Kama ulikuwepo CCM sasa umeamua kurudi huko naamini ni kwasababu ya mazoea kuliko uhalisia, kusema uliondoka CCM kwasababu ya Magufuli na leo umerudi kwasababu ya Samia ni kujidanganya tu, CCM ni ile ile; jana, leo, na kesho.
Kwako kushinda kwa kuiba kura sio tatizo, usiseme tatizo hilo limeanzia wakati wa Magufuli, nop, limekuwepo miaka yote, huko majimboni wapinzani wamekuwa wakiibiwa ushindi wao kwa wagombea wa CCM kushirikiana na wakurugenzi wa miji na majiji, polisi, na maafisa wa Tume ya uchaguzi, now umerudi huko kufurahia ushindi wa aina hiyo.
Suala la kupigwa na kuumizwa viongozi wa upinzani na wanaharakati wengine; wapo waliouwawa toka enzi za JK akiwemo aliekuwa diwani wa Chadema Usa River Arusha wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani hakuna uchunguzi uliowahi kufanyika, yule Dr. Ulimboka nae yalimkuta wakati huo, sasa leo ukisema unarudi CCM naamini kabisa umerudi huko kuutuliza moyo wako kwa chama unachokipenda kilichokulea, lakini sio kwasababu ya hayo uliyoandika eti yamekuwepo wakati wa Magufuli.
Mwisho kabisa nakushangaa unavyosema imani yako imerudishwa kwa maneno, kwangu nilitegemea imani yako irudishwe kwa matendo ili uwe na msingi mzuri wa kujenga defence yako kurudi CCM, lakini maneno pekee wakati mpaka leo bado wapinzani hawaruhusiwi kufanya mikutano, sheria mbovu bado zipo zikiwemo za vyombo vya habari, hakuna Katiba Mpya, haya yote kwako hayana maana tatizo lako lilikuwa Magufuli tu!