1. Kumekucha!
2. Huku kuna watoa misaada kawauwa kwa makusudi, kule kuna jingine na Iran linatokotoka vilivyo; kavunja Geneva convention kwa kushambulia consulate ya wengine ugenini.
3. Alimradi mwana mkaidi kazini!
4. Sasa amri anayoielewa vyema imeshatoka; tena ya babaake kutokea white house ya Marekani: "Vita vikome mara Moja!!"
5. Aungurumapo Simba mcheza nani?
6. Kwamba kumbe watoa misaada wale wakiwa kwenye msafara wa magari matatu, yenye reflective logo (WCK) kubwa za wazi zinazojulikana; zikiwa juu na chini, mbele nyuma na pembeni; IDF wakijua wapo walipokuwa muda ule, waliwarushia makombora matatu kuwauwa; moja baada ya jingine!
7. Kwamba kumbe baada ya gari ya mbele kupigwa, mbili za nyuma zilifika kuwachukua wahanga, ambazo nazo zilikuja kupigwa moja baada ya nyingine; tena punde tu kila walipo maliza kuwaweka wahanga kwenye gari zilizobakia au iliyobakia?
8. Kwamba gari ya mwisho ilipigwa baada ya kuwa imekamilisha kuwachukua wahanga kwenye gari mbili zilizopigwa mwanzo?
9. Kwamba kumbe katika muda wote huo walikuwa kwenye mawasilisho ya moja kwa moja (real time), kuwa: "kulikoni mwatuuwa?"
10. Kwamba kulikuwa na umbali wa angalau 500m kutokea gari moja hadi nyingine baada ya kupigwa?
11. Looh! Ni mwenda wazimu pekee anayeweza kukubaliana na hadithi za Natenyahu za bahati mbaya.
12. Joe Biden anazo sababu zote za kukereka, kwani Kwa hakika ukimwendekeza mbwa atakufuata hadi madhabahuni!
Ama kwa hakika: "la kuvunda halina ubani."