Nategemea kwenda Shinyanga kwa pikipiki aina ya Boxer, CC 125

Kwanini ujichoshe hivyo ndugu maaana mafuta si chini ya laki moja gharama ambayo unakata ticket unapanda bus KATALAMA na pikipiki inapanda roli, unafika shinyanga vizuri unaanza kata mitaa safi jioni unatembelea the deez pale unashangaa sukari za shy town
 
Unataka kujitafutia shida zisizo na msingi mkuu hivi unajua kama pikipiki inachosha tulikuwa tunazitumia Tabora , Singida na Dodoma kwenda kwenye minada unakodi 10,000 kwa siku unaendesha mwenyewe km 60 kuingia ndani. Ukirudi kama umepigwa magongo kuna mwenzetu yeye ndo alijifanya mpori mpori aliumwa kifua mwezi mzima na homa. Sasa sembuse 750 go and return 1,500 Km plus za kuzunguka.
 
Dar-Shy ni 1000km kasoro kidogo.
 
We nenda kuna mmoja yeye kaenda musoma na sasa anatumia mtambo bila wasiwasi
 
shukrani sana....kibwa bajeti yangu ni ndogo bila hivyo siwezi kumudu masafa ya huko kwani nikifika nategemea kuzunguka sana...hivyo nilidhani kwenda na pikipiki yangu kutaniepushia gharama za nauli huko vijijini...
Pikipiki ya 125cc inafanya vizuri masafa hata ya 1000km. Boxer na Tvs zina mfumo wa Timing chain zina utulivu.

Pikipiki za mchina zilipoingia GN/CG 125 kuna watu mpaka leo wanasafiri zaidi ya 700km per day kwa kutumia bike za kichina.
 
Hitimisho lako lina maana aachane na hayo mawazo yake ,apande basi
 
wewe: ulale vizuri unywe maji na uwe na vitu vya kufikiria kwa hayo masaa 10-12 utakayotumia peke yako njiani

safety gears: uwe na helmet sahihi inayofunika
kichwa kizima, yenye shades za jua sio
hizi za 50k kushuka chini. koti na suruali ya mvua, koti na suruali ya kusafiria, na ndani za kuzuia baridi kama sweater. gloves ukipenda. viatu vigumu lakini comfortable shoes, sbb ya upepo beba kitu cha kuzuia kelele cha maskio, dont overdress, be comfortable.

service: service pikipiki vizuri na kagua kila
kitu, paka nati zilizolegea

mafuta: weka mafuta sheli sahihi, na dadisi sehemu gani kuna umbali mkubwa bila sheli
ikibidi uwe na lita 1/2 ya akiba umebeba

stops: full tank inaweza kupa 250-300km. pumzika nusu saa kila full tank ukijaza. kila
ukisimama jinyooshe na unywe na kula vitu light, ukila shibe sana utaanza kusinzia.

njia: kama ni njia mpya kwako, tumia
google maps ikusaidie usijepotea

speed: kwa boxer cruise at 70-90km/hr,
zaidi utaichosha engine maana ni natural
cooled, pia kagua temp au taa yoyote ya alarm
kama inayo.

mvua: angalia weather forecast, kama
mwezi ujao mvua zita anza ni hatari na kero
kuendesha pikipiki kwenye mvua

vibrations: pikipiki ndogo ina vibrations kubwa kwa umbali mrefu uta anza kuskia tofauti kdg, 200-300km ni kawaida, zaidi ya hapo hali inabadilika either ganzi au kupoteza mawasiliano, boresha kiti au vaa sponge trouser

distance: dar shy ni karibu 980km, utatumia 12hrs au zaidi kwa spidi ya boxer (less than 100kph), ukifika dodoma jikague kama uendelee au upumzike hadi kesho yake.

vifaa: beba maji kdg, spana za muhimu, ya kuzibia pancha na pump ndogo ya mkono, ubebe pia nyaraka za pikipiki. beba na kitambulisho au note ata yenye mawasiliano ya watu wako wa karibu ikitokea chochote

donts:
-usiendeshe usiku, kabisa
-usibebe mizigo zaidi ya kibegi cha mahitaji muhimu
-sio mashindano boxer ni pikipiki ndogo, fanya kama unaenda posta tu.
-dont drink

jumla: kama ni adventure usiende mwenyewe tafuta company, au usiende mbali sana (moro panatosha), kama ni kuipelekea shy ipakie lorry tu, kama ni uharaka na adrenaline hutawahi ni shughuli ya siku nzima especially kwa
boxer, kama we sio mvumilivu baada ya km 200 tu utajiuliza sana nani alikutuma ufanye hio safari..
 
πŸ™† Asante sana ndugu. Yangu umenifafanulia vizuri sana..😁😁😁
 
Boxa ilivyo fupi utaumia mgongo bora ungekuwa na kitu XL,900km myb kama unaenda na haurudi.
 
Achana na mambo ya pikipiki [emoji2509] lipa nauli utanishukuru badae, nilishawahi kutembea mwaka 2011 umbali wa km 320 sitasahau. Wenye mabasi wana dharau sana, watakuja wakupitie karibu unakuwa mtumwa barabarani. Af ukichoka sana unaanza kuona mauzauza mara usingizi, kumbuka kanda ya ziwa saiv kuna mvua. Singida pale upepo mkali, Nzega mvua, n.k hilo ni moja.
Kingine gharama itakuwa mara 2 au zaidi ya basi.
Boxer inatumia lita 1 kwa km 40/saa ukiwa speed 60/saa na kuendelea. Inatumia lita 1 kwa km 50 - 60 endapo utaendesha chini ya speed 40/saa pia inategemea ufundi wa kuendesha na kubana mafuta kwenye miteremko. Kumbuka hapa ukiwa unapumzika kila mara pikipiki haichemki. Ukienda umbali mrefu ikachemka inafyonza mafuta balaa, mengine yana evaporate na joto

Maana yangu ni kuwa utatumia 750/40 sawa lita 18.5 ~ 20. Wastani wa bei ya petroli ni 3300. Kwenda utatumia kama 66,000 bila service ya pikipiki. Kuna vifaa vitalika pikipiki inabadilisha sauti ukirudi unaanza majanga. Mengine jiongeze
 
Roughly utatumia full tank 4(pikipiki huchoma mafuta sana 80kmph- 120kmph hasa hizo za cc110,125,150).....
Dar-shy ni 900+km si 750km
Kwahiyo full tank
Lita 12@3200-> 38,400*4 = 153,600/=

Madekenya kusafirisha pikipiki 100,000
Usafiri ally star dar-shy 60,000
Total 160,000/=

So angalia if its worth it, fanya maamuzi
Itakayoumia ni familia yako πŸ˜‚πŸ˜‚(nakutania)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…