Natamani sana andiko hili la hukumu ya Afande Bageni lisomwe vituo vya Polisi na Makazi yao kwenye Paredi

Natamani sana andiko hili la hukumu ya Afande Bageni lisomwe vituo vya Polisi na Makazi yao kwenye Paredi

(Ameandika Malisa G. )
SSP Christopher Bageni atanyongwa hadi kufa. Ndivyo mahakama ya rufaa ilivyoamua. Maamuzi ya leo ni ya mwisho ktk mwenendo wa kesi yake. Hana pengine pa kukata rufaa, pa kukimbilia, wala pa kupinga. Mahakama imeamua anyongwe hadi afe. Jaji Stellah Mugasha amegonga nyundo. Itz over.

Hawezi kukata rufaa tena kwa sababu hukumu ya leo ni review ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo September 16, 2016, ambapo alihukumiwa kunyongwa hadi kufa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Benard Luanda. So hakuna mahakama ya kujadili tena shauri lake, labda Rais ampe msamaha.

Kwa wasiokumbuka Bageni alikua Mkuu wa Upelelezi wilaya ya Kinondoni. Mwaka 2006 yeye na wenzie wakiongozwa na aliyekua Kaimu RPC Dar, Abdalah Zombe, walituhumiwa kupanga njama za kuwauwa wafanyabiashara watatu wa Morogoro.

Zombe anadaiwa ndiye aliyeongoza wenzie kwenye mpango huo, baada ya kujulishwa kuwa wana madini na fedha kiasi cha shilingi milioni 200.

Walikamata gari waliyokua wameikodi. Wakamuongoza dereva hadi msitu wa Mabwepande. Wakapora madini pamoja na fedha zote walizokua nazo. Kisha wakawafunga vitambaa vyeusi usoni na pingu mikononi. Kisha wakawapiga risasi za kisogoni na kuwauwa wote akiwemo dereva wa taxi waliyemkodisha.

Kesho yake Zombe akaita media na kusema wameua majambazi yaliyokua yanarushiana risasi na Polisi. Rais Kikwete akaunda tume ya Jaji Kipenka kuchunguza. Ikabainika hawakuwa majambazi. Kilichouma zaidi walikua ndugu wa familia moja. Mama mmoja alipoteza wanae watatu. Watoto wa familia 4 wakapoteza baba zao, na wake wanne wakawa wajane kwa tamaa za polisi.

Zombe alifanikiwa "kuchomoka" kwenye kesi hii baada ya kusota rumande kwa miaka kadhaa. Lakini Bageni alipatikana na hatia akahukumiwa kunyongwa. Akakata rufaa ikafeli, akaomba review ya kesi, na rulling imesomwa leo kuwa ANYONGWE HADI KUFA.

Waliomtuma hawapo nae Segerea, wala hawatanyongwa pamoja nae. Atanyongwa peke yake. Wanaohangaika nae saivi angalau kumfariji ni familia yake. Zombe hayupo, OCD wake hayupo hata IGP wa wakati huo hayupo. Ni yeye mwenyewe, na atanyongwa mwenyewe.

Hii iwe fundisho kwa wote wanaotumwa kufanya maovu leo e.g kuteka, kuua na kupoteza watu. Ipo siku utajikuta peke yako. Anayekutuma hatakuwepo. Utasimama wewe mwenyewe kutoa hesabu ya maovu yako. Kama si hapa duniani basi hata mbinguni, lakini ipo siku utalipa. Kama ambavyo wema ni mbegu, na ubaya pia ni mbegu. Humea, hukomaa, na ni lazima UVUNE.!
Busara elekezi 👆👆
 
Ingependa na aliyewatuma akaunganishwa katika hiyo Kesi.

Kumuachia Huru Huyo Mkuu wao inafikirisha namna haki inavyotendeka.
Mkuu; Ukiwa kazini esp. Serikalini ni bora mara mia kuzingatia Taratibu za kazi kuliko kujikomba-komba au kujigeuza kuwa chawa wa mkubwa. Siku ikifika; huyo mkubwa unayedai eti ndiye alinituma anaruka futi 100. Kwani aliyewatuma ndo PGO hapo Ofisini?
 
Naunga mkono hoja,hii adhabu ya kifo kwa mtu kunyongwa mpaka afe,ni moja ya adhabu za the colonial legacy ambazo ni very barbaric,ndio maana Nyerere alisaini death warrant 2,Mwinyi akasaini kadhaa,Mkapa,JK na JPM hawakusaini hata moja!,Rais Samia ni mwanamke,hawezi kusaini!,its high time adhabu hii ifutwe!,na hata ikilazimika kubaki,sio kuua kwa kunyonga,tunaweza kuua kwa lether injection,au kwa electric chair,mtu anakufa in a civilized manner na sio barbaric!。 Tumsusitize Rais Samia,aupokee ushauri huu Leo Tanzania Yaamriwa Kuifuta Adhabu ya Kifo kwa Kunyongwa Mpaka Kufa!. Ni Aibu Tanzania Mpaka Ilazimishwe!. Rais Samia, Futilia Mbali Unyama Huu!
p
Unaposema rais samia ni mwanamke una maanisha nini?
 
