Kero yangu ni kwa watu wa NSSF, nilikuwa nafuatilia mafao yangu ya ukomo wa kazi kwenye statement yangu kuna shilingi 7,000,000 kazini nilikuwa nalipwa 600,000, hivyo NSSF nilikuwa nawekewa 120,000 sasa imefika wakati wa kufatilia nakuja kulipwa Shilingi 198,000.
Sasa hiyo hela mimi naifanyia nini kusema kweli, huu ni unyanyasaji eti watakuja kunilipa baada ya mwaka ikiwa sijapata kazi.
Sasa wanajua kesho yangu? Kwanini wanipangie masharti mimi nataka kufanya biashara zangu, kazi zenyewe ngumu kupata, halafu wanakuambia hela watakupa ukizeeka, jamani hawa vijana wote tuchanganyikiwe!