Niko bush sehemu yenye tatizo la network, sipati habari kwa mtiririko mzuri. Ila nashauri sana kwa sasa tuko kwenye kampeni, Lisu anapaswa kufanya siasa za kupata uungwaji mkono wa umma zaidi kuliko siasa za madhila aliyopitia. Nashauri sana Lisu azungumzie mahitaji ya wananchi kwa 80%, kisha madhila yake na ya upinzani ayaongelee kwa 20% tu.
Kushinda pambano la ngumi sio uwezo wa kurusha ngumi nzito pekee, bali ni kurusha ngumi nzito zenye pointi. Ni vyema Lisu asitumie approach aliyoitumia wakati anasaka wadhamini, bali atumie approach ya kuweka mahitaji na shida za wananchi kwanza. Inatakiwa hata akishindwa awe ameacha ahadi za uchonganishi, ambazo zitawafanya kutekeleza hata kama hawapendi.