Mkuu unawazo zuri sana tena hadi nimependa arif,hizo ndio target za kiume unapoingia kufanya kitu unawaza mambo ambayo wengine wanaona Huwezi au unajitekenya mwenyewe.
lakini ukweli ni kwamba katika mawazo bora uliyonayo hilo nalipa no 1,target ni 100k chicken hauzwi kuku haliwi kuku mpka kufika Target,binafsi ni mfanyabiashara wa Gas wakati naanza nilisema nahitaji mitungi 1000 ndipo nianze kula faida ya Gas,
Nilionekana kama naota hivi,nilipokua naongea na wafanyakazi,wazazi wangu,na wale watu wangu wa Karibu lakini hivi sasa naelekea kufika tube 2000 nishafika buku kitambo saivi naitafuta 2000 by december iwe store. (inawezekana)
Shida ninayoiona kwako katika wazo lako ni 1, una wazo zuri lakini huna mikakati ya kukamilisha wazo lako,Kwa wingi huo wa kuku hutakiwi kuwaza Eneo,sijui dawa unazijua nk nk, unatakiwa uwaze namna ya kutengeneza chakula cha kuku wako,unatakiwa kujifunza namna ya kutengeneza dawa za kuku wako.
Project yako ni kubwa sana mkuu,kuku 100k ukirusha drone juu ukasema uwapge picha utasema ni Siafu wala hutosema ni kuku kwa namna watavyoonekana.
Hivyo basi nini ufanye ili ufanikishe hilo Wazo lako, kwanza unatakiwa uwe na uhakika wa chakula, Je pesa unayo? ni wazi pesa hauna hivyo unategemea ufugaji ukutoe, kwa project hiyo haitaki mtu type yako anaetemea kuku ndio wajilishe waljitunze,nk
Unahitaji kuwa mfanya biashara au mkulima,unaweza ukachagua kati ya kufanya biashara ya mazao au kulima mazao ambayo end product yake ni chakula cha kuku mfano Alizet au mahindi,nk
Ukiamua kuwa mfanyabiashara wa mazao ambayo end product n chakula cha kuku utatoboa, au uwe mkulima Lima alizeti lima mahindi,nk nk,ukisema ununue chakula chakuku Hutoweza nunua chakula cha kuku wa kienyeji.
Kuku wa kienyeji wanakula na wanahtaji madini mengi hivyo chakula chao yabidi uwe wewe bnafsi ndio mtengenezaji,kadhalika na dawa ujue namna ya kutengeneza dawa tofaut tofaut, ukifanikisha eneo hilo basi kuku hao utawamudu bila mashaka hawatokushinda.
ila ukisema utaenda kununua chakula sikweliHuwezi fanikisha utashndwa tu,ukisema ukanunue dawa si kweli utaanguka Tu,anza na msingi wa kuku wako mahitaji makuu ni mawili, DAWA na CHAKULA eneo unalo,andaa mazingira ya chakula cha kuku either uanzshe biashara ya chakula cha kuku au uwe mtengenezaji wa dawa zao.
Fanya kama mimi,nina Plan ya kujenga DREAM HOUSE lakini siwezi sema nitaanza jenga sasa hv kidogo kidogo hadi ikamilike HAPANA,nikisema niweke hela bank pia ni kuchezea muda tu.
Nilichoamua kwasasa nimefungua biashara ya HARDWARE hii hardware inauza material zote nitakazokuja tumia ktk ujenzi waangu siku ikifika,kwasasa imeanza nauza vifaa yani kila unachokijua kuhusu ujenzi wangu nauza,naweka mdogo mdogo taratbu hela yangu inaendelea kujizungusha kuptia hii biashara,Lakini lengo langu si Biashara ya Hardware,lengo langu ni kuandaa mazingira yatakayoniwezesha kuja kujenga DREAM HOUSE yangu.
siwezi nunua kila kitu kwa reja reja,ila ukifanya biashara ya hardware utajua m,aterial zipi fake,zipi bora zinauzwaje zinapatkana vipi,nitajua mengi,Muda wangu ukifika nyumba nitakayojenga ama kwa hakika lazima waseme nimetoa mtu kafara.
Lakini kila kitu ni PLANS je umejiandaaje kupokea kuku Laki, usichukulie kuku Laki ukahisi wakifika Laki watakua laki Tu,Hao ni wazazi LAKI umeongelea watoto zao (vifaranga) wanaolalia,nk mzee kufika kuku Laki makadirio utakua na kuku sio chini ya 500k jumlisha na vifaranga, umejiandaaje kupokea hii project mzeee, usiangalie kirahisi juu juu.
Anza na Mzizi wa project yako
CHAKULA
DAWA
MAZINGIRA
WAFANYAKAZI
ULINZI
DHARURA
anzia huko chini kabla hata hujaanza kufuga hao kuku,ukishakamilisha hivyo vitu haya anza sasa Ufugaji wako,kama hujamilisha hivyo vitu usianze wala usijaribu.
utakua n sawa na baba anaetaka mpa mimba mke wake wakati hajaandaa mazingira ya namna huyo mtoto akija atakula nini,atasomaje,atavaa nini,nk nk usiwe na tabia hizo mazingira ya kijacho huandaliwa kabla hajaanza kutafutwa.
Mazingira ya project yako huandaliwa kabla hujaanza hiyo project. ASANTE kwa Muda wako, zaidi tu niseme komalia hapo hapo.