Nataka nikusanye kiasi cha million 25, nitumie mbinu gani?

Nataka nikusanye kiasi cha million 25, nitumie mbinu gani?

Kazanazo

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2023
Posts
7,875
Reaction score
12,665
Kazi ninayofanya inanipa take home ya takriban 500k - 800k per month sasa nahitaji kusave hadi nifikishe kiasi cha sh 25mil kwa ajili ya kutimiza lengo langu (lengo kapuni). Mwaka jana nilijaribu kuhifadhi kwa kucheza kikoba kupitia jina la mama mtoto wangu lakini tuliishia kukopa kwa ajili ya shida zilizotokea kwenye safari ya kusave pesa hivyo nikashindwa kurejesha mwishowe lengo halikufanikiwa

Je ni mbinu gani sahihi nikiitumia nitaweza kusave 25mil? Kiasi gani ni sahihi kuweka na kwa muda gani kulingana na kipato changu?

Karibu
 
Kwa hicho kipato , laki 5-8, huku una familia .... ni ngumu sana kufikia hilo lengo la 25m, labda ukope huko kazn kwako, ama ni mfanyabiashara sijajua!!!

Ushauri ! Buni chanzo kipya cha Mapato, then save na jibane sana pengine ndani ya 3yrs ukawa na hio pesa
 
Mkuu, muhm kucheza na budget yako kwanza uone matumiz yako halafu anza mdogo mdogo hata walau 100k au 150k kwa mwezi uanze kuisave kwa kutumia vicoba, m-wekeza au UTT [Liquid] ambapo ufanye hivo walau kwa mwaka ili uone unaweza kufika hatua gani, Lakini kama unaweza ukaanza mishe nyingine mbal na salary itasaidia zaid
 
Back
Top Bottom