Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 12,826
- 17,371
Lini Zombe kafa?Aliyewatuma ni Bwana Zombe. alishatangulia Jehanam
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Lini Zombe kafa?Aliyewatuma ni Bwana Zombe. alishatangulia Jehanam
dah..una safari ndefu sana ya kujitoa kwenye utumwa wa kifikra...Rais Samia ni mwanamke,hawezi kusaini
Kama marais watatu wanaume, akiwemo rais jembe, rais shoka na rais chuma cha pua, Ben, JK na JPM, walishindwa kusaini, what are the chances mwanamke anyonge mtu?.dah..una safari ndefu sana ya kujitoa kwenye utumwa wa kifikra...
Busara elekezi 👆👆(Ameandika Malisa G. )
SSP Christopher Bageni atanyongwa hadi kufa. Ndivyo mahakama ya rufaa ilivyoamua. Maamuzi ya leo ni ya mwisho ktk mwenendo wa kesi yake. Hana pengine pa kukata rufaa, pa kukimbilia, wala pa kupinga. Mahakama imeamua anyongwe hadi afe. Jaji Stellah Mugasha amegonga nyundo. Itz over.
Hawezi kukata rufaa tena kwa sababu hukumu ya leo ni review ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo September 16, 2016, ambapo alihukumiwa kunyongwa hadi kufa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Benard Luanda. So hakuna mahakama ya kujadili tena shauri lake, labda Rais ampe msamaha.
Kwa wasiokumbuka Bageni alikua Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kinondoni. Mwaka 2006 yeye na wenzie wakiongozwa na aliyekua Kaimu RPC Dar, Abdalah Zombe, walituhumiwa kupanga njama za kuwauwa wafanyabiashara watatu wa Morogoro.
Zombe anadaiwa ndiye aliyeongoza wenzie kwenye mpango huo, baada ya kujulishwa kuwa wana madini na fedha kiasi cha shilingi milioni 200.
Walikamata gari waliyokua wameikodi. Wakamuongoza dereva hadi msitu wa Mabwepande. Wakapora madini pamoja na fedha zote walizokua nazo. Kisha wakawafunga vitambaa vyeusi usoni na pingu mikononi. Kisha wakawapiga risasi za kisogoni na kuwauwa wote akiwemo dereva wa taxi waliyemkodisha.
Kesho yake Zombe akaita media na kusema wameua majambazi yaliyokua yanarushiana risasi na Polisi. Rais Kikwete akaunda tume ya Jaji Kipenka kuchunguza. Ikabainika hawakuwa majambazi. Kilichouma zaidi walikua ndugu wa familia moja. Mama mmoja alipoteza wanae watatu. Watoto wa familia 4 wakapoteza baba zao, na wake wanne wakawa wajane kwa tamaa za polisi.
Zombe alifanikiwa "kuchomoka" kwenye kesi hii baada ya kusota rumande kwa miaka kadhaa. Lakini Bageni alipatikana na hatia akahukumiwa kunyongwa. Akakata rufaa ikafeli, akaomba review ya kesi, na rulling imesomwa leo kuwa ANYONGWE HADI KUFA.
Waliomtuma hawapo nae Segerea, wala hawatanyongwa pamoja nae. Atanyongwa peke yake. Wanaohangaika nae saivi angalau kumfariji ni familia yake. Zombe hayupo, OCD wake hayupo hata IGP wa wakati huo hayupo. Ni yeye mwenyewe, na atanyongwa mwenyewe.
Hii iwe fundisho kwa wote wanaotumwa kufanya maovu leo e.g kuteka, kuua na kupoteza watu. Ipo siku utajikuta peke yako. Anayekutuma hatakuwepo. Utasimama wewe mwenyewe kutoa hesabu ya maovu yako. Kama si hapa duniani basi hata mbinguni, lakini ipo siku utalipa. Kama ambavyo wema ni mbegu, na ubaya pia ni mbegu. Humea, hukomaa, na ni lazima UVUNE.!
Mkuu; Ukiwa kazini esp. Serikalini ni bora mara mia kuzingatia Taratibu za kazi kuliko kujikomba-komba au kujigeuza kuwa chawa wa mkubwa. Siku ikifika; huyo mkubwa unayedai eti ndiye alinituma anaruka futi 100. Kwani aliyewatuma ndo PGO hapo Ofisini?Ingependa na aliyewatuma akaunganishwa katika hiyo Kesi.
Kumuachia Huru Huyo Mkuu wao inafikirisha namna haki inavyotendeka.
Kuna kipindi zombe kama aliwehuka..sijui kama aliponaIngependa na aliyewatuma akaunganishwa katika hiyo Kesi.
Kumuachia Huru Huyo Mkuu wao inafikirisha namna haki inavyotendeka.
Michongo ndio hiyo, kama Ditopile. Ila mwisho wa dhulma huwa si mzuri.Zombe alitoka kwa michongo sidhani kama dini inaplay part hapa.
Unaposema rais samia ni mwanamke una maanisha nini?Naunga mkono hoja,hii adhabu ya kifo kwa mtu kunyongwa mpaka afe,ni moja ya adhabu za the colonial legacy ambazo ni very barbaric,ndio maana Nyerere alisaini death warrant 2,Mwinyi akasaini kadhaa,Mkapa,JK na JPM hawakusaini hata moja!,Rais Samia ni mwanamke,hawezi kusaini!,its high time adhabu hii ifutwe!,na hata ikilazimika kubaki,sio kuua kwa kunyonga,tunaweza kuua kwa lether injection,au kwa electric chair,mtu anakufa in a civilized manner na sio barbaric!。 Tumsusitize Rais Samia,aupokee ushauri huu Leo Tanzania Yaamriwa Kuifuta Adhabu ya Kifo kwa Kunyongwa Mpaka Kufa!. Ni Aibu Tanzania Mpaka Ilazimishwe!. Rais Samia, Futilia Mbali Unyama Huu!
p
Ninamaanisha kuna vitu wanaume wanaweza, wanawake hawawezi , kunyonga mtu rais mwanaume amaweza, rais mwanamke hawezi!.Unaposema rais samia ni mwanamke una maanisha nini?
Kwani yeye ndo anayenyonga?si mahakama ndo imeamua? Kwanini Sasa anapelekewa Tena kesi yeye?kuua wapinzani wanaweza Ila kuua wahalifu hawawezi?Ninamaanisha kuna vitu wanaume wanaweza, wanawake hawawezi , kunyonga mtu rais mwanaume amaweza, rais mwanamke hawezi!.
P
Safi kabisa. Mwisho wa dhuluma huwa sio mzuri. Utawahadaa na kuwaghilibu watu hapa duniani lakini itakapofika siku ya kuwepo mbele za haki ni lazima utakuwa na cha kusema. Ila kwa uhakika malipo huwa ni hapa hapa duniani.Michongo ndio hiyo, kama Ditopile. Ila mwisho wa dhulma huwa si mzuri.
Pesa HazikupatikanaHivi zile hela zilipatikana?