed kubeba abiria/wageni, lakini anakomaa nayo tu, hata akikamatwa na matrafiki “yanazungumzika”.

Wewe ambaye umetoka kwenye reputable organization, una experience nzuri, una support system (your former Boss) una gari nzuri, naona uko kwenye nafasi nzuri zaidi ya kufanya vizuri, unless una tatizo lingine au umepamiss kwenu.

Wazanzibar hawa ni wakuishi nao hivyo hivyo tu, samaleko nyingi ilimradi yako yanaenda.

Usikate tamaa, binafsi naona ukiamua kukomaa utafanikiwa, tena una pakuishi kabisa. Labda kuna mengine haujayasema.
 
Hizi Dini tumeletewa tu na wala hakuna Dini itakayompeleka mtu mbinguni, kwanza asilimia kubwa hatujachangua Dini tuliyopo tumefata Dini za wazazi wetu Mimi nikifika maeneo Kama hayo na nikaona salama yangu ni kubadili Dini Hata sijiulizi Mara mbili.
 
Sijapenda hapo tu uliposema "wavaa vipedo" kwa kuwa unabagaza imani za watu lakini ni ukweli usio na shaka wazanzibar (wengi wao) ni wabaguzi na haubaguliwi kwa kuangaliwa dini yako tu bali unabaguliwa kutokana ubara wako.
 
Pole sana kwa maswahibu mdogo wangu.

Hongera yako angalau wewe una kitu sema ni changamoto tu za dunia zinakusibu, pambana nazo.

Nakushauri usiweke hela zote katika biashara moja..

Uza hivyo vitu vyako ila usije ukajiingiza kwenye makundi yasiyo na maana
 
Katika kitu ambacho kimefichwa kwa ajili ya kuboresha muungano wetu ni hiki:

unwritten law : law based chiefly on custom rather than legislative enactments​


wewe njoo na NIDA kama hupati ardhi hapa Zanzibar!
Na kitambulisho cha Mzanzibari atapewa bila usumbufu. Wengi wa watanganyika wanavyo.
 
Pambania gari Yako beba wagenj utateleza sana ila utasimama....hakuna kazi rahisi tunajikausha tu....
 
Yah nimefanya research kabla na nimekulia sana maeneo Yale! Thow izo nyumba hazina finishing nzuri lkn ndo zilivyo nyumba nyingi za Dar hasa maeneo ya uswazi
Mwanangu unaenda kuuziwa nyumba za udongo wewe! Labda kama nia ni kupata kiwanja!
 
Hapana mkuu hakuna ambalo sijasema, hakuna nililoficha. Asante sana kwa ushauri. Nimeupokea
 
Ila ku supply nako changamoto saivi.....suppliers washakuwa wengi
Kila sehem ni mapambano. Dunia uwanja wa vita! Uzuri wa Zanzibar uchumi wake ni hybrid yani sio wa kitanzania Moja kwa Moja. Huyu akirudi dsm anaenda kupambana na uchumi wa mtanzania halisi... Kabla ya yote kwanza atafute mganga
 
Ni vyem kuhama huko hasa kam utategea kaz za watu wa zanzbr wata kunyanyasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…