Natarajia Mbowe kupinga utekelezwaji miradi saba ya ujenzi wa barabara kwa njia ya EPC+ F huku bara

..basi iwe ruksa kwa Watanganyika kuajiriwa ktk taasisi za Zanzibar, na kuteuliwa kuwa mawaziri ktk Serikali ya Mapinduzi.

..Wazanzibari na Watanganyika tuwe na haki sawa ktk muungano. Sio sahihi Wazanzibar kuwa na haki zaidi yetu Watanganyika.
Ukifika kwenye ukweli huu, watetezi wote wa huu muungano fake wanapotea.
 
Wakuu bado ninasubiri kauli ya Mbowe kupinga "Wazanzibari" kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara huku bara. Kwa akili zake za kibaguzi nadhani hili pia lilitakiwa limuume na sio bandari tu. Siku nyingine mmiliki wa CHADEMA atafakari sana kabla ya kuropoka. Kauli yake ya kibaguzi ingekemewa sana na hayati Mwalimu Nyerere kama angekua hai. Au ni mbinu yake ya kuikosesha kura CHADEMA 2025? Hata kama kaamua kumuunga mkono Mama Samia ajitahidi kutumia mbinu salama.
Soma hapa chini taarifa ya wizara ya ujenzi na uchukuzi.

BARABARA ZA EPC+ F HAZITALIPIWA

Serikali imesema kuwa utekelezaji wa miradi saba ya ujenzi wa barabara kwa njia ya EPC+ F haitalipiwa na wananchi watakaotumia barabara hizo kama ambavyo baadhi ya wananchi wanavyodhani.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, wakati wa utiaji saini wa miradi hiyo ambayo inatarajiwa kutekelezwa katika Kanda za Kaskazini na Kusini na kujengwa na makandarasi wanne (4).

“Tanzania haina barabara za kulipia mpaka sasa, hivyo upotoshaji unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kulipia kwenye barabara hizi si sahihi kwani barabara hizi ni za kawaida ‘high way’ kama zilivyo barabara nyingine” amesema Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa mradi huu ni wa kwanza na mkubwa kutekelezwa nchini kwani utapita katika mikoa 13 na lengo likiwa ni kuboresha mtandao wa barabara nchini na kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri na usafirishaji ili kuchochea uzalishaji katika maeneo zinapopita barabara hizi na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

“Barabara zitazojengwa zitapita katika mikoa ya Morogoro, Ruvuma, Arusha, Manyara, Dodoma, Tanga, Singida, Mbeya, Songwe, Lindi, Mtwara, Simiyu na Iringa na hivyo zitarahisisha usafiri wa wananchi na usafirishaji wa mazao ya misitu, biashara, chakula, uvuvi na ufugaji, malighafi za madini kama vile makaa ya mawe, grafaiti na Chuma”, amefafanua Waziri Mbarawa.

Aidha, Prof. Mbarawa ametaja miradi itakayotekelezwa kuwa ni ujenzi wa barabara ya Kidatu - Ifakara - Lupiro - Malinyi - Kilosa Mpepo - Londo - Lumecha/Songea (km 435.8) , Barabara ya Arusha – Kibaya – Kongwa (km 453.42), Handeni - Kiberashi - Kijingu - Njoro - Olboroti Mrijo Chini - Dalai - Chambalo - Chemba - Kwa Mtoro – Singida (km 384.33), Igawa - Songwe – Tunduma (km 237.9), Masasi - Nachingwea - Liwale (km 175), Karatu - Mbulu - Hydom - Sibiti River - Lalago – Maswa (km 339) na barabara ya Mafinga - Mtwango – Mgololo (km 81).

Uwezo wako wa kufikiri ukilinganishwa na Mbowe, ni sawa na kulinganisha ewezo wa kutembea kati ya konokono (wewe) na farasi (Mbowe).
 
Huu mtindo wa ujenzi wa barabara ni kama tumejipiga bao wenyewe. Mtu mjinga wa aina yako ndio hajui madhara ya ujenzi wa aina hiyo.
Wewe mjanja umeweza kujijengea nini chako binafsi?
 
Tanganyika ilipata Uhuru 9-12-1961, na nyerere akawa waziri mkuu baada ya mwaka mmoja 9-12-1962 ikawa jamuhuri Nyere akawa Rais wa Kwanza waTanganyika. Nchi iliyopata Uhuru kwanini isiwepo?
Labda kama umeamua kujitoa akili ndo utakuwa hujui kama Tanganyika haipo.
 
..basi iwe ruksa kwa Watanganyika kuajiriwa ktk taasisi za Zanzibar, na kuteuliwa kuwa mawaziri ktk Serikali ya Mapinduzi.

..Wazanzibari na Watanganyika tuwe na haki sawa ktk muungano. Sio sahihi Wazanzibar kuwa na haki zaidi yetu Watanganyika.
Jokakuu ina maana huelewi kwanini Tanganyika na Zanzibar ziliungana?
 
Ufafanuzi mleta mada hautoshi

Source ya ku finance hizo barabara ni ipi? Ukijenga hoja maliza kila kitu kuepuka hicho kiitwacho upotoshaji

Hizo barabara kujenga source inatoka wapi na je kuna masharti yeyote?

Sometimes mnawapa Room upinzani kwa kuto kuwa elaborative enough

Hizo pesa ujemzi wake pesa zinatoka wapi ?
 
