masozist
JF-Expert Member
- Nov 19, 2019
- 352
- 316
Na jingine tuache kudanganyana kuwa mwanaume atakuwa na mkewe mmoja peke yake wanaume tulivyo umbwa ni kutamani tu na ndio maana mwenyezi mungu alie tuumba anatujuaUmesema kweli, KWENYE UISLAM. Lakini ndoa haina maana hiyo uliyoitoa, ndio maana huko ndoa imepoteza maana yake. Hoja ya msingi hapa tujiulize, kwa nini leo hii divvorce rates imekuwa kubwa kuliko zamani? Nini kimebadilika?
Ukipata jibu la hilo swali utajua mzizi wa tatizo. Mimi ni mkristo, namshukuru Mungu kwa sababu ya ndoa yangu. Napitia changamoto za kawaida tu ambazo hazijalishi kama ni mwislamu ama mkristo, kwa kiasi kikubwa Mungu ameniepusha na majaribu yanayoshinda uwezo wa mwanadamu kuvumilia.
Sasa nikikuambia, habari ya talaka ni mfumo wa mwanamume kumuumiza mwanamke na pia ni roho ya ubinafsi. Ni ngumu kunielewa hapa hata kwa wanawake kwa sababu ya fikra tulizopandikizwa, lakini ni ukweli mweupe kabisa kiwa thamani ya mwanamke hupanda mbele ya jamii pale anapoolewa na hushuka maradufu pale anapoachika.
Mwanamke akiachwa hutazamwa kama bidhaa isiyo na thamani na huongelewa negatively na wanaume walio wengi. Wako wanawake ambao baada ya kuachia walipata ndoa nyingine stable, lakini wengi wao waliishia kuwa wadangaji ama washirika wa waganga wa jadi. Sababu kubwa ni kuwa mwanamke hakuumbwa kuolewa na kuachwa hovyo, kwani thamani yake inaambatana na yule mtu wake wa kwanza, aliyeutoa usichana wake na kumwingiza kwenye daraja ya mwanamke.
Ukitaka kuhibitisha hili jiulize ni wanaume wangapi waliofanikiwa kimaisha watakwenda kuoa mwanamke mwenye ndoa 3, ama ni vijana wangapi ambao wana malengo kimaisha (wasiopumbazwa na maumbo ya kisasa) wataacha kujitwalia mabinti wabichi wakaoe watalaka.
Ndoa za wake wengi ni namna ya KUJIBU TAMAA YA KINGONO YA MWANAMUME kwa kigezo za kumsaidia mwanamke. Watu wamehalalisha uzinzi kwa kujipachika jukumu la kuwasaidia wanawake ingawa mpaka leo hakuna ndoa yenye furaha kwa sababu tu mume ana wake wengi. Huku ni kudanganyana na sio ukweli halisi.
Furaha ya kweli ni ipi? Je,
1. Ni kuoa wanawake wengi?
2. Kuwa na uwezo wa kutoa talaka wakati wowote?
Nasubiri majibu
Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Sent using Jamii Forums mobile app