Natamani urudi hata kwa dakika tano mke wangu

Kwa uzoefu wangu kwenye haya mambo, kama kweli ulichondika ndivyo kilivyo, kaka hauna maisha marefu, lazima na wewe ufe soon, yaani haina kukwepa hiyo!

Kuna jamaa mmoja tuliwahi kuishi naye nyumba moja maeneo fulani Iringa, alikuwa mhasibu kwenye kampuni moja ya kitalii, alikuwa anaishi na mkewe na mtoto mmoja, jamaa alipata mwanamke mmoja mzuri sana, alikuwa na umbo matata mpaka kila mtu alimsifia, jamaa akaanza kumtamkia mkewe maneno makali sana hata mbele za watu...

Kuna wakati jamaa aliacha kurudi home kabisa, mke (asiye na kazi) akawa anajihangaisha kulea peke yake, jamaa akipigiwa simu hapokei wala hajali chochote!

Usiku mmoja mke wa jamaa akatugongea,akasema anajisikia homa kali sana anaomba tumpigie jamaa simu aje ampeleke hospital, tukapiga simu sanaaa jamaa hakupokea!

Tukamkimbiza mke wa jamaa hospital, asubuhi yake nikamfuata jamaa kazini kwake kumfahamisha habari ya mkewe kulazwa, mbele za watu akaniambia "bro, kwani wewe hauna kazi za kufanya mpaka utumwe kunifuata fuata kazini?" Daah nilijisikia hasira sana nikataka kumtwanga ngumi mle ndani, nikatolewa na walinzi pale....

Siku hiyo hata hospital kwenda kumuona mgonjwa sikwenda, usiku wa saa tatu (siku hiyo hiyo niliyojibiwa vibaya na mshakaji) napokea taarifa mke wa jamaa amefariki...

Mwili umeletwa home jamaa kumbe yupo kwa huyo mwanamke wake wanakula maisha, akapelekewa taarifa manually kuwa mkewe amefariki, (maana alikuwa akiona simu za watu wa pale home hapokei)

Jamaa akaja usiku wa kama saa tisa hivi, anaanza kulia watu wote wanamcheki tu, jamaa sauti yake tu ndo inasikika! shughuli za msiba zimefanyika mpaka mazishi jamaa hakuna anayeenda kumpa pole...(kwa wanaomfahamu labda wageni wageni tu)

Mtoto wa jamaa alikuwa na miaka kama 4 hivi, dada wa marehemu akaondoka naye!
Jamaa wiki tatu tu baada ya mazishi akamleta yule mchepuko wake pale pale home, alitoa baadhi ya fenicha zilizokuwa mle ndani (sofa) akaleta zingine akaendelea kuishi hapo na mchepuko!

Baada ya miezi minne tu, mshkaji akaugua ugonjwa usioeleweka, jamaa akawa anajikojolea tu, na network ikawa kama inakata hivi kwa brain yake, yule mchepuko alivyoona hali inakuwa mbaya akamshawishi jamaa wauze gari, ikauzwa!jamaa alikuwa na viwanja 2 Donbosco wakauza, (kimoja nikanunua mimi maana bei zilikuwa sawa na bure) na mchepuko ndo alikuwa anapanga bei!

Siku moja tunamsikia jamaa kama anakoroma hivi, kwenda kugonga kumbe mshkaji ana siku 4 hajala chochote bibie alishaondoka sisi hatujui...

Tukamkimbiza hospital haikuchukua muda jamaa akafariki pia! Wanaume tunajisahau sana wakati mwingine, jamaa tukampoteza namna hiyo yaani
 
Wengi Wataona kama hadithi ila ndivyo ililivyo, unakuta mke hana shida yeyote mme kimeo hatari, mpaka unajiuliza huyu mwanamke alikutana wapi na hili bazazi!
 
Wengi Wataona kama hadithi ila ndivyo ililivyo, unakuta mke hana shida yeyote mme kimeo hatari, mpaka unajiuliza huyu mwanamke alikutana wapi na hili bazazi!
Vipi na mke akiwa na shida mkuu anasaidiwa je mwanaume
 
Sio wote wanaweza kuchukua maamuzi hayo. Wanakomaa hadi wanafia humo humo.


Huko wala sio kukomaa ni sababu ya ujinga!

Elimu ya mahusiano inahitajika sana ili kunusuru maisha ya watu yatokanayo na kutendwa na wenzi wao.
 
Wengi Wataona kama hadithi ila ndivyo ililivyo, unakuta mke hana shida yeyote mme kimeo hatari, mpaka unajiuliza huyu mwanamke alikutana wapi na hili bazazi!
Hii ni dhahiri kabisa, R.I.P baba Prince, Wilolesi-Iringa mjini...
 
Ni story nzuri, ingekua poa kama ungeshea nasi ni wapi umeikopi ili tupate visa vingi ama lah uwe unashea nasi kila kitachopostiwa huko.
 
Kama hii story ni yako Na Ni kweli Wewe Ni kenge Kwenda zako Na huna maana dunian!
Mwanaume na ...mbu zako zote 2, unampa simu mchepuko amjibu mkeo!! Hustahili kuitwa mume.

Mwanaume hata mkeo awe kero kiasi gani, gombana naye kiasi chochote, lakini usiruhusu ndugu au mchepuko kukusaidia kumdharau mkeo. Kama ni ndugu wakusaidie kushauri tu lakini siyo kumdharau hata kidogo.

Wanaume tujifunze katika hili hata kama ni la kughani.
 
Wewe unajua chanzo cha kifo cha huyo Mke?

Hii tungo haijaelezea chanzo cha kifo.
Huyu mama ninafikiri alikuwa mgonjwa. Text yake kwa mumewe ilisema naomba urudi nyumbani maana najisikia vibaya. Baada ya text kutojibiwa aliamua kupiga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…