Mkuu Fiber inaChimbiwa Chini kama dawasco, imagine tu kutoa Mfereji Mjini mpaka mwananyamala, gharama kiasi gani? Bado waya za Fiber, Nguzo, manpower, Router na mambo mengine kibao. Sina Cost za kibongo bongo sababu hawapo wazi ila kwa nchi za Wenzetu inaweza fika Hadi milioni 200 kwa KM, ila sababu huko ulaya manpower ni gharama sana assume huku haitafika hivyo, ila still ni hela Kubwa, kwa Cost ya 70,000 kwa mwezi unaweza pata watu angalau 1000 mwananyamala?
Ila kwa serikali Hio ni Hela Ndogo TTCL wanaweza Fikisha Fiber hadi hayo Maeneo na kampuni Binafsi zikawa zinasupply tu Mtaani.
Unaongelea mwananyamala ila huongelei toka huko mjini mpaka mwananyamala umepita potential clients wangapi.
Unaweza pata wateja 50 mwananyamala ila njia nzima ukapata wengine 150.
Lakini bado watu hawajawa na ile awareness ya hidden costs za vifurushi vya simu vs fibre.
Akipatikana mwekezaji jeuri mwenye pesa yake akatawanya fibre dar nzima akafanya kampeni ya nguvu na huduma zikawa reliable, ndani ya miaka 5 atakuwa anasumbua sana.
Mfano, ukitoa fibre toka posta mpaka bunju, hapo kati utakuwa ume-cover wateja wangapi? Kuna mahospitali, vituo vya afya, garage, migahawa, malls, offices, mashule na vyuo, petrol stations, offices, viwanda, maduka ya aina mbalimbali, wedding halls, makanisa, hotels, masoko n.k.
Watu wanajaa Grano Coffee kwasababu ya wifi ya bure na sio ile kahawa, wengi wanapatumia kama working space or meeting point.
Kwahiyo nadhani inaonekana ni gharama kupeleka huduma ila hatujajua opportunities zinazokuja baada ya hapo.