KERO Natakiwa kulipwa Milioni 7 ya NSSF, nimepewa 198,000, nyingine hadi mwaka upite, wanajua kesho yangu?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kero yangu ni kwa watu wa NSSF, nilikuwa nafuatilia mafao yangu ya ukomo wa kazi kwenye statement yangu kuna shilingi 7,000,000 kazini nilikuwa nalipwa 600,000, hivyo NSSF nilikuwa nawekewa 120,000 sasa imefika wakati wa kufatilia nakuja kulipwa Shilingi 198,000.

Sasa hiyo hela mimi naifanyia nini kusema kweli, huu ni unyanyasaji eti watakuja kunilipa baada ya mwaka ikiwa sijapata kazi.

Sasa wanajua kesho yangu? Kwanini wanipangie masharti mimi nataka kufanya biashara zangu, kazi zenyewe ngumu kupata, halafu wanakuambia hela watakupa ukizeeka, jamani hawa vijana wote tuchanganyikiwe!
 
Social Security ni Ponzi scheme. Ni legalised theft.

Nje ya mada: Ukiwa mfanyakazi, huwa inaaminika kwamba wewe huwezi jiongoza achilia mbali kusimamia pesa zako. Ndio maana mshahara pia unaongezwa kwa mbinde. Mafao yanatoka kwa kuviziana, kudai sana na wakati mwingine kuzinguana na watoa mafao. 😊
 
Kero yangu ni kwa watu wa NSSF, nilikuwa nafuatilia mafao yangu ya ukomo wa kazi kwenye statement yangu kuna shilingi 7,000,000 kazini nilikuwa nalipwa 600,000, hivyo NSSF nilikuwa nawekewa 120,000 sasa imefika wakati wa kufatilia nakuja kulipwa Shilingi 198,000.

Sasa hiyo hela mimi naifanyia nini kusema kweli, huu ni unyanyasaji eti watakuja kunilipa baada ya mwaka ikiwa sijapata kazi.

Sasa wanajua kesho yangu? Kwanini wanipangie masharti mimi nataka kufanya biashara zangu, kazi zenyewe ngumu kupata, halafu wanakuambia hela watakupa ukizeeka, jamani hawa vijana wote tuchanganyikiwe!
Sheria moja ya kijinga Sana iliasisiwa kipindi cha jiwe
 
Not sure, je uliomba fao la kukosa ajira? Ilipaswa wakulipe 33% ya mshahara wako wa mwisho kwa miezi 6. Then baada ya miezi 21 unaweza omba yote iliyobaki.

Je uliomba fao gani?
 
Mzee nssf ni utapeli wa waziwazi.
Mimi nimeenda Leo wananiambia nilipwe asilimia 33.3 ya mshahara wangu wa mwisho.
Alafu nitalipwa hyo hyo.mpaka miezi 6 iishe.alafu nitakaa miezi 18.ndo nikadai mafao yangu yote.
Kweli?
 
Mbona wengine wanapewa yote? Rafiki yangu juzi kachukua 25m cash bila usumbufu, haikuchukua zaidi ya miezi mitatu toka asimamishwe kazi, kwa nini kuwe na double standard?
 
Halafu watu wakitaka kuandamana kudai haki wanadaiwa ni wapinzani, chadema mara wamelipwa na mataifa ya nje. Kwa mtindo huu wa kulipwa 198k kati 7m kwa nini nisijilipue?

Kunahitajika mabadiliko makubwa NSSF.
 
Mimi hapa nilipitia huo msoto wa miezi 18 baada ya kulipwa 33.3% tarehe 17.06.2026 ndo niliweka fingerprint nikambiwa nisubiri ndani ya siku 30 za kazi....mpaka leo ni wiki 2 za kazi sijui watalipa kweli hawa wahuni maana kila kitu nil is haka mil is ha.
 
Mzee nssf ni utapeli wa waziwazi.
Mimi nimeenda Leo wananiambia nilipwe asilimia 33.3 ya mshahara wangu wa mwisho.
Alafu nitalipwa hyo hyo.mpaka miezi 6 iishe.alafu nitakaa miezi 18.ndo nikadai mafao yangu yote.
Kweli?
Hiyo 33.3% haikatwi kwenye michango yako hivyo ukipata kazi nyingine hapo kati basi utaanzia ulipoishia kuchangia.

Il miezi 18 ikipita na hujapata kazi nyingine basi ukienda kuchukua hela yako utakuta hiyo pesa ya miezi 6 wameikata na utachukua balance.

Lakini nakumbuka regulations mpya zinaruhusu kutoa hela yako yote na hiyo option ipo kwanini usiwaulize? Siku hizi wapo chap mimi nilienda siku moja tu baada ya wiki 2 hivi nikapokea hela yangu.
 
Hiyo uliyolipwa ni 33% ya mshahara wako wa mwisho. Utalipwa kila mwezi hicho kiasi kwa miezi 6 mfululizo. Katika hiko kipindi wana-assume unatafuta kazi nyingine.

Kama hutapata kazi baada ya miezi mitatu watakulipa yote iliyobaki. Kama unahitaji pesa yote fasta tumia shortcut
 
Hiyo 33.3% haikatwi kwenye michango yako hivyo ukipata kazi nyingine hapo kati basi utaanzia ulipoishia kuchangia.

Il miezi 18 ikipita na hujapata kazi nyingine basi ukienda kuchukua hela yako utakuta hiyo pesa ya miezi 6 wameikata na utachukua balance.

Lakini nakumbuka regulations mpya zinaruhusu kutoa hela yako yote na hiyo option ipo kwanini usiwaulize? Siku hizi wapo chap mimi nilienda siku moja tu baada ya wiki 2 hivi nikapokea hela yangu.
😀😀😀Acha kujichanganya.
Mimi nimeenda Leo.
Kwanza wanaangalia mshahara wako wa mwisho ni kiasi gani.alafu Wana calculate Kwa hyo 33.3%
Baada ya hapo ndo wanakupa hyo kutoka kwenye mafao yako.zingatia kutoka kwenye mafao yako.
Kwa muda wa miezi 6.
Ulitokea unataka Hela zako zilizobaki zote uchukue ndo unatakiwa ukae miezi 18.
Hyo 33.3 inatoka kwenye mafao yako ndugu
 
Sasa unachosema kina tofauti gani nilichosema? Ni kweli ukienda kutoa kiasi kilichobaki watakukata pesa uliyokwisha chukua

Ila USIPOENDA kuchukua iliyobaki kwa kupata kazi nyingine basi michango inaanzia ulipoishia kuchangia na pesa uliyochukua kwa miezi 6 haikatwi hata buku kwenye michango yako.
 
Back
Top Bottom