Kinengunengu
JF-Expert Member
- May 3, 2021
- 1,716
- 4,375
Hahaaaaaa, nimecheka sana kwa kweliSasa mbona kama unaniambia mimi kijana wakati muhusika mwenye uzi unamuacha
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hahaaaaaa, nimecheka sana kwa kweliSasa mbona kama unaniambia mimi kijana wakati muhusika mwenye uzi unamuacha
Kwa uzoefu wangu kwenye haya mambo, kama kweli ulichondika ndivyo kilivyo, kaka hauna maisha marefu, lazima na wewe ufe soon, yaani haina kukwepa hiyo!Naumia si kwasababu Mungu amekuchukua bali ni kwakua sikupata kuwa mume wako katika kipindi chote cha miaka sita ya ndoa yetu. Bado nakumbuka meseji yako ya mwisho uliyonitumia uliniambia “Mume wangu njoo tu nyumbani, samahani kwa kukusumbua lakini nataka tu nikuone sijisikii vizuri!”
Niliisoma na ulipoona siijibu ulipiga simu, natamani hata ningepokea mimi na kusikia sauti yako kwa mara ya mwisho lakini nilimpa mwanamke mwingine akapokea.
Sijui kama ulijua lakini ulimuambia aniambie kwa heri. Nikijua ni vile vitisho vyako vya kila siku kuwa utaondoka nilipuuza na kuamua kulala huko huko mpaka saa sita usiku rafiki yangu mmoja alipokuja kunigongea usiku.
Nilizima simu na hakuna mtu aliyekua akijua nilipokua kasoro yeye hivyo alitafutwa na kuja kunipa taraifa, alikuja na kugonga kisha kuniambia tuondoke, hata hakunionea huruma aliniambia kuwa “Mke wako hayuko tena, amefariki!”
Niliishiwa nguvu sijui nini cha kufanya, nilirudi nyumbani na kuwakuta wenetu wadogo wakilia hawajui wanalia nini lakini walilia kwakua wanaona watu wengine wanalia.
Waliniona badala ya kunikumbatia walikua wananikwepa, walikua wanaogopa kwakua Mama yao hayupo tena. Mimi ni kama mgeni kwao, hawanijui na mimi siwajui. Mke wangu baada ya mazishi watu wote wameondoka.
Nimebaki mimi nawatoto tu, ndugu zangu wote wamerudi kuendelea na familia zao, michepuko yangu nayo hata hainitafuti tena, wale wanawake wote waliokua wanakupigia simu kukutukana hawanipigii tena simu.
Binti wa kazi uliyemuacha ameondoka siku mbili tu baada ya mazishi. Nakumbuka mara ya mwisho niliyokupiga nilikuambia kama umechoka ondoka uniachie wanangu.
Naona umechoka kweli umeondoka na kuniachia wanangu lakini sasa sijui hata niwapeleke wapi? Kila siku wanamuulizia mama, naumia zaidi kwani mimi wananiogopa, wananiangalia kama shetani wananiona kama natisha, hii ni kwasababu sikuwahi kuwa Baba yao, siku zote nilikua bize na starehe.
Nakukumbuka sana mke wangu ni miezi miwili tu tangu uondoke lakini naona kama miaka mia, kweli nilikukosea natamani hata urudi kwa dakika tano tu ili niwe mume wako nikuonyeshe namna ninavyojutia.
Kwa kimombo ndo kusema machozi shot on target.Machozi yamenilenga [emoji3064]
Haaa haa leo umeenda ibada kweli?kwa kimombo ndo kusema machozi shot on target.
Wengi Wataona kama hadithi ila ndivyo ililivyo, unakuta mke hana shida yeyote mme kimeo hatari, mpaka unajiuliza huyu mwanamke alikutana wapi na hili bazazi!Kwa uzoefu wangu kwenye haya mambo, kama kweli ulichondika ndivyo kilivyo, kaka hauna maisha marefu, lazima na wewe ufe soon, yaani haina kukwepa hiyo!
Kuna jamaa mmoja tuliwahi kuishi naye nyumba moja maeneo fulani Iringa, alikuwa mhasibu kwenye kampuni moja ya kitalii, alikuwa anaishi na mkewe na mtoto mmoja, jamaa alipata mwanamke mmoja mzuri sana, alikuwa na umbo matata mpaka kila mtu alimsifia, jamaa akaanza kumtamkia mkewe maneno makali sana hata mbele za watu...
Kuna wakati jamaa aliacha kurudi home kabisa, mke (asiye na kazi) akawa anajihangaisha kulea peke yake, jamaa akipigiwa simu hapokei wala hajali chochote!
