Natamani sana Ndoa za dini ya Kiislamu " Its the best marriage Ever"

Nyenyere, Hizi unazozungumzia ni special case, tunazungumzia zile ndoa zilizofungwa kwa misingi ya upendo na sio tamaa tu za mwili ambapo pande zote zipo. Anachoongelea mtoa mada ni kuwa ukiona waislamu wamekaa na kudumu kwenye ndoa jua wanapendana tofauti na sisi unaweza kuona mtu ndani kunafukuta ila hana namna ya kutoka, kifupi kwenye ndoa za kikristo kuna vituko vingi sana....watu wanatutangazia wao ni mume na mke ila ndani wametengana vyumba, eti mume hali chakula kilichopikwa na mkewe hadi ale na watoto kwa hofu ya kuwekewa sumu, kama kungekuwa na talaka haya yasingekuwepo kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ndiyo point tuongeee yote ila ndoa za kikristo zi ashida sana ......mi ni mkristo ila navutiwa na ndoa za kiisilamu hakuna kuzenguana muda wowote ,

Kama mtu anaweza kukatwa kiungo ili kuopesha usalama wa mwili kwa nini kungangania mpk kufa ?

Kwani umezaliwa naye , ndoa nyingi zipo hoi maigizo ni mengi na ni pasua kichwa

Sent using i phone x
 
Tatizo sio ndoa za kikristo wala kiislamu, huko ni kukwepa msingi wa tatizo. Wengi wanaingia kwenye huo mtego kwa sababu tu hawakuzingatia misingi ya kuingia kwenye ndoa hivyo kujidanganya kuoa na kuacha ndio msimamo mzuri, huo si ukweli.

Ukijua ndoa ni nini utaingia kwa usahihi na utampata mtu sahihi na mataishi kwa furaha maisha yenu yote. Hizi habari za wakristo hawana furaha ni nyimbo za watu wenye tamaa lakini nawajua wakristu wengi tu wenye amani kwenye ndoa zao kama niwajuavyo waislamu wasio na amani kwenye ndoa zao.

Uzoefu wako na ubaki kwako mwenyewe, walio na masikio ya kusikiliza maonyo na maongozo wanaishi kwa amani tu kwenye ndoa zao bila kutii tamaa za mwili kutamani kila kitu.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Nenda visiwani kuna watu wana vyuo mpaka 6. Halafu ana miaka 25 tu..
Msichana akikuambia nina vyuo vitatu ujue kaolewa na kuachika mara 3.
Hiyo ndo raha ya uislam maana pamoja upumbavu wake au wa waumee zake angekuwa mkristo aangeendelea kuwa kwenye ndoa lakin uislam umempa fursa ya kuachwa na kuelowa na mwingine
 
Nyenyere, Nafahamu wapo wakristo wenye ndoa zao nzuri tu, lakini kuna wengine inatokea bahati mbaya wanakosea kuingia na watu ambao sio sahihi...tungepewa na sisi walau nafasi ya kurekebisha makosa [emoji14]....hata moja tu au mbili

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu umesema kweli 100/100. Ndoa za kikristo ni NDOANO. Watu tunakufa na tai zetu shingoni ndani ya ndoa. Huwezi kuamini jinsi wanawake wanavyoleta nyodo na ngebe kwa kuwa ndoa zao zina bima ya 'pingu za maisha'. Ushuzi mtupu[emoji32][emoji32][emoji32][emoji32][emoji777]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika. Wengine wamekubali ndoa tu kwa kuwa waliona umri unaenda na wamepoteza matumaini ya kuolewa. Lakini baada ya kuingia kwenye ndoa wamekuwa vichomi.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Very true.

Dini yangu ya kikristo ni nzuri sana Ila kuna mafundisho (theolojia) inalazimisha mambo wakati ni hiyari.

Kuoa na kuolewa ni hiyari kama ilivyo kutoa sadaka ni hiyari.

Ninachopigania ile uhiyari wa mtu kuingia katika ndoa na awe na uhiyari wa kutoka katika ndoa.

Kama nilivyosema hapo awali. Mimi nimeoa ndoa ya kikristo, huyu niliye naye ni part ya research yangu, baada ya kuona karibia wote wananfanana ndiyo nimekuja ku conclude kwamba kwenye ndoa hizi za dini hii na ile kuna tofauti kubwa.


Nisamehe kama nimekukwaza but that is true.
 
huo uchunguzi uliufanya wapi? we kama unataka kuoa kiislam nenda tu acha kutafuta justification, hujalazimishwa kukaa kwenye ndoa ya kikristo, badili dini, oa kiislam basi jipe furaha unayoitafuta
 
(Ndoa za kikristo zimebadirika sana na kupindukia. Sasa kuna ndoa za kikristo za mashoga, sasa kuna ndoa za kusagana, sasa kuna ndoa za mikataba). Hizi zipo kwenye biblia gani?
 
Du hiki ni "kifungo cha nje". Yaani hata mtu usichepuko hata mkeo akiwa na mimba? Ut@t0mB@ wapi?[emoji32][emoji32][emoji32]
Sent using Jamii Forums mobile app
 
huo uchunguzi uliufanya wapi? we kama unataka kuoa kiislam nenda tu acha kutafuta justification, hujalazimishwa kukaa kwenye ndoa ya kikristo, badili dini, oa kiislam basi jipe furaha unayoitafuta

Ok.

kuna ndoa za mashoga na mikataba na za jinsia moja katika ukristo huu huu ni kwa kitabu gani? ni hii hii biblia au kitabu kingine?.

Hii inaonesha kwamba waalimu wetu wa biblia kuna kitu hawaweki sawa katika mafundisho ya ndoa.
 
Ndio maana huwa nawashangaa sana vijana wadogo wanaotaka kuoa mapema. Kwanini wanataka kujitumbukiza kwenye matatizo ktk umri mdogo?[emoji32][emoji32][emoji32][emoji32][emoji22][emoji22]
Nafikiri kuna watu wengi hawaelewi maana ya kuoa wake wengi humu na Google hawaitendei haki
Kama hujaelewa kitu ni bora kuuliza tu na kuuliza sio ujinga bali ni kuongeza maarifa tu
Google please


Sent from my iPhone using Tapatalk

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ahsante mkuu na ww nakupa tano kwa ufafanuzi mzuri ndo maana mm sidharau imani ya mwenzangu najua kua Anamafundisho yake tatizo tunatoka nje ya mafundisho kisha tunatafuta mchawi .Maana kosa la Muumini hali haribu Uzuri wa dini .Imam au Padri akizini haimaanishi kua dini zimeruhusu zinaa
 
Hiyo Dini ya kuruhusu kuoa na kuachana ni Dini ya hovyo sana

Si ni bora hiyo ndoa isifungishwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Umeongea vizuri kabisa nakubaliana nawewe

Swali langu kwako upo teyari kuolewa na kufukuzwa mara ngapi katika maisha yako?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…