Natamani urudi hata kwa dakika tano mke wangu

Natamani urudi hata kwa dakika tano mke wangu

Labda umletee ukimwi afe, ila kuna option mme akikushinda kisa umalaya wake usidubiri kufa kwa stress ondoka utapata akupendae
Sio wote wanaweza kuchukua maamuzi hayo. Wanakomaa hadi wanafia humo humo.
 
Naomba iwe tungo tu isiwe ni halisia, maana imeleta hisia za kuumiza zaidi na kutafakarisha sana

Lakini hata kama ilikua ni kisa cha kweli, pamoja na kua maisha yetu kuja na kuondoka sio kwa kutaka kwetu bali aliye juu yetu.

Lakini huyo mama atakua amekosea mno kwa sababu ya hao watoto, mume ni bora lakini watoto ni bora zaidi kwa sababu wanamhitajia mno, yeye atakua labda ameona heri apumzike, lakini pumziko lake halitakuwa pumziko jema kwa sababu ya maumivu na mahangaiko wanayopitia wale watoto.

Kuna namna mtu anatoka duniani kila mtu anasema heri akapumzike, hapo kweli utapumzika kwa amani.

Lakini kwa hii situation ya huyu mama pumziko lake halitakuwa la amani.
Yawezekana alikuwa anasumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu, mpaka mola akamchukua.
 
Naumia si kwasababu Mungu amekuchukua bali ni kwakua sikupata kuwa mume wako katika kipindi chote cha miaka sita ya ndoa yetu. Bado nakumbuka meseji yako ya mwisho uliyonitumia uliniambia “Mume wangu njoo tu nyumbani, samahani kwa kukusumbua lakini nataka tu nikuone sijisikii vizuri!”

Niliisoma na ulipoona siijibu ulipiga simu, natamani hata ningepokea mimi na kusikia sauti yako kwa mara ya mwisho lakini nilimpa mwanamke mwingine akapokea.

Sijui kama ulijua lakini ulimuambia aniambie kwa heri. Nikijua ni vile vitisho vyako vya kila siku kuwa utaondoka nilipuuza na kuamua kulala huko huko mpaka saa sita usiku rafiki yangu mmoja alipokuja kunigongea usiku.

Nilizima simu na hakuna mtu aliyekua akijua nilipokua kasoro yeye hivyo alitafutwa na kuja kunipa taraifa, alikuja na kugonga kisha kuniambia tuondoke, hata hakunionea huruma aliniambia kuwa “Mke wako hayuko tena, amefariki!”

Niliishiwa nguvu sijui nini cha kufanya, nilirudi nyumbani na kuwakuta wenetu wadogo wakilia hawajui wanalia nini lakini walilia kwakua wanaona watu wengine wanalia.

Waliniona badala ya kunikumbatia walikua wananikwepa, walikua wanaogopa kwakua Mama yao hayupo tena. Mimi ni kama mgeni kwao, hawanijui na mimi siwajui. Mke wangu baada ya mazishi watu wote wameondoka.

Nimebaki mimi nawatoto tu, ndugu zangu wote wamerudi kuendelea na familia zao, michepuko yangu nayo hata hainitafuti tena, wale wanawake wote waliokua wanakupigia simu kukutukana hawanipigii tena simu.

Binti wa kazi uliyemuacha ameondoka siku mbili tu baada ya mazishi. Nakumbuka mara ya mwisho niliyokupiga nilikuambia kama umechoka ondoka uniachie wanangu.

Naona umechoka kweli umeondoka na kuniachia wanangu lakini sasa sijui hata niwapeleke wapi? Kila siku wanamuulizia mama, naumia zaidi kwani mimi wananiogopa, wananiangalia kama shetani wananiona kama natisha, hii ni kwasababu sikuwahi kuwa Baba yao, siku zote nilikua bize na starehe.

Nakukumbuka sana mke wangu ni miezi miwili tu tangu uondoke lakini naona kama miaka mia, kweli nilikukosea natamani hata urudi kwa dakika tano tu ili niwe mume wako nikuonyeshe namna ninavyojutia.

🤣🤣🤣🤣
 
Kama ni kisa cha kweli inasikitisha sana tubu dhambi zako Mungu wetu ni Mungu wa rehema na ni mwepesi wa kusamehe.
 
Wanawake wana vitimbi sana, ila kama umeshaamua awe mkeo mpe heshma, asitokee kenge yoyote akamvunjia heshma wewe ukiona na ukavumilia, mpende na haswaa penda familia yako, hao wanaokupa joto leo wapo kwa sababu tu na siku sababu hizo zikitoweka utaaibika
 
Na hayo ndio maisha ya wanandoa wengi, wanaume wengi huwachukulia wake zao for granted sana.
Kuna boya nae last month mkewe kaondoka ghafla kwa ajali, analia tu hata hajui pa kuanzia wakati mkewe alivyokuwa hai alimnyanyasa mnooo na michepuko isoisha.
Ndiyo aoe sasa hiyo michepuko Kapata nafasi
 
Uzuri anaendelea kukua hivyo ipo siku atayaonja japo simwombei yamkute!
Kwa hawa hawa wanaume wa kibongo atayakuta tu, akikwepa hili tego basi itakuwa ni bahati yake
 
Back
Top Bottom