Wakuu bado ninasubiri kauli ya Mbowe kupinga "Wazanzibari" kutekeleza miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara huku bara. Kwa akili zake za kibaguzi nadhani hili pia lilitakiwa limuume na sio bandari tu. Siku nyingine mmiliki wa CHADEMA atafakari sana kabla ya kuropoka. Kauli yake ya kibaguzi ingekemewa sana na hayati Mwalimu Nyerere kama angekua hai. Au ni mbinu yake ya kuikosesha kura CHADEMA 2025? Hata kama kaamua kumuunga mkono Mama Samia ajitahidi kutumia mbinu salama.
Soma hapa chini taarifa ya wizara ya ujenzi na uchukuzi.

BARABARA ZA EPC+ F HAZITALIPIWA

Serikali imesema kuwa utekelezaji wa miradi saba ya ujenzi wa barabara kwa njia ya EPC+ F haitalipiwa na wananchi watakaotumia barabara hizo kama ambavyo baadhi ya wananchi wanavyodhani.

Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa, wakati wa utiaji saini wa miradi hiyo ambayo inatarajiwa kutekelezwa katika Kanda za Kaskazini na Kusini na kujengwa na makandarasi wanne (4).

“Tanzania haina barabara za kulipia mpaka sasa, hivyo upotoshaji unaosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kulipia kwenye barabara hizi si sahihi kwani barabara hizi ni za kawaida ‘high way’ kama zilivyo barabara nyingine” amesema Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amesisitiza kuwa mradi huu ni wa kwanza na mkubwa kutekelezwa nchini kwani utapita katika mikoa 13 na lengo likiwa ni kuboresha mtandao wa barabara nchini na kuongeza ufanisi katika sekta ya usafiri na usafirishaji ili kuchochea uzalishaji katika maeneo zinapopita barabara hizi na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.

“Barabara zitazojengwa zitapita katika mikoa ya Morogoro, Ruvuma, Arusha, Manyara, Dodoma, Tanga, Singida, Mbeya, Songwe, Lindi, Mtwara, Simiyu na Iringa na hivyo zitarahisisha usafiri wa wananchi na usafirishaji wa mazao ya misitu, biashara, chakula, uvuvi na ufugaji, malighafi za madini kama vile makaa ya mawe, grafaiti na Chuma”, amefafanua Waziri Mbarawa.

Aidha, Prof. Mbarawa ametaja miradi itakayotekelezwa kuwa ni ujenzi wa barabara ya Kidatu - Ifakara - Lupiro - Malinyi - Kilosa Mpepo - Londo - Lumecha/Songea (km 435.8) , Barabara ya Arusha – Kibaya – Kongwa (km 453.42), Handeni - Kiberashi - Kijingu - Njoro - Olboroti Mrijo Chini - Dalai - Chambalo - Chemba - Kwa Mtoro – Singida (km 384.33), Igawa - Songwe – Tunduma (km 237.9), Masasi - Nachingwea - Liwale (km 175), Karatu - Mbulu - Hydom - Sibiti River - Lalago – Maswa (km 339) na barabara ya Mafinga - Mtwango – Mgololo (km 81).
Kweli kabisa maana haitekelezwi Zanzibar! Asipoipinga atakuwa si mtu wa kuaminika kwa kuwa ni wazanzibar hao hao aliowapinda kwenye ishu ya DP WORLD ndo wanajenga hizo barabara bara na si Zanzibar.
 
..basi iwe ruksa kwa Watanganyika kuajiriwa ktk taasisi za Zanzibar, na kuteuliwa kuwa mawaziri ktk Serikali ya Mapinduzi.

..Wazanzibari na Watanganyika tuwe na haki sawa ktk muungano. Sio sahihi Wazanzibar kuwa na haki zaidi yetu Watanganyika.
Muungano mimi binafsi nauona umekaa kihuni sana, mwl alikurupuka sana kutokuweka mizania baina na nchi mbili, kwa hii hoja yako sina comment. Lakini siafiki mtu kusemwa vibaya kwa kuangalia asili yake, wamepita watanganyika wangapi ikulu na wakaiingiza nchi kwenye mikataba ya hovyo kwanini hatukukosea asili zao?

Mjadala wa bandari ungelenga zaidi kukosoa mkataba wenyewe badala ya kuanza kuwaatack watu personally.
 
..waliomsema Samia wamekosea.

..lakini ukweli lazima usemwe kwamba Prof.Mbarawa ni Mzenj na hastahili kuongoza wizara isio ya muungano.

..pamoja na hayo hata wizara ingeongozwa na Mtanganyika bado Samia ingeipiga bei bandari.
 
Jokakuu ina maana huelewi kwanini Tanganyika na Zanzibar ziliungana?

..yanayotokea yanafanya watu wauchukie muungano.

..Watanganyika na Wazanzibar wakiwa na haki sawa, na fursa sawa ndani ya muungano, malalamiko yatapungua, kama sio kwisha kabisa.
 
Kweli kabisa maana haitekelezwi Zanzibar! Asipoipinga atakuwa si mtu wa kuaminika kwa kuwa ni wazanzibar hao hao aliowapinda kwenye ishu ya DP WORLD ndo wanajenga hizo barabara bara na si Zanzibar.

..EPC+F ikitekelezwa Zanzibar, atakayelipa deni ni Tanganyika.
 
Back
Top Bottom