Natakiwa kumfukuza kazi muajiriwa aliekuwa kwenye kampuni kwa miaka 17, Nifanyeje?

Natakiwa kumfukuza kazi muajiriwa aliekuwa kwenye kampuni kwa miaka 17, Nifanyeje?

Dady Jr pole kwa majukumu mazito japo mepesi kitaaluma.
-Kwanza nasikitika sana kama Hr mwenzangu mwenye kutakiwa kufata misingi ya kazi, taratibu,sheria na kanuni za kazi na kutakiwa kusimama katikati ili kubalance pande zote za mwajiri na mwajiriwa kwa kutenda haki badala yake unataka kukengeuka kwa sababu mabosi hawamtaki mfanyakazi.
-pili, kama umesema kosa linasameheka, unashindwa nini kushauri bosi wako juu ya jambo hilo? Je kabla ya kutaka kumfukuza kazi kwa kosa lake, mmempa nafasi ya kujieleza mbele ya menejimenti au uhuni unataka kupewa nafasi ili kumwondoa mnyonge wa watu?
-HR ikumbuke kipimo upimiacho wenzio kama si kwa haki ndicho nawe siku moja utapimiwa zaidi. Binafsi nilishawahi kuacha kazi zaidi ya sehemu 2 kwa misingi ya kutokubaliana na wakurugenzi uchwara au mabosi kama waitwavyo kwa kutokubaliana nao kwa hoja zao.
-Nashauri simamia sheria kama Hr vinginevyo huyo mtumishi aliwahi kutenda kosa huko nyuma na hivyo hilo liwe ni kosa kubwa linaloendana na kumfukuza kazi kisheria na akiwa amepewa nafasi ya kujitetea.
Ndugu HR, endapo mtafukuza kazi pasipo haki,ieleweke kubwa mtamlipa pesa nyingi zaidi ya kile mnachokikwepa kwa sasa,hivyo ni hasara kwa kampuni na itaonekana pia umeigharimu kampuni kwa kushindwa kushauri vema kama Hr.
-Ndugu Hr, naomba mtakapomaliza mchakato wa kumfukuza, niunganishe naye ili mmlipe zaidi.
NB: nashauri huyo mtumishi asije akasauriwa kuresign- kuacha kazi mwenyewe kama mdau mmoja juu alivyoshauri maana itamsumbua pia kwenye mafao yake. Yeye akomae na kampuni ndio imwachishe kazi ili apewe barua ukomo au kufukuzwa kwa kazi ili awe salama zaidi kwa mambo mengine yajayo.
 
Back
Top Bottom