Natamani sana Ndoa za dini ya Kiislamu " Its the best marriage Ever"

Hiyo namba moja nakubaliana na wewe kwa asilimia zote, wazazi wanapofikiria kuachana kwa ufupi wanakuwa wamejifikiria wao wenyewe tu...ni ubinafsi
Namba mbili, kwa hiyo unakubaliana kuwa mwanamke akishaota makunyanzi, matiti kulala anakuwa hafai tena? Basi huna tofauti na wao, tofauti yenu ni kwamba yeye anatoa talaka ila wewe hutatoa bali utamwacha mkeo ndani unaenda nje kutafuta dogodogo...na ndicho wanaume wengi mnachofanya, mnajifanya mna ndoa ya mke mmoja ambayo ni ya maisha yote ila vituko mnavyowafanyia wake zenu havielezeki. Watu mnabaki mnaishi ndani hamsalimiani hayo mahitaji ya ngono anawatimizia nani? Si bado mnatafuta vi slay queen na vimarioo kwaajili ya kukidhi haja zenu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Mwanamke/mwanaume mliechokeshana nikitu kimoja. Mnahistoria....mnaelewana kwa mambo mengi sana


Ukisha nunua suruali mpya au gauni jipya

Hata vinapofubaa ni vyako unaendelea kuvaa tena ukijivuna gauni langu lilikuwa zuri sana likiwa jipya nalipenda sana japo limechakaa lakini nalipenda lipo ndani ya roho yangu.

Lakini huwezi kujivunia suruali aliyoivaa mwenzio muda mrefu na kuitia vilaka kibao nayo imefubaa.....utaanazaje?
 
Hiyo Dini ya kuruhusu kuoa na kuachana ni Dini ya hovyo sana

Si ni bora hiyo ndoa isifungishwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na dini Ambayo ukioa ni kama roho haitoki mpaka ufe ni ya Ajabu sana wakati inajua binaadamu tunamapungufu inafika wakati unashindwa kuvumilia mateso anayokupa mwenzio eti kwa kisingizio cha ndoa . Ndoa na kiungo chama mwili wako bora nn ? Watu hutia saini kabisa kiungo kikatwe kunusuru Maisha .Au Yale Magunia ya mkaa Ndio njia sahihi ya matatizo yanapokua hayana suluhu tena
 
Hehehe, kwenye magauni tena loh....hata hivyo unachokisema kingekuwa kinafanyika hivyo ingekuwa raha sana na wala sie wengine tusingekuwa tunatamani Mungu abadilishe sheria zake...yanayofanyika yanatisha ndio maana tuko kwenye maombi Bwana Yesu atengue ile kauli yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio hapo sasa ndugu yangu, mweh

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndio hapo sasa ndugu yangu, Nisamehe sana nimetumia maneno makali kidogo ila ibaki kila mtu afate imani yake haina haja ya kubezana ukiona imani hiyo haikufai Si watu wanabadili dini Ije iwe Ndoa tu.
 
Funga ndoa ya mkataba wa miaka mitatu mitatu au miwili miwli kwa Wakili yeyote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu wetu sio Mungu wa uharibifu. Unapomlala mwanamke ukamtoa bikra kisha ukamwacha basi umemweka mashakani. Ana uwezekano mkubwa wa kuishia kutangatanga, ndio maana siki hizi wanawake wameasi ndoa na kugeuka watafutaji. Hii ni kwa sababu wanaume wameasi majukumunyao na kukimbilia kujistarehesha tu.

Mungu habadiliki, ukipanda uharibifu utavuna huo. Ukifuata maagizo yake utaishi, la usipofuata utakufa hakika

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
 
Amen

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Boss kiukweli ni kwamba uislam ni dini imejitosheleza haina walakini wala kasoro yyt ila kuna conspiracy iliyo enezwa ulimwenguni ya kuonesha kwamba uislam ni dini ya ma terorist ,dini ya unyanyasaji ila kiukweli hamna kitu kama hicho katika uislam ujuwe kwamba hata uislam wenyew unatufunza kuwaheshimu wanawake,,kuwatunza na tusiwanyanyase kwa namna moja ama nyingine,,soo unapoongelea swala nzima la ndoa ndoa sisi kwetu ni ibada na imewekewa misingi itakayo fatwa ili iendeshwe vizuri itakapo vunjwa basi ujuwe kwamba na ndoa pia itavunjwa hamna mambo ya kulazimishana katika dini hutaki kuishi na mwenzio basi !!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu nikushauri yafuatayo.
1. ukristo hujabanwa unaweza badili ukaenda huko kuzuri.
2. Wewe sio mkristo lakini ni mtu wa dini, hujui hata ukristo ni nini. Ukristo huwezi ingia jambo lolote kwa majaribio, iwe ndoa, iwe huduma au wito wowote. hivi vitu havijaribiwi katika ukristo.
mkristo ukitaka kuoa sio swala la kupenda tu ni swala la Mungu kuridhia hio ndoa maana sio majaribio. Ndoa ya kikristo ni ndoa bora kuliko zote duniani kwa sababu inakufanya usiingie ndoa kichwa kichwa lakini umtegemee Mungu katika jambo hilo.

Hausomi hata maandiko maana hata hio biblia unasema inabadirishwa, hii sijawahi kuona popote na haijawahi kutokea biblia ikabadirishwa, hakuna hata neno moja linaweza kuondolewa katika biblia.

Nimeoa ndoa nzuri ya kikristo naifurahia sana, nilimuomba Mungu karibia kwa mwaka mzima, Mungu alipomleta huyu mtu ukweli sijawahi kujuta, anakosea sana lakini bado ni mwanamke bora sana kwangu.

Ndoa yako imekushinda unatafta kichaka, ulikimbilia ndoa ukidhani kazi ya ndoa ni kutiana tu, hujui maana ya ndoa.
 
Kingine umesahau ni kuwa pia ndoa za kiislamu ni very simple ukiamua kufanya mbwembwe ni wewe tu unaweza kuelekezwa nyumba ukaoe kama binti umemridhia na tabia zake ni njema na ww zako ni njema ukaoa siku hiyo hiyo hizo mbwembwe na ukumbini ni utashi wako tu.
 
Cheki huyu jamaa madhaifu yake katika ndoa yake ndo anafanya generalization ndo zote za kiislamu na za kikristo zinachangamoto zake pia mkuu kama haujui mgawanyo wa mali au mirathi kwenye ukristo jielimishe mzee...
 
Cheki huyu jamaa madhaifu yake katika ndoa yake ndo anafanya generalization ndo zote za kiislamu na za kikristo zinachangamoto zake pia mkuu kama haujui mgawanyo wa mali au mirathi kwenye ukristo jielimishe mzee...
pure bogus kabisa
 

Tumefundishwa kuwa ndoa yenye baraka zaidi ni ile isiyokuwa na gharama nyingi Mkuu


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Katika Ndoa za kiislam kipengele kina sema hivi ikibidi kuachana muachane kwa wema kwa maana imefika mahala suruhu imeshindikana zimeitwa pande zote mbili za wazazi imeshindikana hapo ndio talaka inatoka na ikitoka taraka mwanamke anakuwa chini ya imaya yako kwa kutoa huduma ndani ya miezi mitatu sasa kama wote mlikuwa na hasira na mmechukiana katika kipindi chote hicho hizo ni hasira za juu kabisa mpaka kushindwa kusameheana na kuachana si ugomvi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…