Natamani viongozi wote wa mataifa ya Afrika waiunge mkono kauli ya Nana Akufo Ado

Natamani viongozi wote wa mataifa ya Afrika waiunge mkono kauli ya Nana Akufo Ado

Mi nadhani lengo sio kutajirika,kikubwa hapo ni kurejesha fidia ya uharibifu na wizi walioufanya. Haiwezi kulipia machungu na maumivu waliuopitia waafrika ila ni inasaidia kuwajulisha watesi wetu kuwa walichokifanya hakikuwa sawa.
Kwa Afrika hii ni kuongeza tu listi ya mafisadi haitawasaidia wananchi.
 
Kabisa,yaani maisha yananipelekesha,nafanya kazi kwa bidii kutafuta mtaji lakini wapi,kwasababu dependants ni wengi na suwezi nikasema nisiwasaidie,maana ni ndugu zangu,naomba ajira TAMISEMI,wanachukua wa 2020,2021,wananiacha mimi,naomba sensa,wanapeana kimchongo,sasa hizo pesa eti zije,si zitaliwa tu.....?
Wao wawape nchi nyingine,ila huku,hapana kwakweli,mi sintafaidika kivyovyote vile,this country is corrupt,hata viongozi wake ni corrupt.... wanaila sana hii nchi,nilipofikia hata leo waseme ni mwisho wa dunia,niko tayari,tufe wooote.... labda tukiumbwa upya,kutakua usawa.
Waache waendelee kuikataa katiba mpya,siku wakiikubali nadhani tutafukua makaburi
 
Kabla hawajalipa bara la Africa inabidi elimu zote vichwan mwa wa Africa ziondolew waafrica wabaki na akili zakuzaliwa nazo tu pamoja na viongozi wake I'll tuanze moja kuijenga africa
 
Ifike wakati Sasa Afrika tuungane Katika kutetea masilahi yetu. Linapokuja suala la Afrika lisiachwe liwe la mtu mmoja,au taifa moja.
Afrika tuoneshe kujitambua.View attachment 2325477
Bila kubeza wazo lenyewe; lakini hata leo hii kukitolewa fidia hakuna chochote kitakachobadilika Afrika kwa akili za viongozi waliopo.

Hizo fidia zilizotolewa Ujerumani, Japan na kwingineko haziku'replace' juhudi za wananchi na viongozi wa nchi hizo kujiletea maendeleo wenyewe.
Unaweza kusema, fidia hizo zilikuwa ni kichocheo (mchango) tu wa juhudi za nchi zenyewe zilizofidiwa.

Leo hii akina Samia haipiti siku bila ya kuimba nyimbo za "uwekezaji", wakidhani hiyo ndiyo njia ya kuleta maendeleo hapa; kumbe ni njia ya kuwa na utegemezi zaidi.
Vietnam walifidiwa na nani, mbona wanaendelea mbele zaidi baada ya kuvurugwa kote kule walikofanyiwa?
 
Kuendelea kuzungumza masuala ya utumwa ni kuendelea kumtukuza mzungu na wao wanapenda iendelee hivyo vizazi na vizazi
Tungefutiwa madeni yetu yote kuliko kulipwa fidia maana kama ni pesa tumekuwa tukipewa sana zinaishia kwenye ufisadi
 
Mwl. Nyerere alituasa, ili tuendelee tunahitaji vitu vinne tu - ardhi, watu, siasa safi, na uongozi bora - fedha (fidia) sio miongoni mwa mahitaji hayo. By the way, wasingekuja wazungu (na waarabu) Afrika ingekuwa na hali mbaya sana kuliko iliyo nayo sasa.
Hapo ningeondoa hayo maneno ya mwisho tu; kuanzia kwenye "By the way..."
 
Read the poem to see the impact of Africa colonization
1656996789.jpg
 
Kama ingekubalika natamani mgao ugawiwe kulingana percentage ya athari za ukoloni katika taifa husika
Subiri sensa ipite tuone kila kaya itapata kiasi gani cha mgao. This time hakuna cha vyama wala nini. Wakati mabibi na mababu zetu wanauzwa watemi walikuwa ndo wapanga bei hivyo kama umetoka ukoo wa watemi kaa mbali na mgao wetu.
Naunga mkono hoja.
 
😄😄😄 Wamewatesa Sana Babu zetu na athari zinaendelea kutesa kizazi na kizazi. Wameiba mali nyingi Sana
Mlipwe kwa lipi wakati kila mwaka mnapewa misaada? Naona huyu mchana ameanza kuvimbiwa asali ya urais.
 
Mlipwe kwa lipi wakati kila mwaka mnapewa misaada? Naona huyu mchana ameanza kuvimbiwa asali ya urais.
Hakuna msaada wowote wanaopewa Afrika,ni lugha fulani za kuaminishana upumbavu na kuendelea kuwanyenyekea wazungu. Hakuna misaada halafu iwe na masharti, misaada mingi inatugharimu.
 
Back
Top Bottom