Usiku mmoja mke wa jamaa akatugongea,akasema anajisikia homa kali sana anaomba tumpigie jamaa simu aje ampeleke hospital, tukapiga simu sanaaa jamaa hakupokea!
Tukamkimbiza mke wa jamaa hospital, asubuhi yake nikamfuata jamaa kazini kwake kumfahamisha habari ya mkewe kulazwa, mbele za watu akaniambia "bro, kwani wewe hauna kazi za kufanya mpaka utumwe kunifuata fuata kazini?" Daah nilijisikia hasira sana nikataka kumtwanga ngumi mle ndani, nikatolewa na walinzi pale....
Siku hiyo hata hospital kwenda kumuona mgonjwa sikwenda, usiku wa saa tatu (siku hiyo hiyo niliyojibiwa vibaya na mshakaji) napokea taarifa mke wa jamaa amefariki...
Mwili umeletwa home jamaa kumbe yupo kwa huyo mwanamke wake wanakula maisha, akapelekewa taarifa manually kuwa mkewe amefariki, (maana alikuwa akiona simu za watu wa pale home hapokei)
Jamaa akaja usiku wa kama saa tisa hivi, anaanza kulia watu wote wanamcheki tu, jamaa sauti yake tu ndo inasikika! shughuli za msiba zimefanyika mpaka mazishi jamaa hakuna anayeenda kumpa pole...(kwa wanaomfahamu labda wageni wageni tu)
Mtoto wa jamaa alikuwa na miaka kama 4 hivi, dada wa marehemu akaondoka naye!
Jamaa wiki tatu tu baada ya mazishi akamleta yule mchepuko wake pale pale home, alitoa baadhi ya fenicha zilizokuwa mle ndani (sofa) akaleta zingine akaendelea kuishi hapo na mchepuko!
Baada ya miezi minne tu, mshkaji akaugua ugonjwa usioeleweka, jamaa akawa anajikojolea tu, na network ikawa kama inakata hivi kwa brain yake, yule mchepuko alivyoona hali inakuwa mbaya akamshawishi jamaa wauze gari, ikauzwa!jamaa alikuwa na viwanja 2 Donbosco wakauza, (kimoja nikanunua mimi maana bei zilikuwa sawa na bure) na mchepuko ndo alikuwa anapanga bei!
Siku moja tunamsikia jamaa kama anakoroma hivi, kwenda kugonga kumbe mshkaji ana siku 4 hajala chochote bibie alishaondoka sisi hatujui...
Tukamkimbiza hospital haikuchukua muda jamaa akafariki pia! Wanaume tunajisahau sana wakati mwingine, jamaa tukampoteza namna hiyo yaani
Vipi na mke akiwa na shida mkuu anasaidiwa je mwanaumeWengi Wataona kama hadithi ila ndivyo ililivyo, unakuta mke hana shida yeyote mme kimeo hatari, mpaka unajiuliza huyu mwanamke alikutana wapi na hili bazazi!
Za Ulaya zimestaarabika??
Sio wote wanaweza kuchukua maamuzi hayo. Wanakomaa hadi wanafia humo humo.
Sio wote wanaweza kuchukua maamuzi hayo. Wanakomaa hadi wanafia humo humo.
Hii ni dhahiri kabisa, R.I.P baba Prince, Wilolesi-Iringa mjini...Wengi Wataona kama hadithi ila ndivyo ililivyo, unakuta mke hana shida yeyote mme kimeo hatari, mpaka unajiuliza huyu mwanamke alikutana wapi na hili bazazi!
Kweli kabisa.Huko wala sio kukomaa ni sababu ya ujinga!
Elimu ya mahusiano inahitajika sana ili kunusuru maisha ya watu yatokanayo na kutendwa na wenzi wao.
MmmHii ni dhahiri kabisa, R.I.P baba Prince, Wilolesi-Iringa mjini...
[emoji23][emoji23][emoji23] umenichekesha..hata wazungu wanazinguaNdoa za kibongo ni upumbavu uliotukuka.
Cc😡Liverpool VPN
Ila yapo kwenye jamii zetu.Tungo nzuri
Mwanaume na ...mbu zako zote 2, unampa simu mchepuko amjibu mkeo!! Hustahili kuitwa mume.Kama hii story ni yako Na Ni kweli Wewe Ni kenge Kwenda zako Na huna maana dunian!
Huyu mama ninafikiri alikuwa mgonjwa. Text yake kwa mumewe ilisema naomba urudi nyumbani maana najisikia vibaya. Baada ya text kutojibiwa aliamua kupiga.Wewe unajua chanzo cha kifo cha huyo Mke?
Hii tungo haijaelezea chanzo cha kifo.