Michongo ndio hiyo, kama Ditopile. Ila mwisho wa dhulma huwa si mzuri.
Safi kabisa. Mwisho wa dhuluma huwa sio mzuri. Utawahadaa na kuwaghilibu watu hapa duniani lakini itakapofika siku ya kuwepo mbele za haki ni lazima utakuwa na cha kusema. Ila kwa uhakika malipo huwa ni hapa hapa duniani.
 
Mwangwi wa sauti ya Wakabing'oko!

SSP Christopher Bageni, atanyongwa hadi kufa! Ndivyo Mahakama ya Rufaa ilivyoamua. Hakika uamuzi wa leo ni wa mwisho katika mwenendo wa kesi yake. Hana pengine pa kukata rufaa, pa kukimbilia wala pa kupinga, ni kweli Mahakama imeamua anyongwe hadi afe. Hivyo Jaji Stellah Mugasha amegonga nyundo. Its over! imeisha!!

Hawezi kukata rufani tena kwa sababu hukumu ya leo ni review, marejeo ya hukumu iliyotolewa na mahakama hiyo 16 Septemba 2016 ambapo alihukumiwa kunyongwa "hadi kufa" na jopo lile la majaji watatu wakiongozwa naye Jaji Benard Luanda. So hakuna mahakama ya 'kujadili' tena shauri hilo labda iwe kupitia msamaha wa Rais

1740064883457.jpg

Sasa kwao wasiokumbuka, Bageni alikua Mkuu wa Upelelezi, wilaya ya Kinondoni. Mwaka 2006 yeye, akiwa na wenzie, wakiongozwa na aliokua Kaimu RPC Dar Abdallah Zombe, walituhumiwa "kupanga njama" za kuwauwa wafanyabiashara watatu wa Morogoro. Sasa A. Zombe anadaiwa kuongoza wenziye kwenye 'mpango' huo baada ya kujulishwa kuwa wana madini na fedha kiasi cha shilingi milioni 200.

Hivyo 'wakaikamata' gari waliyokua wameikodi! Na kisha Wakamuongoza dereva hadi msitu wa Mabwepande. Kisha "wakapora" madini pamoja na fedha zote walizokuwa nazo. 'Wakawafunga' vitambaa vyeusi usoni, na hadi pingu mikononi. Wakapigwa risasi za 'kisogoni' na kuuawa wote akiwemo dereva wa taxi waliyemkodisha. Aise!!

Na kesho yake Zombe akaita media na kusema wameua majambazi, yaliyokua yanarushiana tu risasi na Polisi. Rais Kikwete akaunda 'tume' ya Jaji Kipenka kuchunguza jambo hilo. Ikabainika jamaa, hawakuwa Majambazi. Kilichouma zaidi walikua ndugu wa "familia moja". Mama mmoja alipoteza wanae watatu pia watoto wa familia 4 wakapoteza baba zao. Na wake wanne wakawa wajane kwa tamaa za watumishi wachache!

Zombe alifanikiwa 'Kuchomoka' kwenye kesi hii baada ya kusota "rumande" kwa miaka kadhaa!! Lakini Bageni 'alikutwa' na Hatia! Akahukumiwa kunyongwa. Akakata rufaa na akafeli. Akaomba review ya kesi sasa rulling imesomwa leo kuwa ANYONGWE HADI KUFA. Yani si kunyongwa tu!

Hakika waliomtuma hawapo nae Segerea. Wala hawatanyongwa pamoja nae. Atanyongwa peke yake. Na Wanaohangaika nae sasa hivi angalau kumfariji ni familia yake, A. Zombe hayupo OCD wake hayupo na hata IGP wa wakati ule hayupo pia. Ni yeye mwenyewe, na atanyongwa pekee!!

Hakika hii iwe fundisho kwa wote wanaotumwa kufanya maovu leo i.e kuteka kuua na kupoteza watu. Ipo siku utajikuta peke yako. Aliyekutuma hatakuwepo, basi utasimama mwenyewe kutoa hesabu, ya maovu yako. Kama sio hapa duniani basi hata kule mbinguni. Lakini ipo siku utalipa. Kama ambavyo, Wema ni Mbegu. Na Ubaya pia ni mbegu, humea hukomaa na ni lazima uvune! Usijitume wala Kutumwa kwa mabaya, Hukumu ya Mungu ni ya haki. Hakuna jasiri wa kudumu!!

Nchi yangu, Machozi yako, Nchi tamu ya uhuru!
 
Back
Top Bottom